JINA LAKO au MAJINA YAKO?

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Napatwa utata pale mtu anapoulizwa jina lake au kuagizwa aandike jina lake, kisha anajibu au kuandika, mimi ni fulani fulani fulani ( John Alfa Mohamedi).
Ni sahihi mtu kujibu au kuandika majina matatu wakati kaulizwa JINA lake?
 
kwa hakika ukiulizwa jina wewe ukataja majina zaidi ya moja unakuwa umefanya zaidi ya kile ulichoulizwa. Lakini kwa kuwa jina la mt linaonesha utambulisho (identity) wake, ndiyo maana mtu haishii kutaja jina moja tu. Inabidi ataje majina zaidi ya moja ili kuondoa ambiguity inayoweza kujitokeza. Kule Kenya mara nyingi huulizwi "jina lako nani", bali unaulizwa "majina yako nani"?
 
Wakenya ndi wanajua kiswahili vizuri. Angalia kipindi cha vioja mahakamani, utasikia, majina yako kamili... nae anajibu, odieki ojware muthui, mheshimiwa
 
........................... ndiyo maana mtu haishii kutaja jina moja tu. Inabidi ataje majina zaidi ya moja ...................

BABUYAO,
Hapa naona unanipa wakati mgumu zaidi.
Kwa nini mtu ataje majina zaidi ya moja wakati mtu mmoja anapaswa kuwa na jina moja?
Ukiulizwa jina lako nani , ukataja majina zaidi ya moja, kwangu inamaanisha umetaja na majina ya watu wengine.
Kwa kawaida, Jina la mtu, ni moja tu. Au?
 
Mimi nafikari ni sahihi kutaja majina na siyo kutaja jina. Kwa mfano ukiulizwa unaitwa nani na wewe ukajibu naitwa EXAUD, unakaribisha tena swali la pili kuwa, Exaud nani? Ili kukutofausha wewe na Exaud mwingine ndipo kunakopelekea kutaka majina mengine zaidi. Hata majina mawili bado yanaweza kutokukutambulisha sawa sawa hadi kuhitaji lingine la tatu au hata la nne.
 
KYACHAKICHE,
Mheshimiwa wazo lako linazua maswali pia.
Ukweli uko wapi sasa?
Kama ukiulizwa jina lako ni nani, unapaswa kutaja jina na siyo majina.
Kama ukisema jina lako ni KITAKACHO KUJA KIJE,
Mimi sioni kuwa umejibu ulichoulizwa kwa mujibu wa lugha ya kiswahili.
Jina ni umoja siyo wingi.
 
Mkuu, usipige ikulu!
 
BABUYAO,
Hapa naona unanipa wakati mgumu zaidi.
Kwa nini mtu ataje majina zaidi ya moja wakati mtu mmoja anapaswa kuwa na jina moja?
Ukiulizwa jina lako nani , ukataja majina zaidi ya moja, kwangu inamaanisha umetaja na majina ya watu wengine.
Kwa kawaida, Jina la mtu, ni moja tu. Au?

Utifautishe mambo mawili: kuna suala la lugha, na pili kuna suala la ujumbe wenyewe.
Lugha: Kuulizwa jina moja ni namna ya kuongea kifasihi Kiswahili. Lakini kinachotafutwa ni zaidi ya jina moja. Ndiyo maana ukiuliza kama Wakenya "majina yako ni nani" watu watakucheka siyo namna ya kuongea Kiswahili. Kumbe unapoulizwa jina, inaonekana kinachotakiwa ni jina moja. Siyo hivyo hiyo ni namna ya kuongea Waswahili ambayo haikufungi useme jina moja tu. Inadai zaidi. Kwani kwa swali hilo mtu angeweza bado kukuuliza "unaitwa nani"? Na hapo anamaanisha implicitly jina zaidi ya moja.

Kuhusu kiini au ujumbe unaotafutwa ni kwamba mtu anakuuliza jina akitaka kujua identity yako. Wewe ni nani. Sasa uwewe wako hauko kama kisiwa. Wewe hukujizaa, hukujiumba, wala hukutoka kwenye mti. Umetoka kwa watu: wazazi, ukoo, nk. Uwewe wako ni muungano wa yote hayo. You are unique but not isolated. Wewe ni zaidi ya jina moja. Wewe uliye mtu mmoja identity yako ni zaidi ya jina. Wewe ni wengine pia, ni majina mengine pia yenye uhusiano na nafsi yako. Yote hayo yanakutambulisha wewe. Ndiyo maana ukiulizwa utasema mf. mimi naitwa "John Kalumanzila"., maana yake majina hayo yote "ni wewe". Ndiyo maana wazungu watasema "jina lako la kwanza unaitwa nani?" (first name), na tena utaulizwa wewe huyo huyo "jina lako la ukoo, je" (Sir name). Ni majina mawili lakini mtu ni mmoja, na identity ni moja. Mswahili atakuuliza jina lako nani? akimaanisha siyo jina moja tu, bali na la pili , na la tatu, nk ili uweze kuji-identify bila ambiguity. Uwe bayana.
 
Utifautishe mambo mawili: kuna suala la lugha, na pili kuna suala la ujumbe wenyewe.
Lugha: Kuulizwa jina moja ni namna ya kuongea kifasihi Kiswahili. Lakini ,,,,,,,,,,,,,,,,, Mswahili atakuuliza jina lako nani? akimaanisha siyo jina moja tu, bali na la pili , na la tatu, nk ili uweze kuji-identify bila ambiguity. Uwe bayana.

BABUYAO,
Turudi upande wa Lugha.
Unapotetea uhalali wa kutoa jibu la wingi katika umoja, lugha haikupi usahihi.
Hata wajukuu zako watachanganyikiwa.

Napata wazo kuwa, kutokana na mawazo yako, Lugha haina swali sahihi la kupata full identity ya mtu.
AU?
 
Mimi sijui wewe mwenzangu ni wa wapi lakini lugha nyingi za Kibantu zinatumia wingi kwa kumaanisha umoja. Je, hayo ni makosa kifasihi? Hapana! Mfano katika lugha nyingi unaweza kusikia (tafsiri tu) mtu anakuambia kwa kilugha "karibuni, jongeeni" wakati wewe ni mtu mmoja. Kwa nini wingi wakati mtu ni mmoja. Pia hata katika lugha za Kizungu, mf. Kijerumani na Kiitalia kuna namna hiyo ya kuongea. Hizi zinaitwa mode of expression. Zinakataa mantiki ya kawaida ya ku-reason kwa mstari ulionyooka. Ilikufahamu maana yake lazima uingie katika utamaduni wa watu, ujifunze namna yao ya kuongea.

Ndiyo hivo. Kwa hiyo usione ajabu unapoulizwa jina ukatakiwa kutoa majina yote. Na kwa msingi majina yote ni wewe. La ukoo ni lenu wote katika makabila fulani, mf. Wahehe.
 
Jina lako nani? Mimi? Ndio wewe! Jina langu asumani, jina la babayako? Samani, ahaa! Hayo ndo majina yako enh? Ndiyo. Akhsante sana.(hapa kuna utambulisho ulio wazi, na sidhani iwapo aulizwaye atapata utata, labda vikitumika vilugha vitumikavyo kila siku) na sioni haja ya mtu kusifu utajaji/utambulishaji fulani, bora ktk mazungumzo ni kuelewana tu na hakuna lugha ikosayo utata au ukakasi katika baadhi ya masuala yahusuyo mahusiano ya kimaongezi.
 
Jina ni moja, lakini linaweza kuwa na maneno zaidi ya moja. Jina ni kitambulisho. Mtu mmoja anakuwa na jina moja. Augustine Moshi ni jina langu, na sio majina yangu.

Kwa wale Wakristo, nisemehe hivi: Yesu aliwaamuru wafuasi wake waende duniani kote wakiwabatiza watu kwa JINA la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Sio kwa MAJINA ya ......, kwani Mungu ni mmoja na jina lake ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Ni jina moja tu.

Kwa hivyo basi, anayechanganikiwa hapa ni yule anayedhani jina lazima liwe neno moja.
 
Mkuu kwa hapo tuko pamoja.
 
AUGUSTINE, NA KYACHAKICHE,
Hapo siko pamoja nanyi.
Kusema kuwa Augustine Moshi ni jina lako, ni kama unalazimisha wewe binafsi kumiliki jina la ukoo wako.
Wewe ni Augustine, na Moshi ni jina la ukoo wako.
Wakuu tazameni ukweli huo.
 
Nadhani hajalazimisha hilo ndio jina lake, labda swali lilitakiwa kuuliza JINA LAKO KAMILI na si jina lako. Mtu hatambuliwa kwa jina moja, inatakiwa majina yake kamili.
 
Nadhani hajalazimisha hilo ndio jina lake, labda swali lilitakiwa kuuliza JINA LAKO KAMILI na si jina lako. Mtu hatambuliwa kwa jina moja, inatakiwa majina yake kamili.

KIJUNJWE,
Asante kwa mchango wako.
Hapa umeleta changamoto mpya,"JINA LAKO KAMILI" na "MAJINA YAKO KAMILI".
Utata huo ndo ulionipelekea kuona kuwa kuna haja ya kufikiri kama ni sahihi kumuuliza mtu jina lake halafu jibu lake liwe mlolongo wa majina.

Sasa naona umezidi kuchochea utata huu.
 
Kaka Exaud, kwa jinsi ninavyo elewa mimi, haya mambo ya jina na mtu akakutajia majina mawili mpaka matatu, ni matokeo ya mazoea ya kitamaduni tulio rithi toka kwenye tanaduni zetu. Na vile vile inategemea na mazingira uliokuwepo wakati unaulizwa swali.

Mfano: Ukiwa benki au unajihandikisha kwenye taasisi yoyote ile utakapo ulizwa jina lako hapo automatic utataja majina zaidi ya moja.

Na vile vile inasaidia sana kuondoa utata katika utambulisho.

Kuna kina Exaud wengi sana hapo bongo. Lakini utakapo taja majina yako mf, Exaud J. Makyao...! Moja kwa moja itajulikana ni yupo anaye ongelewa.
 
Waungwana,

Mtu jina lake ndilo linalomtambulisha yeye mmoja pekee katika kundi. Mathalan, mtu akisema jina lake John au Kidawa au Ali anakuwa hajajitambulisha kikakamilifu kwa kuwa ametumia jina la kawaida. Kuna akina John au Kidawa au Ali kibao. Na akitumia jina la ukoo pekee, kwa mfano Mazengo au Ng'wanakilala au Magohagasenga, hao nao wako kibao katika ukoo. Lakini mtu akijitambulisha kama John Robert Mazengo, hilo kiutambulisho linakuwa jina la mtu mmoja lililokamili na kiutaratibu linahesabiwa jina moja na kiihesabu yanakuwa majina matatu yanayomtambulisha mtu mmoja.

Kupanga ni kuchagua!
 
KWAMINCHI,
Kwa hayo mawazo yako, basi mtu anapaswa kujibu orodha ya majina kadhaa, atakiwapo kujitambulisha na siyo aulizwapo JINA LAKO NANI.
 
Napatwa utata pale mtu anapoulizwa jina lake au kuagizwa aandike jina lake, kisha anajibu au kuandika, mimi ni fulani fulani fulani ( John Alfa Mohamedi).
Ni sahihi mtu kujibu au kuandika majina matatu wakati kaulizwa JINA lake?

Mkuu, kutokana na mazoea tu na kuepuka ile ya kuulizwa mara mbili mbili. Unaweza kuulizwa jina lako nani, ukajibu mimi naitwa Exaud. Then anakuuliza tena, Exaud bin nani? jibu linakuwa Makyao. So, kuepuka hiyo, watu wamezoea kutoa majina yote ili kuepuka swali la pili.

Ni sawa na mtu anayeenda bar kukata kiu na maswali yanaweza kuwa hivi:

Mteja: Naomba Bia

Muuzaji: Bia gani?

Mteja: Kili

Muuzaji: Ya moto au baridi?

Mteja: Baridi

Muuzaji: Utatumia glass?

Mteja: Oh, yes please!

Ingekuwa rahisi sana kama mteja angefika na kusema, hey, nipatie Kili bariiidi kabisa, na glass!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom