Jinsi Nilivyofedheheka: Mtoto wa Waziri fulani akaalikwa chakula...!

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
736
Qouted in 2006....

Mimi nina umri wa miaka 34.
Malezi na makuzi yangu yalikuwa ya wazazi ambao kwa sasa wangeitwa "machekibobu". Yaani watu wa kujionyesha kwamba wana fedha,na hawana maisha ya shida..
Nami nilikua na kuishi maisha hayo.Nilikuwa mtu wa kujikweza sana.

Mwaka 2000 nilipata kazikwenye ofisi binafsi maeneo ya Vingunguti..(nilimaliza masomo chuo cha biashara).
Kazi yangu ilikuwa ya kawaida tu,kutumwa hapa na pale,kujaza fomu za hesabu za fedha,na mengine ya aina hiyo.

Nikiwa hapo kazini,nilikutana na msichana mmoja aliyekuwa anafanya kazi kampuni jirani na yetu. Nilikutana naye kwenye mgahawa maeneo hayohayo nilipoenda kupata mlo wa mchana.

Kwa kweli nilimpenda ghafla,lakini naye alionekana kunipenda pia! Tulijikuta tukiwa marafiki baada ya kuwa nimemwanza. Ilikuwa kuna kaugumu kumtongoza kwani alikuwa mzuri sana na alikuwa anamiliki gari aina ya RAV 4 ya milango mitayu. Ila alinikubalia kirahisi hadi nikashangaa.

Katika kujitambulisha,nilijipa ujiko wa ajabu sana! Mimi ni mtu wa Tanga,na baba yangu kidogo anajuana na waziri mmoja mkubwa sana serikalini. Sasa badala ya kusema ukweli kuhusu baba yangu,ambaye kwa maisha yake ya kichekibobu,alikuwa amechalala sana,nilimtaja waziri huyo kama baba.

Yule binti aliamini,na nyumbani kwao,bila shaka alitangaza amepata ampendaye ambaye baba yake ni mtu fulani. Siku hiyo binti alinialika nyumbani kwao kwa ajili ya chakula cha mchana.Ilikuwa Jumapili.
Nilijitahi sana kukodi gari la rafiki yangu kwa Tshs 40,000,ili wajue nina gari.

Unajua kilichotokea?nilipofika nyumbani kwao,nilimkuta mama yake na yule binti. Baba yake alikuwa amefariki zamani. Lakini pia nilimkuta mtu mwingine...! Jaribu kuotea alikuwa nani ................!!!!

Alikuwa ni baba yangu! Nilibabaika sana na kujiuliza maswali mengi bila majibu. Nilipigwa na butwaa kwa muda,na hata baba pia alishikwa na mshangao. Baada ya kumsalimu mama wa binti,nilimsalimu baba,na kumuuuliza,"uko huku?" baba alisema "nashangaa nawe waijua hii familia.
"Mama Lewis tulikuwa naye kazini zamani. Siku nyingi sijamtembelea,leo nimeamua kuja kumuona..."

Yule mama mkwe "mtarajiwa" aliuliza," kwani mnajuana....?"
Baba akajibu,"huyu ni mwanangu wa kwanza.."
Halafu palizuka kimya. Yule mama kwa ajili ya kuua soo,akanikaribisha. Lakini ghafla nilimwona yule binti,alikuwa amebadilika,hakuwa na furaha tena.

Tulikula katika hali ya undavaundava tu. Tulipomaliza kula,sikupoteza muda nikaamua kuaga,kwani nilijua binti na mama yake walikuwa wananisanifu sana. Yaani kutoka mtoto wa mkubwa hadi kuwa mtoto wa mzee aliyecheza na maisha siku za nyuma.

Mbaya zaidi,baba alikuwa amefika pale kuomba msaada! Niliaga na kumwacha baba akiendelea "kupiga virungu" vyake. Nilikuwa na hakika ya kuwa baba aloambiwa yote kwani aliponitembelea jioni kwangu,aliniambia nimejisanifu sana kujifanya mtoto wa waziri.

Je una haja ya kujua kama urafiki na binti uliendelea?
 
Mimi napenda kuongea ukweli sababu naamin ntapata wa size yangu.
 
Kwanini ulijikweza? Kwani ungesema mtoto wa Matonya usingependwa? Aaah nakuuliza usingependwa?? Haya tuambie kama urafiki uliendelea.
 
Kwanini ulijikweza? Kwani ungesema mtoto wa Matonya usingependwa? Aaah nakuuliza usingependwa?? Haya tuambie kama urafiki uliendelea.

Aaah.. Mtalingolo... Yaani unaamini kuna urafiki tena hapo? Dada yule anaonesha alikuwa kajitambua. Yaani thamani yake haipo kwenye maisha ya juu aliyonayo.. Tofauti na mimi niliyemtathimini kwa mali alizonazo. Nilikua kujua kuwa I was wrong.. So nilijifunza mkuu Mtalingolo..
 
Unamkana baba???

Yaani kwa kweli ilikuwa hivyo..

Ila hili najua limewahi kutokea kwa wengi tu,kukana baba au mama kwa kuona kama vile hafananii na wewe ulivyo... Unajiona uko baab kubwa kupitiliza...
 
Duh kweli ulifedheheka.. Enhe, Ikawaje sasa na huyo dada?

Unadhani kuna nini tena hapo...

Nikawa nikimwona natamani ardhi ipasuke nidumbukie ndani!

Hata ule mgahawa niliuhama!

Hadi leo nikiona Rav 4 short chassis...aah,nashtuka Amyner!
 
Mdada mwenyewe asije akawa ni memba wa JF,ikawa noma..

Atanichana liiive!
 
Ameumbuka.
Ndo maana huwa sipendi fiksi za kijinga,
kazi ya zege,
demu wa kizee,
kinywaji gongo.
 
duh story tamu kweli,lakini madem nao wanapenda kupigwa fix,nakumbuka miaka ya nyuma kuna mdada alinitoa hapa dar mpaka kwa mshua wake moshi huku sina sentano mfukoni,bibie akandakisha kilinda mfuko ili tukifika nisiadhirike,kufika korogwe binti ananiambia nitoe unyonge nikifika nijifanye mtu wa bussiness flani kubwa kubwa yaani najiweza kinoma,bac namie nilivyokabidhiwa rungu ndo niliua band maana nilivofika na mzee akanikaribisha na safari lager toka mlangoni bac wee ilipofika mda wa mahojiano nilitomboka nkataja maduka ya spea karibia yote pale msimbazi namiliki,taja na mabiashara kibao dem mwenyewe alikimbia nje kucheka maana nilizidisha.kutoka hapo mzee wa kichaga akanikarimu vizuri saaana mpaka naondoka,sheshe lilikuja alipotia timu dar kutafuta spea za magari yake ilibidi nizuge nimeenda dubai.mara nairobi mradi hamna amani.badae niliachana na huyo binti baada ya kumzalisha mtoto mmoja
huyo mzee hatujaonana mpaka leo anantafuta japo anione tu maana alikuja jua fix zoote
 
Ah babu kijana.. Hiyo yako nayo kali... Ila mi naamini wanawake ni watu wa tofauti sana! Hasa wakipenda...

Anaweza akafanya mambo ya ajabu sana,yote sababu ya kupenda..
 
Dah ningekuwa mimi natafuta chupa yangu ya konyagi iko wapi,nipunguze aibu alafu nagangamara mpaka mwisho siondoki.
 
Dah ningekuwa mimi natafuta chupa yangu ya konyagi iko wapi,nipunguze aibu alafu nagangamara mpaka mwisho siondoki.

ha ha ha.... Vodka bana..

Ila ni kama vile kanyang'anywa tonge mdomoni..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom