Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 14,970
- 10,462
Ndugu wana JF,
Sio lengo langu kuvurga biashara ya upigaji na usafishaji picha wa hawa ndugu wa Photo Point ya pale Mlimani City. Lengo tu ni kuwatahadharisha ndugu mnaoenda kupiga picha za matukio mbalimbali pale mahali (kama za Sendoff, Ubarikio, Harusi, birthdays na graduation). Kimsingi huduma hizi zinalipiwa bei kubwa na huambatana na ahadi za zawadi kemkem kama vile kuchapishiwa picha zako katika foronya, mito, vikombe, bakuli, sahani, fulana n.k.
Mnamo tarehe 10 ya mwezi Julai nilienda kupiga picha pale ofisini kwao Mlimani City. Gharama ya picha zile ilikuwa shilini 96,000, ikiwa ni kupiga na kusafisha picha 20 za ukubwa wa 5'x7' na moja ya ukubwa wa 12'x16' ambazo zingewekwa katika albamu pamoja na kuchapishiwa sahani moja yenye picha ya tukio.
Mpaka ninavyoongea hivi sasa albamu wanasema hawana, sahani na vikombe hawana, zimeisha, ilhali vimeshalipiwa katika package zao tulizolipia. Nikiwa katika harakati za kufuatilia picha zangu jana nikakutana na kundi la wateja wengine wenye malalamiko kama yangu wakidai kurejeshewa sehemu ya fedha zao walizolipia huduma.
Mpaka sasa sijajua mustakabali wa albamu na vitu vingine, kwa hiyo ndugu zangu mnaoenda kupiga picha pale Photo Point Mlimani City muwe makini na utapeli huu.