Jina la sasa la Twitter" X" lina utata sana

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,028
12,352
Toka billionaire Musk auchukue mtandao wa Twitter kuna mabadiliko kadha wa kadha amefanya.

Moja ya mabadiliko hayo ni kutoka kuitwa Twitter mpaka kuitwa "X".

Hili jina limekuwa na ukakasi mwingi sana hasa katika kulitumia kutambulisha mtandao unaotumia hata kufungua app yake katika kundi la watu lililo kuzunguka.

Hili jina "X" limejenga picha sio nzuri katika sehemu kubwa duniani ndani ya jamii hasa upande wa maadili.

Kuutamka mtandao "X" mbele ya watu lazima usindikize na Twitter ili usieleweke vibaya, naoa watangazaji wengi wa vipindi vya runinga na redioni lina wapa ukakasi mkubwa kulitamka.

Mfano: Mwanzo videos zilizopo Twitter zilikuwa zinaelezwa kama "Twitter videos" sasa hivi inabidi useme "X videos" tafrani tupu.

Sijui mtaalamu musk aliwaza nini juu ya hili jina maana limekaa kimagumashi balaah.
 
siti ya mbele hapa tuwasubiri watumiaji wa X waje.....
Just imagine unafungua hii kitu mbele ya umati wa watu

IMG_20231002_183016.jpg
 
Toka billionaire Musk auchukue mtandao wa Twitter kuna mabadiliko kadha wa kadha amefanya.

Moja ya mabadiliko hayo ni kutoka kuitwa Twitter mpaka kuitwa "X...

Mwenye mali kaamua ndugu. Si waona trump kaanzisha wake? Wanasema raha jipe mwenyewe.
 
Yaani nina siku nyingi sijaingia twitter sas juzi bhana nikataka nichungulie tena kule, sas mimi nagoogle twitter wenyewe wanaleta × sas nkahisi hyo ni scam, nkawa natafuta kwingine kila nkiandika wanaleta hvo hvo duu, kumbe bhana wamebadili
 
Back
Top Bottom