Jinsi nilivyotumia Tsh. Milioni 1 kuzalisha faida ya Tsh. Milioni 10 ndani ya miezi kumi

Ligaba

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
1,045
2,821
Onyo:
Usijaribu nilichokifanya kama huna ozoefu katika biashara hasa katika kipindi hiki kigumu cha Covid-19.

Tuanze na maelezo.

Je Umeshawahi kucheza ule upatu wa uswahilini ule wa kuchanga hela kila baada ya muda na mmoja anachukuwa kwa mzunguko? Na je unautumiaje na unawezaje kurejesha fedha za mzunguko?

Soma kisa changu.

Mwaka Jana mwezi wa tano kuna rafiki yangu alinitafuta na kunijulisha kuwa wapo 9 members wanataka kuchangiana kila mwezi 1M na fedha atapewa mmoja na target iwe miezi kumi ili kila mmoja ameet dreams zake, hivyo kama nitaweza nijoin.

Nilimkubalia ila kwa masharti kwa vile yeye ndiye anawafahamu na kwa nature ya shughuli yangu biashara nitaomba niwe wa kwanza kupokea ili nisizohofishe biashara zangu. Nilipomuuliza juu ya hao wengine aliniambia wote ni wafanyakazi wenye vipato vya kutosha kutoa hiyo 1M pasipo kuyumba.

Baada majadiliano tukapanga siku tukutane wote 10 na tukaandika muhtasari wetu wa makubaliano na mwezi ambao kila mmoja atachukua na tutakubaliana kila mmoja atachukua kwa maandishi na muundo Fulani hivi wa kisheria.

Nikakubaliwa kuwa wa kwanza kwa nature za shughuli zangu za biashara. Miongoni mwa hao members kulikuwa na washkaji wa Bandari, Doctors na michanganyiko mingine yenye kipato cha wastani ila wengi hawakuwa na ndoto za biashara.

Mwisho wa mwezi May 2019 nikakabidhiwa fungu la 10M ikiwa na pamoja na million yangu na zao 9M. Nilichokifanya kwa vile niko nafanya biashara za fedha za mtandao nina uzoefu wa maeneo ambayo ukiweka biashara haitokutupa. Nikaamua hizi hizi hela zao ndio mtaji wangu. Nikatafuta sehemu nikapata fremu ya 300k monthly for six months.

Mchanganuo wa matumizi.
1. Kodi miezi 6 = 1.8M
2. Ukarabati na design front view = 500k
3. 236k Machine ya CRDB
4. Line za uwakala na machine ya NMB nilihamisha kutoka kwenye moja ya ofisi yangu yenye machine 2 na line za ziada.
5. Usiniulize leseni najua nimeipataje.
6. Mfanyakazi, nilimuhamisha mmoja kutoka ofisi yangu za zamani mshahara wake ni 300k kula juu yake.
7. Mtaji wa uzungushaji ulibaki around 7.2M

Mwanzo wa biashara.

Nashukuru Mungu sehemu ile ulikuwa na return nzuri ya around 1.6m mwezi wa kwanza kwa maana mwisho wa mwezi wa 6/2019. Hii nikawa natoa 1M kurudisha upatu na 300k ya mfanyakazi inayobaki naiacha iongeze biashara. Kwa kadri muda ulivyokwenda biashara imekuwa ikitoa profit kubwa na miezi yote nafanya kutoa hiyo 1M na 300k za mfanyakazi na kusave mpaka tulivyomaliza mzunguko mwisho wa mwezi wa pili 2020. Sasa nimebakiwa na around 10M ambazo nimezipata kwa ile 1M yangu na monthly profit around 2M monthly. Mantiki yangu hapa ni kwamba kama ningekaa nazo tu zile hela mpaka mzunguko unaisha nilipaswa kubaki na 1M only.

Malengo ya baadae.

Malengo yangu ni kwamba mpaka mwisho wa mwaka huu nikusanye 10M nyingine kutoka kwa hii miezi 7 iliyobaki kwa kusave profit ya 1.5M ambayo roughly nitapata 10.5M ambazo zitafanya mtaji ufike 20M. Ikishafika hiyo 20M nitaweza kupata around 3M as monthly profit.

Kwa rate 3M nataka mpaka mwisho wa 2021 nikusanye profit ya 30M kutoa kodi ya frem na mfanyakazi. Hii itafikisha around 50M kama mtaji. Ikifikia hapo nitabreak into 2 business branches. Nitawajulisha kama Mungu ataweka hai.

Hii nataka iwe historia ya kipekee katika maisha yangu. Sizitumii fedha hizi vile nina vyanzo vingine mpaka majariwa itakapofika 100M kutoka kwa hii 1M. Wale members wenzangu wengine wamenunua viwanja, wengine magari ya kubebea madem kila mtu mradi anatimiza alichokusudia. Mbaya tu nimesikia wale wa mwanzoni kule walinunua magari na tayari wameshayauza.

Katazo la mwisho.

Sijaandika ili kujigamba au kwa nia ovu, na sitojibu ujumbe wa mtu yeyote PM ukiwa na maoni au tatizo tuulizane hapa hapa wala sihitaji kuja kuitwa mwizi au tapeli.

Kuna ambao mutahisi hii ni hadithi ya kusadikika. Nakuwekea record za biashara kwa kitabu cha kuanzia January 2020. Usipoamini pita tu tafadhali bila kukwazana.

Mubarikiwe wote.

IMG_20200510_070852_8.jpeg
IMG_20200510_070943_4.jpeg
IMG_20200510_071045_1.jpeg
IMG_20200510_071131_2.jpeg
IMG_20200510_071242_2.jpeg
 
Duuh hongera,
Kwa lugha rahisi ni tuseme ulikopa mil9. Kuanzisha biashara kwa kutegemea hela ya mkopo 100℅ ni risk sana.

Nadhani kilichokusaidia zaidi ni kuwa ulianzisha biashara huku huitegemei ikuendeshee maisha. Nafikiri ndio maana umefaulu vyema sana.
 
Duuh hongera,
Kwa lugha rahisi ni tuseme ulikopa mil9.
Kuanzisha biashara kwa hela ya mkopo ni risk sana. Nadhani kilichokusaidia zaidi ni kuwa ulianzisha biashara huku huitegemei ikuendeshee maisha. Nafikiri ndio maana umefaulu vyema sana.
Shukrani troublemaker ndio maana nimetoa onyo hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Naomba kuuliza,
Hivi naweza pata laini ya wakaka bila leseni ya biashara.?
Nina mpango wa kuanzisha kibanda cha uwakala ila wamenambia lazima niwe na tin number na leseni ya biashara.
Naomba muongozo.......

Sent using myLG leon
 
Back
Top Bottom