Jina la mtoto...

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,111
115,905
Kuna rafiki yangu ambaye ameoa hivi karibuni,mkewe
kajifungua mtoto wa kike...
Tatizo sasa ni kuwa yeye baba mtoto alitaka kumpa
mtoto jina la mama yake ambalo ni mwajabu.....
Mama mtoto hataki jina hilo anadai la kishamba...
Yeye anataka mtoto aitwe preta jina la msichana wa
kwenye tamthilia ya wa brazil inayoitwa shades of sin ambayo
inaendelaea sasa hivi.....

Mimi nimemuunga mkono baba mtu......

Nynyi mnaonaje????????????

Tuwashauri vipi???????
 
mambo ya kurithi majina yamepitwa na wakati bwana, mpeni mtoto jina zuri ikiwezekana kama mkristo tafuta jina kwenye Biblia
 
mambo ya kurithi majina yamepitwa na wakati bwana, mpeni mtoto jina zuri ikiwezekana kama mkristo tafuta jina kwenye biblia

ishu sio kurithi jina..
Ishu majina ya kwenye tamthilia ni sahihi kwa watoto???????
 
Apewe jina la mama mzazi wa baba yake yaani Mwajabu,huko ni kutunza kumbukumbu za familia na ukoo kwa ujumla ,ndio maana halisi ya kuwapa watoto majina ya vizazi vyetu.
 
ishu sio kurithi jina..
Ishu majina ya kwenye tamthilia ni sahihi kwa watoto???????

Skubaliani na majina ya kwenye tamthilia hata kidogo! wenzetu wanapeana majina kwa maana zao, ss tunaiga tu. Mpe mtoto jina lenye maana katika jamii.
 
bila shaka jina la mwajabu limepitwa na wakati, lakini si vibaya kumuenzi mzazi mtu. lakini hilo jina la kwenye tamthilia halijulikani la dini gani.
 
washauri kuwa jina linakuja kuwa na athari huko mbele katika mafanikio ya mtoto believe you me!...Hilo jina la Mwajabu sijui maana yake..lakini ajabu zaidi ni hilo la Preta.... wanajua maana yake? je wameshaona akina Preta ni watu wa namna gani?
 
Du haya mambo ya kurithishana majina unaweza kuta bibi anapenda wanga na katoto kakarithi kuwanga vilevile
na huyo preta anatabia zipi kwenye hiyo tamthilia

isije kuwa kama ile tamthilia ya ruby ..ruby mwenyewe tabia yake kutamani kuiba wachumba wa wenzake
 
washauri kuwa jina linakuja kuwa na athari huko mbele katika mafanikio ya mtoto believe you me!...Hilo jina la Mwajabu sijui maana yake..lakini ajabu zaidi ni hilo la Preta.... wanajua maana yake? je wameshaona akina Preta ni watu wa namna gani?

Angalieni pia na huyo mama mzaa chema kama ana tabia njema, namaanisha kama mkorofi au tabia yoyote mbaya basi tegemeeni hayo kwa huyo binti yenu.
 
Kumpa mtu jina la mzazi ndio ni heshima ila mara nyingi tabia huambatana na jina kama mtu amepewa sababu ya fulani. Na hilo la tamthilia pia siliafiki, wakae chini watafute jina watakalokubaliana pamoja bila kupendelea upande mmoja..wanaweza hata kutunga la kwao ila majina ya kurithi siyafagilii kabisa
 
Naungana na wote hapo waliosema kuwa kumpa mtoto jina la tamthilia au la kurithi ni jambo baya.Jamani majina yana maana sana na huwa yanabeba tabia ya mtu.There is power in names.
Huyo mtoto akipewa jina la bibi kuna uwezekano mkubwa wa kurithi tabia za bibi.
Mpeni a brand new name tena lenye kubeba maana nzuri mf,Upendo,Neema,Furaha,Victoria nk.na sio Mawazo,Matatizo,Siyawezi,Sikujua,Majuto(noma jamani haya majina)
 
jina ni kitambulisho muhimu kwa mtoto atakapokuwa. jina baya litakuja kumfanya mtoto ajiskie hata aibu kujitambulisha kwa wenzake wakati akiwa mkubwa (hasa katika zama hizi za kujikweza), ni vyema wazee wakakaa kitako na kutafuta jina ambalo atakuja kulifurahia kuitwa mtoto wao akiwa mkubwa. (bila kuzingatia mila wala tamthilia).

quiet
 
Kuna rafiki yangu ambaye ameoa hivi karibuni,mkewe
kajifungua mtoto wa kike...
Tatizo sasa ni kuwa yeye baba mtoto alitaka kumpa
mtoto jina la mama yake ambalo ni mwajabu.....
Mama mtoto hataki jina hilo anadai la kishamba...
Yeye anataka mtoto aitwe preta jina la msichana wa
kwenye tamthilia ya wa brazil inayoitwa shades of sin ambayo
inaendelaea sasa hivi.....

Mimi nimemuunga mkono baba mtu......

Nynyi mnaonaje????????????

Tuwashauri vipi???????
ni kaaazi kwelikweli!
wapendanao mimi nilidhan wangepewa nafasi kila mmoja wao kuelezea hisia zake, ila kwakua jina ni maisha ya mtoto.
wakae faragha maana sijaona sababu za msingi hapo lipi jina linamfaa mtoto ingawa navutika na jina la bibi yake,
lakin ni ukweli pia sio jina zuri saaana
kumpa mtoto katika zama hizi za utandawazi!
kwa ushauri baba atumie busara
kumwachia mama mtoto nafasi
kwakua ni jinsia yake ila kubwa zaid ni
kumwomba mama achague jina zuri
na litakaloweza kumfurahisha na mumewe
pia sio kigezo kizuri kuchagua jina
sababu tu ni la kwenye tamthilia!
kwakuzingatia ushauri huu
nawaomba warudi chumban
bila kuathiri afya ya mtoto
watuletee jina watakalo mpa mtoto wao
majina yaliyotumikaaaaaaaaaaaaaa
yanakua yamemaliza baraka!
Tchao
 
Hapo umemaliza Frankie, mwekeni mtoto pembeni au mpelekeni chumbani kwa dada ili mjadiliane na kukubaliana jina la mtoto.
 
washauri kuwa jina linakuja kuwa na athari huko mbele katika mafanikio ya mtoto believe you me!...hilo jina la mwajabu sijui maana yake..lakini ajabu zaidi ni hilo la preta.... Wanajua maana yake? Je wameshaona akina preta ni watu wa namna gani?

hata mimi naona majina ya tamthilia sio sahihi kwa watoto...
Ingawa wabongo wanaona fashion.....
 
Kama hamjapata jina mwiteni KUNTAKINTU, angekuwa men mngemwita KUNTAKINTE.
 
Back
Top Bottom