Jihadhari na Utapeli wa Photo Point ya Mlimani City

hobi nyingine bana
hivi mpaka leo mnapiga picha ili iweje. Nafuatilia matumizi ya picha hizo naona ni kupoteza kabisa pesa. Sawa! Hata kuvuta sigara ndo ivo ivo
ila poleni, mngeanza hayo mambo zamani msingefanya leo

mkuu majala kimolonafikiri kwanza uwape hongera kwa kufunga ndoa badala ya lawama haya ni moja ya matokeo ya ndoa...wapo wengi pengine na wewe mnatafakari na 40's lini mtaoalabda nikueleze picha ni moja ya kumbukumbu binafsi nilikuwa mke wangu akiniiudhi nikiangalia picha za harusi na mwanangu roho inatullia kabisa...sasa zamani picha zenu zilikuwa nyeupe tupu yawezekana amkuwa na picha kam za sasahivi sikuhizi ukiangalia zina mvuto mnato upendo kama utaangalia hata style za kukaa kwenye picha mlikuwa mnapiga kama mko bar hata picha za harusi...ndio maana kuna watu maalum kama photo nk aprt na uhuni wwao anyway tuwape muda....vijana wekeni kumbukumbu zenu sio mnakufa mnatafuta hata picha za kuweka mbele
 
....Mliandikishiana au ndio mali kauli,....
Mkuu Mfianchi, kama umeisoma posti yangu vema kabisa ni kwamba, pale mahali kuna katalogi yenye bei mbali mbali kwa picha mbalimbali zinazoambatana na zwadi mbalimbali. Unapochagua aina ya bidhaa unazotaka ndipo unalipia kianzio (advance) kutokana na bei ya ile huduma unayotaka, na unapewa risiti. Mpaka ninapoandika ujumbe huu hapa nimetoka hapo mahali nikiwa na risiti yangu na hadithi ni zile zile, wameishiwa sahani, vikombe n.k., ilhali nimeshavilipia na nastahili kupewa.

Ndugu Idimi,

Nadhani umetoa changamoto. Ila neno UTAPELI umeitumia visivyo. Tapeli ni yule anayekuzungusha bila SABABAU ya kueleweka. Makampuni makubwa tu mfano SIGARA kuna wakati Sigara ya Embassy ilikua haipo mtaani sembuse hao wajisiriamali wa Kizalendo???

Wa Tanzania tumezoea mpaka tuone WAGENI wana wekeza ndo tuone SAFI ila akiwekeza MZALENDO basi tatizo DOGO tu utaambiwa TAPELI, ANANYANYASA WAFANYAKAZI, HALIPI KODI n.k.

Wakati nakubaliana na wewe kuhusu kuishiwa na vifaaa (LABDA) na kutokupa taarifa mapema nadhani umefanya vizuri kuweka wazi ila KICHWA cha habari/taarifa ingekuwa kingine na sio UTAPELI.

Ila safi sana, wewe ni mteja mzuri..

Wako FP

Mkuu FP,
Kutangaza kwamba unatoa huduma A ilhali unakuja kutoa huduma B ni wizi. Mie ni binadamu kama wao, ningeambiwa mapema kwamba zile "Fringe Benefits" zinazoambatana na kupiga na kusafisha picha ni "majaliwa", kwamba zinaweza kuwepo ama kutokuwepo, ningewaelewa. Wakati naweka oda waliweka na msisitizo kwamba bidhaa zipo, nilipokwenda kuchukua picha ndipo wakasema hawana na hawajui watazipata lini. Samahani kwa kutumia neno hilo, ila ndio hali halisi waliyo nayo. Leo nimetoka hapo, stori ni zilezile! Hawana.

na wewe una roho nyepesi kama kamasi, mlikubaliana biashara/service..........huenda jamaa kaharibikiwa mitambo au vifaa vimeisha......subiri daaaaaaaah

Barry, ningeambiwa kwamba mtambo ni mbovu wala nisingemaindi, ningewaelewa na kuwa na subira, ila hawasemi ukweli. Hata hivyo, roho yangu hapo hivyo, ni siku 20 zimepita sasa bado nazungushwa.


haahhaaahaaha eti Vikombe saani vimeisha. Kumbe kuna vikombe na sahani spesho kwa ajili ya kazi kama hii. Nilidhaniunaweza kuweka picha kwenye kikombe au sahani yeyote.

Inawezekana kuna baadhi ya vifaa vyao vimeharibika na hawasemi ukweli wa tatizo halisi linalowakabili.

Kabisa


Neema Apson vipi tena photo point yako inachemka? labda wafanyakazi wako wanakuchezea hapo kukuharibia biashara.
Jamani kuna ingine ya Mayfair, Mikocheni mie niliwafurahia huduma zao ila ni picha tu na kusikilizwa kupata nilichotakaga
Carrie,
Hilo jina lina uhusiano na lile la mgombe Ubunge wa Mbeya? Kama jibu ni "NDIYO", madai yangu yanaishia leo!


mkuu majala kimolo nafikiri kwanza uwape hongera kwa kufunga ndoa badala ya lawama haya ni moja ya matokeo ya ndoa...wapo wengi pengine na wewe mnatafakari na 40's lini mtaoalabda nikueleze picha ni moja ya kumbukumbu binafsi nilikuwa mke wangu akiniiudhi nikiangalia picha za harusi na mwanangu roho inatullia kabisa...sasa zamani picha zenu zilikuwa nyeupe tupu yawezekana amkuwa na picha kam za sasahivi sikuhizi ukiangalia zina mvuto mnato upendo kama utaangalia hata style za kukaa kwenye picha mlikuwa mnapiga kama mko bar hata picha za harusi...ndio maana kuna watu maalum kama photo nk aprt na uhuni wao anyway tuwape muda....vijana wekeni kumbukumbu zenu sio mnakufa mnatafuta hata picha za kuweka mbele

Asante!
 
Back
Top Bottom