Jinsi Watumishi wa Serikali wanavyotumiwa kama uchochoro wa kupiga fedha za miradi

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
476
1,244
Watumishi wengi wa serikali hasa watumishi walioajiriwa kwa taaluma yao serikalini ni waadilifu ni wachache sana ambao si waadilifu katika kusimamia miradi ya maendeleo

Wafuatao ndiyo wanapiga fedha za miradi kwa kutumia watumishi wa serikali na mtumishi anapojaribu kuhoji hii kitu imekaaje huambulia vitisho vya kushushwa cheo, kupigwa adhabu kwa kuhamishwa kwenda mazingira magumu au kutungiwa kesi na wengi wanaogoma huambulia demotion ya wakurugenzi na wakuu wa Idara

1. Wakurugenzi wa Halmashauri, hawa watu wengi wao wanapopewa kazi hii wanataka utajiri wa haraka hivyo hushirikiana na manunuzi kutafuta wazabuni kwa gawio la percentage kadhaa, hivyo wenye miradi hupewa majina ya wazabuni ambao unapaswa kuchukua vifaaa,mfano kama mradi utatumia milioni 200 kununua vifaa basi mzabuni atatakiwa kupandisha bei ya vifaa hivyo mkurugenzi apate kiasi fulani kwenye miradi, fikiria mkurugenzi amepokea bilioni 20 kwa ajili ya miradi, mkurugenzi atahakikisha anaondoka na milioni 500 za mradi kwa janja janja nyiiingi ,( Utajiri wa haraka baada ya kusota mitaani)

2. Madiwani nao ni miongoni mwa wanaolazimisha watumishi wanaosimamia miradi kupiga fedha za miradi mfano, Diwani anahitaji anayesimamia shule au zahanati inayojengwa ampe kitu kidogo ili asifuatilie kila kitu kwenye mradi,endapo mtumishi amegoma Diwani huunda zengwe la kutafuta kasoro yoyote kwenye mradi ili mtumishi huyu apate dosari na ikibainika mtumishi ana dosari ya mradi Diwani hutumia njia hiyo kupata kiasi fulani kutokana na mradi unaoendelea

3. Wakuu wa Idara, licha ya watu hawa kuwa ni watumishi wa serikali, hawa watu wakishaona mkurugenzi amepata kiasi fulani kwenye mradi na wao hawatulii, hutumia mbinu mbalimbali ili nao wapate kidogo mbona boss amepata kwa nini isiwe sisi ?

4. Kamati za siasa za CCM Wilaya nazo zinashiriki kupora fedha za miradi, ikiwa mradi unaanzishwa sehemu fulani mara moja Kamati ya siasa ya ccm huanza kupitapita na kuweka vitisho kwenye miradi, endapo kule juu wameishamega kifungu fulani kwenye mradi kwa vyovyote mradi nao utaanza kuyumba, matokeo yake Kamati ya CCM ikipita nayo ili itulie itaanza kudai chao ili huyu mtumishi anayesimamia mradi asichukuliwe hatua kali na chama

Reference: Mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Magoma, Halmashauri ya Tarime DC
 
Back
Top Bottom