Jihadharini wanawake Dar es salaam - serial killer on the loose!

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Haya mauaji ya wanawake Dar es Salaam ni vipi?
Hadi sasa wameshauwa wanawake 7 kwa style hiyo hiyo!
Tumeanza kuwa na serial killers jamani akina dada mjihadhari!
 
Mshukiwa ni mwanaume mtanashati ( handsome), anavaa cap, maji ya kunde, siyo mnene wala mwembamba, Mrefu,
Anauwa wanawake weupe, wake za watu kwenye nyumba za kulala wageni!
 
Hii ni hatari sana. Ni wakati sasa wadada muanze kujifunza martial arts kwa ajili ya self defense. Pia anzeni kubeba pepper spray. Kwa maelezo na dondoo zaidi msisite kuni-PM.
 
Yani inakuwaje kuwaje mpaka wanauawa?? Unaeza kutujuza zaidi WOS??
 
Wanasemaga serial killers ni wazungu tu...
But kumbe hata waafrika wapo......
 
Huyu mkaka sijui anakutana nao vipi au hata kukubaliana nao vipi . Ila kinachotokea ni kwamba anaenda nao "guest houses" anapanga chumba. Anatoka kijanja huku kaacha maiti ndani ya chumba.

Wa mwisho kauawa Magomeni . Mkaka alitoka asubuhi sana akaaga anafika dukani na huku kamwaacha mwanamke chumbani.Muda ulipopita sana wahudumu ilibidi wavunje chumba.Wakakuta mwanamke kasogezwa pembeni mwa kitanda kalala kifudifudi huku keshakufa! Inamaanisha alimuua na kulala naye hadi asubuhi kisha akajiondokea taratibu! Pochi ya dada ilikutwa ina kila kitu! Kesho kamanda Kova atazungumzia hii ishu redioni.Labda tutasikia mengi zaidi.
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Huyu mkaka sijui anakutana nao vipi au hata kukubaliana nao vipi . Ila kinachotokea ni kwamba anaenda nao "guest houses" anapanga chumba. Anatoka kijanja huku kaacha maiti ndani ya chumba.

Wa mwisho kauawa Magomeni . Mkaka alitoka asubuhi sana akaaga anaika dukani na huku kamwaacha mwanamke chumbani.Muda ulipopita sana wahudumu ilibidi wavunje chumba.Wakakuta mwanamke kasogezwa pembeni mwa kitanda kalala kifudifudi huku keshakufa! Inamaanisha alimuua na kulala naye hadi asubuhi kisha akajiondokea taratibu! Pochi ya dada ilikutwa ina kila kitu! Kesho kamanda Kova atazungumzia hii ishu redioni.Labda tutasikia mengi zaidi.
Duh hii mbaya sana lakini kama wewe ni kijana mtanashati ( handsome), unavaa cap, maji ya kunde, siyo mnene wala mwembamba, Mrefu, na unapenda kupeleka wanawake guest nadhani huu ni muda muafaka wa kuacha tabia yako..

Pili kwa Inteligensia zaidi si ingekuwa bora kuweka mtego na kutokutoa information zaidi kwamba wanajua appearance yake ili waweze kumshika huyu jambazi..! Sababu sidhani kama atavaa cap tena
 
Wanasemaga serial killers ni wazungu tu...
But kumbe hata waafrika wapo......

Waafrika nao wameanza catching up pretty fast!!
Serial Killer wa kwanza documented kwenye " Crime Library" unaweza kuangalia website, anatoka South Afrika.

Kuna hiyo notion kuwa serial killers ni wazungu - lakini ukiingia kwenye fani ya " criminality" usome kuhusu criminal mind utaona kuwa hizo features na profiles ziko hata kwa waafrika. Sasa sijui kwanini wanaanza kujitokeza kwa kasi miaka hii kuliko huko nyuma. Kwa mfano profile ya huyu muuaji anafuata wanawake walioolewa, lakini wako kwenye umri usiozidi 35, weupe, wenye makalio makubwa na inasemekana pia akishaua analala nao hadi asubuhi na kuwavua pete na kuondoka nazo! Hii profile inasema mengi kuhusu hasira ya muuaji.
 
Mambo ya stereotypes ni mabaya sana. Good law enforcement ni kutokuondoa kundi lolote lile katika orodha ya watu wanaoweza kufanya uhalifu.

Unawakumbuka wale DC snipers wa mwaka 2002? Watu si waliingia mkenge bana....so called experts wakaja na kila aina ya profiles. Oh eti lazima atakuwa mzungu...wa miaka fulani...anasumbuliwa na hiki na kile. Kumbe wapi bana...jamaa walikuwa wanugu na katikati ya mauji yao kuna siku walikuwa pulled over na polisi kwa sababu ya traffic violation lakini kwa vile profile iliyokuwa imeshatolewa na 'wataalamu' ni ya mzungu huko kukamatwa kwao hakuku-raise any suspicion kwa huyo police officer aliyewasimamisha na mwishowe wakaendelea na mauaji yao. Laiti kama wangewekwa chini ya ulinzi siku hiyo maafa mengine yangepunguzwa.

So good law enforcement never puts anything past anybody. Everybody is a suspect (or person of interest) until the perpetrator is found and apprehended.
 
Niko very interested na hii habari... hivi vifo vilifuatana saana lakini nakumbuka mara ya

mwisho mtu wa saba ni kama mwezi mmoja na nusu ago... kaongezeka mwingine??

Na kama kaongezeka atakua wa nane....
 
Huyu kweli ana issue na wanawake waliolewa. Labda anawafundisha adabu kidogo maana kama ni mke wa mtu unakubalije kwenda nyumba ya kulala wageni na mtu ambaye sio mumeo??? na si ajabu wanakuwa wamekutana siku hiyo hiyo na kama unavyosema ni mkaka mtanashati lazima wadada waingie mkenge.......
 
dah huyu jamaa lazima atakua ametendwa na mke wake either ameachwa au alikataliwa au mke alikua natoka nje ya ndoa tujiulize
  • kwann anaondoka na pete za ndoa
  • kwann wake za watu tu
  • kwann wawe wa umbo fulani?
  • kwann awauwe usiku na kulala nao mpaka asubuhi?
Hv kweli hapa tanzania tumekosa intalijensia ya kuchunguza kitu kama hicho?
hatuna Investigation reporters? hata kutangaza kwa watu kuhusu matches za huyu mtu?
hatuwezi kuleta asumption kuhusu mtu wa aina fulani ambae aliwahi kuwa na mke au mchumba wa aina fulani ?
nadhani tuna matatizo kwenye jeshi letu la polisi,lakini ngoja...hivi hatuna vyombo vingine vya usalama vinavyoweza kusaidia Hili?
Hebu Imagine wife wako kauawa gesti na muuaji....aibu,uchungu,loss,frustration na mengine mengi sana,
by the way...sikubali kabisa inteligence ya jeshi letu la polisi..
 
Yule aliyeua miezi iiyopita si tulisikia ameshikwa? Au ndio huyuhuyu anaendeleza ufirauni wake?

Kuna habari kama hizi zililetwa humu miezi iliyopita.
 
Mambo ya stereotypes ni mabaya sana. Good law enforcement ni kutokuondoa kundi lolote lile katika orodha ya watu wanaoweza kufanya uhalifu.

Unawakumbuka wale DC snipers wa mwaka 2002? Watu si waliingia mkenge bana....so called experts wakaja na kila aina ya profiles. Oh eti lazima atakuwa mzungu...wa miaka fulani...anasumbuliwa na hiki na kile. Kumbe wapi bana...jamaa walikuwa wanugu na katikati ya mauji yao kuna siku walikuwa pulled over na polisi kwa sababu ya traffic violation lakini kwa vile profile iliyokuwa imeshatolewa na 'wataalamu' ni ya mzungu huko kukamatwa kwao hakuku-raise any suspicion kwa huyo police officer aliyewasimamisha na mwishowe wakaendelea na mauaji yao. Laiti kama wangewekwa chini ya ulinzi siku hiyo maafa mengine yangepunguzwa.

So good law enforcement never puts anything past anybody. Everybody is a suspect (or person of interest) until the perpetrator is found and apprehended.

Kweli stereotypes huchangia katika poor investagations. Its funny kwamba wazungu say USA wana bias kwamba race fulani ndio inafanya makosa ya aina fulani.Hata hao experts ambao ni wazungu wamekuwa kwa miaka mingi wakiamini weusi hawawezi kufanya makosa fulan fulani - sijui ni kwa vile hayo makosa yanafanywa kwa 'ustadi mkubwa" hivyo kuona weusi hawa hiyo sophistication au sijui ni nini!

Niko very interested na hii habari... hivi vifo vilifuatana saana lakini nakumbuka mara ya

mwisho mtu wa saba ni kama mwezi mmoja na nusu ago... kaongezeka mwingine??

Na kama kaongezeka atakua wa nane....

Well Ashadii nadhani huyu ndio wa saba. Which means jamaa bado yuko mawindoni.

dah huyu jamaa lazima atakua ametendwa na mke wake either ameachwa au alikataliwa au mke alikua natoka nje ya ndoa tujiulize
  • kwann anaondoka na pete za ndoa
  • kwann wake za watu tu
  • kwann wawe wa umbo fulani?
  • kwann awauwe usiku na kulala nao mpaka asubuhi?
Hv kweli hapa tanzania tumekosa intalijensia ya kuchunguza kitu kama hicho?
hatuna Investigation reporters? hata kutangaza kwa watu kuhusu matches za huyu mtu?
hatuwezi kuleta asumption kuhusu mtu wa aina fulani ambae aliwahi kuwa na mke au mchumba wa aina fulani ?
nadhani tuna matatizo kwenye jeshi letu la polisi,lakini ngoja...hivi hatuna vyombo vingine vya usalama vinavyoweza kusaidia Hili?
Hebu Imagine wife wako kauawa gesti na muuaji....aibu,uchungu,loss,frustration na mengine mengi sana,
by the way...sikubali kabisa inteligence ya jeshi letu la polisi..

Profile yake inaonyesha kabisa anafanya mauaji ya kulipiza kisasi.Ila hatuwezi kusema kwa uhakika aliyemtenda ni mke maana yawezekana ni mwanamke mwingine yeyote aliyewahi kuwa karibu nae kinasaba au kimapenzi. Tutajua tu.
 
Yule aliyeua miezi iiyopita si tulisikia ameshikwa? Au ndio huyuhuyu anaendeleza ufirauni wake?

Kuna habari kama hizi zililetwa humu miezi iliyopita.

Kweli kulikuwa na yule aliyekuwa ameua bar maid nadhani Magomeni miezi kadhaa iliyopita. Tusubiri tutasikia zaidi.
 
Back
Top Bottom