Jinsi ninavyo design (+ kanuni za design) Ep. 01: 3 bedroom house #01

HENRY14

JF-Expert Member
May 13, 2021
2,367
4,415
TENGERU HOUSE

Habari zenu.

Nikiwa mdau wa ubunifu na usanifu majengo, nimeona niwashirikishe kwa ufupi namna mimi na baadhi ya wasanifu majengo tunavyofikia utekelezaji wa majengo na bidhaa tunazobuni. Nitatumia design yangu ya nyumba ya vyumba vitatu isiyo ya ghorofa iliyobuniwa kuwa Tengeru, Arusha. Huko mbele nitawaleea mifano mingine niliyodesign yenye approach tofauti tofauti.

Natumaini uzi huu utawasaidia wanaotamani kujenga kwa kujifunza baadhi ya kanuni za wabunifu na kupata machache yanayohusika katika ubunifu wa nyumba zao na bidhaa nyingine. Huenda kuna ambao watajifunza na kutumia vitu hivi katika kazi zao. Pia nimeona ni vema kupata feedback kutoka kwa wengine na kujifunza kutoka kwao pia. Hii kazi ni ‘work-in-progress’.

Tutaanza na michoro, kisha tutaichambua. Nitatumia michoro michache tu kwanza: Ground Floor Plan, Cross Section na Elevations.

Mimi napenda kusema kuwa designs zangu zina taratibu kuu mbili, nazo ni:

1. Concept Design

2: Design Development


Japo ni muhimu kuelewa kuwa hizi taratibu huingiliana kila wakati na inawezekana kusema kiuhalisia ni utaratibu mmoja tu uitwa designing, na kwa wengine hizi taratibu zimegawanyika zaidi na wao wana taratibu mpaka nne na zaidi ila kwa ajili ya huu uzi na kuweza kuelewesha umma vizuri zaidi nitatumia hizi zangu mbili.

Hii design kwa sasa bado iko katika Concept Design stage.

Kwa kifupi:

Concept Design inaanza na brief ya mteja, ikifuatiwa na site analysis na building design kwa hatua za awali. Hapa tutazungumzia Plans, Sections, Elevations na ikibidi 3D models na BIM na Renderings. Nitajitahidi kueleza zaidi kipengele hichi maana ndicho watu wengi hujali.

Design Development ni muendelezo wa concept design, ikijumuisha construction drawings (ambayo fundi anapewa kujengea), ikibidi michoro ya Structural Engineer, Services Engineer, makadirio ya Quantity Surveyor, michoro ya kuombea vibali kwa mamlaka mbali mbali, details mbali mbali, schedules, nk. Kwa kawaida ujenzi wa nyumba za watu binafsi hazifiki stage hizi sana. Wengine hata sketch ya kwanza tu wanaingia nayo site na kujenga. Nitajitahidi kuelezea vyote hivyo kwa manufaa ya umma.


Ifuatayo ni michoro ya nyumba kama ilivyofika hadi sasa…

TENGERU HOUSE _GROUND FLOOR PLAN.jpg

Fig. 1: TENGERU HOUSE_ Ground Floor Plan


TENGERU HOUSE.jpg

Fig 2: TENGERU HOUSE_Cross Section



TENGERU HOUSE_ELV 1 AND 2.jpg

Fig 3: TENGERU HOUSE_Elevations 1 & 2


TENGERU HOUSE_ELV 3 AND 4.jpg

Fig. 4: TENGERU HOUSE_Elevations 3 & 4.

Baada ya kuangalia michoro, sasa twende kwenye maelezo.

1. CONCEPT DESIGN:

A. Project Brief:


Project ama Client’s brief ni maelezo ya mteja anataka nini. Mteja wangu alitaka kwanza nyumba yenye bedrooms tatu za kufanana kila kitu na zote ziwe self-contained, hivyo hakutaka specific master bedroom. Alipendelea vyumba vyote viingilike na kutokea kwa nje pia. Pili alitaka ‘open concept’ kwa jiko, dining room na lounge. Maongezi na mteja yanamjulisha designer juu ya aina ya maisha, ‘lifestyle’ ya mteja na anavyotarajia kuishi katika jengo. Je anafamilia kubwa? Je ni mpenzi wa gardening au ufugaji mdogo mdogo ama anapenda kusoma na kufanya kazi nyumbani? Majadiliano haya yaliniruhusu kupendekeza baadhi ya vitu ambavyo vingeweza kuongeza thamani ya nyumba yake na kuweka chachu kwa lifestyle yake tarajiwa. Hatimae tulishauriana kubuni nyumba itayofaa kuwa ‘Bed n Breakfast’ pia.

B. Site Analysis

Kiwanja, site, ni cha mstatili, flat, chenye barabara upande wa kusini na kimezingirwa na viwanja vingine vya majirani pande za mashariki, kaskazini na magharibi. Upande wa Kaskazini una ‘view’ ya Mount Meru, ingawa si ya kutegemea kwa sana kwa sababu ya udogo wa eneo na uwezekano wa jirani wa upande wa kaskazini kuja kujenga ghorofa kubwa baadae. Hivyo kwa haraka haraka, design ilitaka ‘views’ zijitengeneze zenyewe ndani ya kiwanja. Ukijani, ‘greenery’ ama garden kwa wingi iwezekanavyo na nyumba iwe ‘outward facing’, yaani kutafuta namna ya kuelekeza macho ya walio ndani nje kwenye gardens nzuri. Design ikaanzia hapa hapa.

Mimi ni mpenzi wa art na ni mchoraji pia hivyo nikapendekeza kuwa na kuta na platforms zitazoweza kuwa na picha, vinyago, nk. Hapo kichwani tayari nikawa nimepata ‘concept’ ya nyumba hii. Kwa sababu mteja alishapendekeza vyumba vya kulala viweze kuingilika kwa nje, nikamalizia kwa kutaka vyote view na baraza ‘veranda’ za kupumzikia, kama hotel.

B. 1. Site organization.

Kwa kuwa nilishaanza kupata wazo kwa mbali la nyumba itakuwa ya namna gani, ninagawa site kwa ‘zones’ kadhaa. Hii inaangalia ‘access’ yaani site iingiliwe kwa wapi, wapi nyumba ikae na kwa muelekeo upi. Jengo likaka kwa katikati ya site, likijaa zaidi kwa upande wa mashariki na kwa upande wa kaskazini. Hii ni kwa kutengeneza gardens mbili kubwa, moja kaskazini kwa ajili ya vyumba, ya pili kusini ambapo patakuwa mbele, kwa ajili ya sebule na baraza ya mbele.

Niliona kutakuwa na jengo dogo la pembeni, service building, ambalo litakaa kona ya kaskazini na magharibi. Hili litakuwa na jiko na stoo pamoja na bafu. Ikibidi hata chumba kidogo cha kulala pia. Uwanja wa kati ya nyumba na hili jengo la services litatumika kama laundry yard pia. Nguo zikianikwa hapa zisionekane kwa mbele ya nyumba. Shughuli za kijamii za Kitanzania ziweze kufanyika hapa pia bila kuonekana kwa mbele (mf. Mapishi kwa ajili ya sherehe mbali mbali, upasuaji wa kuni na uchinjaji wa mbuzi, nk). Eneo hili ni muhimu sana kama maeneo mengine, ingawa kwa bahati mbaya designs za nyumba zetu nyingi hazizingatii eneo hili (matokeo yake kijana fulani anakuja kwako kutoa posa na mshenga wake anakuta baraza la mbele kuna wamama wanapeta mchele, kwenye mlimao ulio garden ya mbele kuna mbuzi kaning’inizwa anachunwa ngozi, kwenye parking yamewekwa mafiga na supu inachemka…mifano ni mingi ila tuachane nayo kwa sasa).

Geti la kuingilia likaamuliwa liwe karibu na upande wa magharibi, driveway iishie kwenye parking area na hapo hapo kuwe na access ya ‘uwani’ ama ‘kitchen yard’ ili iwe rahisi kwa wenyeji na mizigo ya sokoni, nk. kuweza kufika jikoni na store bila kupitia kwenye nyumba. Hii ‘yard’ inafichwa na ukuta ama screen. Hapo hapo pia ni rahisi kufika main entry.


Diagram ya chini inaelezea mpangilio wa kiwanja.


View attachment TENGERU HOUSE _SITE ORGANIZATION EXTENDED.jpg
Fig 5: TENGERU HOUSE: Site Organization-extended


TENGERU HOUSE _SITE ORGANIZATION CLOSEUP.jpg


Fig 6: TENGERU HOUSE: Site Organization_Closeup

Mpangilio mzuri wa site unapelekea matumizi mazuri ya ardhi, urahisi wa upangaji wa materials na huduma wakati wa ujenzi, hali nzuri ya mazingira na gharama nafuu ya baadhi ya vitu vya ujenzi (mf. Paving).

C. Building Design

Baada ya kupangilia site na kujua kwa kiasi nini kinaenda wapi, design ya nyumba ni rahisi.

Hii imegawanika mara mbili;

Private zones, zikiwemo vyumba ya kulala na vyoo, public toilet na scullery.

Public zones; zikiwemo baraza la mbele, dining. Lounge na outdoor lounge. Kitchen iitwe ‘semi-public’ ingawa imeungana moja kwa moja na dining.

Awali niligusia kuhusu ‘plan’, ‘section’ na ‘elevations’. Huwa nasema designer mzuri ni yule anayejua kudesign in plan. Designer mzuri zaidi anajua kudesign ‘in section’. Designer mzuri haswa au mkali, anajua kudesign ‘volumetrically’.

Note: nazungumzia ku ‘design’ na siyo kuchora au kudraft. Mtaani tunakutana na kazi nyingi sana zilizochorwa ila haziko designed, au design ni dhaifu.

Nyumba hii imedesigniwa ‘kwa plan’ na ‘kwa section’ na pia ‘kwa elevation’. Hizi huingiliana sana na si ajabu ‘plan’ kubadilishwa kwa sababu ya design ya ‘elevation’ ama ‘section’ na hivyo hivyo kwa vingine.

‘Concept’ ya nyumba hii ni nyepesi; Public na Private areas zimegawanywa ukuta. Ukuta huu nauita ‘ANCHOR WALL’. Ukuta huu ndio msingi wa concept hii kote kwa ‘plan’ na kwa ‘section’.



Tuanze na plan.

C.1 PLAN

Rejea ramani yetu ya awali (Fig. 1) na diagram hii:

TENGERU HOUSE _PUBLIC AND PRIVATE.jpg

Fig 7: TENGERU HOUSE: Public vs Private spaces.

Diagram hii inaonesha hii ANCHOR WALL (Nyekundu) ikitenga ‘public’ na ‘private’ areas, ikipunguza au kuondoa corridors na kuficha milango ya vyumba. Hakuna vyumba vinavyofungukia private areas moja kwa moja. Pia ina ‘anchor’ na kushikilia baadhi ya vitu muhimu kama makabati na meza za kusomea za vyumbani, counter na fridge za jikoni, fireplace za sebuleni na nje na ledges. Huu ukuta umekuwa ‘multifunctional’ na ndio ukuta mkuu wa kuweka TV na sanaa mbali mbali. Kwa namna hii unajihalalisha kuitwa ‘anchor (nanga)’ wall na kuipa nguvu ‘concept’.

Plan pia imezingatia ‘outward facing’ concept. Vyumba vyote na sebule vina access ya garden na vinajifungua kwa views na kuleta mazingira ya nje ndani kupitia madirisha makubwa (kuta za baraza ni za kioo na grilles) ili mtu hata akiwa ndani ajihisi kama yuko nje.

TENGERU HOUSE _OUTWARD FACING CONCEPT.jpg

Fig 8: TENGERU HOUSE_Outward-facing Concept.

Kingine ni ‘flow’ ya kutoka nje hadi ndani na ya ndani kwa ndani. Kitchen inahusiana na Dining lakini pia na Scullery na Scullery inahusiana na Parking area na Laundry/Kitchen Yard, ambayo inahusiana na Service building. Dining inahusiana na Kitchen na Lounge na Veranda nk. Kuna ‘implied corridor’ inajitengeneza baada ya ukuta na ledge, ambayo ndiyo inasaidia kujua furniture zitapangwaje mpaka hata taa za ukutani na ceiling zitawekwaje.


TENGERU HOUSE _IMPLIED CORRIDOR.jpg

Fig 9: TENGERU HOUSE: Implied corridor


Baada ya kutafakari haya katika kudesign, asilimia kubwa ya ‘general planning’ inakuwa imekamilika na tunaanza kuangalia ‘specifics’ kama vipimo, furniture layout, kitchen layout, bathroom layout nk. Kwa mfano, concept ya design ya makabati ya vyumbani ni kwamba yakae kwenye ‘Anchor Wall’ na yawe na bookshelf baada ya mlango, yawe na sehemu ya nguo na viatu katikati na kisha kuwa na meza ya kusomea mwishoni. Hapo hapo panaweza kuwa na laundry basket, connections za TV au data, nk. Kunakuwa hakuna haja ya kuwa na furniture nyingi chumbani. Hapa mtaona ile concept ya ‘anchor wall’ inavyoendelea kuwa explored na stretched.

Tunaweza kughairisha analysis yetu ya plan hapa kwa sasa. Ni tumaini langu kuwa kuna kitu mmepata mpaka hapa.


Tutaendelea….
 
Boss msingi wake unaweza chukua kiasi gani??? Kama site ni flat.
Kwa sasa siwezi kujua boss (mimi siyo quantity surveyor na huwa napendelea wao wafanye hesabu hizo) ila nikitulia nitaweza kufanya mahesabu ya kukadiria kwa kiasi fulani.
 
Asante sana mkuu. Hapa nimeweka chache tu muhimu. Nadhani lecturer anataka kuona kama mwanafunzi anaelewa anachofanya 😄😄😄
Good job imenikumbusha studio work lecturer anataka aone process zote hizo 😁😁😁
 
Kwa mara ya kwanza nimekutana na andiko la uchoraji ramani za nyumba lililonielimisha!!
Asante mkuu. Nafikiri ni vizuri Watanzania wengi zaidi wakijua juu ya basics kadhaa za uchoraji na design. Asilimia ndogo sana ya watu wanaojenga nyumba zao hutumia wasanifu majengo. Wale wengi wasiowatumi wakipata elimu kidogo nao wanaweza kujijengea makazi bora zaidi na jamii Kwa ujumla ikawa inaishi kwenye makazi na mazingira bora zaidi. Hatimae jamii inastawi vizuri zaidi.
 
Kazi nzuri Sana mtaalam.

Lakini ningeshauri hapo sitting TV ikawa upande ambao movement flow ya watu haiingilii visibility ya watu kwenye TV..

Yaan kitaalam naweza kusema sitting room Iko less furnishable.

Yote kwa yote, design imetulia Sana. Hongera kwa kazi nzuri
 
Kazi nzuri Sana mtaalam.

Lakini ningeshauri hapo sitting TV ikawa upande ambao movement flow ya watu haiingilii visibility ya watu kwenye TV..

Yaan kitaalam naweza kusema sitting room Iko less furnishable.

Yote kwa yote, design imetulia Sana. Hongera kwa kazi nzuri
Asante sana mkuu.
Kuhusu TV...niliona hapo ilipo ndiyo ideal Kwa sababu lounge hii imekaa ki 'social' ama 'conversational' zaidi. Priority ni watu waweze kukaa na kuzungumza (ndiyo maana pia niliweka window seat dirisha kubwa la mashariki). Kwa movements hapo labda ni Kwa wanaoenda vyumbani ambazo siyo movements nyingi sana. Ingekuwa karibu na dining ambapo Kuna movements za jikoni na chumbani na public toilet (especially kama Kuna wageni) labda ingesumbua kidogo. Inaweza pia kukaa ukuta wa kusini Kwa kusimamishwa kwenye stand mbele ya pazia. Shukran sana mkuu
 
Asante sana mkuu.
Kuhusu TV...niliona hapo ilipo ndiyo ideal Kwa sababu lounge hii imekaa ki 'social' ama 'conversational' zaidi. Priority ni watu waweze kukaa na kuzungumza (ndiyo maana pia niliweka window seat dirisha kubwa la mashariki). Kwa movements hapo labda ni Kwa wanaoenda vyumbani ambazo siyo movements nyingi sana. Ingekuwa karibu na dining ambapo Kuna movements za jikoni na chumbani na public toilet (especially kama Kuna wageni) labda ingesumbua kidogo. Inaweza pia kukaa ukuta wa kusini Kwa kusimamishwa kwenye stand mbele ya pazia. Shukran sana mkuu
Pamoja Sana Architect
 
Asante sana mkuu.
Kuhusu TV...niliona hapo ilipo ndiyo ideal Kwa sababu lounge hii imekaa ki 'social' ama 'conversational' zaidi. Priority ni watu waweze kukaa na kuzungumza (ndiyo maana pia niliweka window seat dirisha kubwa la mashariki). Kwa movements hapo labda ni Kwa wanaoenda vyumbani ambazo siyo movements nyingi sana. Ingekuwa karibu na dining ambapo Kuna movements za jikoni na chumbani na public toilet (especially kama Kuna wageni) labda ingesumbua kidogo. Inaweza pia kukaa ukuta wa kusini Kwa kusimamishwa kwenye stand mbele ya pazia. Shukran sana mkuu
Vipi uko Arusha
 
Back
Top Bottom