JF ninaomba sala zenu leo ni kura za maoni!

mmmh wewe huwezi kuomba kwani,au unafikiri watu wanapiga kura jf nn?, ccm wanamungu tangu lini, ccm pesa tu jipange kaka na fedha nyingi sana ili ufanikiwe,hilo liko wazi

Haha, jamaa anakuja hapa kutuchora tuu. "Baba, Mama" wote wazito CCM.

Baba pesa ipo na jina kubwa. Mama hivyo hivyo. Hamna mtoto wa kigogo anaeleweka na amebaki kwenye list zaidi yake.... Kwanini wasimpitishe???

Huyu jamaaa bwanaaaa....argggg
 
Wana JF, leo ninakwenda kusimama mbele ya Wabunge wote wa CCM kuomba kupitishwa kwenye kura zao za maoni ya kugombea Ubunge wa EAC, ninaamini niaenda pale nikiiwakilisha JF sasa ni muhimu sana leo tukaweka tofauti ya itikiadi zetu pembeni na kwua kitu kimoja katika kuombeana na kutakiana heri, kupita kwangu ni kupita kwa JF.

Hapo tu umeshalikoroga....

Tangu lini JF ikawakilishwa kwenye chaguzi za kisiasa? Kwani JF ni jimbo au taasisi inayotafuta uwakilishi??

Naomba ndugu yangu uwe mkweli......Huko unaenda mwenyewe kwa maslahi yako binafsi (mambo ya kuchumia tumbo) na chama chenu....JF haihusiki na ugombea wako na hata kwenye mikakati yako...hakuna hata moja linaloihusu JF!!!
 
Mimi nakutakia kila la kheri Bro! You have my blessings and I pray for you.

Kikubwa kama utabahatika kupata nafasi hiyo, basi kaiwakilishe vyema Nchi yako, epuka ulevi wa madaraka na pia uwe unajibu au kutatuakero za watanzania kulingana na uwezo utakao kuwa nao na pia usiwe muoga kuwakilisha maoni na matatizo ya watanzania walio wengi ambayo kwa njia moja au nyingine umekua ukiyapata kupitia hapa JF.

Naamini kwa dhati kabisa kama ukipata nafasi hiyo, na usipobadirika kutokana na ulevi wa madaraka ambao viongozi wengi wamekua wakibadirika. Utakua muwakilishi mzuri sana wa mahitaji ya watanzania tulio wengi maana uwepo wako JF umejifunza mengi kuhusu nini hasa watanzania wanakitaka katika nchi yao, pia ndani ya JF unapata muelekeo wa nchi ilipo na inapokwenda.

Namalizia kwa kukutakia kila la kheri, watakao kubeza wasikilize, kilicho muhimu chukua, kibaya waachie. Na hata ikitokea umeikosa nafasi hiyo, usikate tamaa. Elewa huo ni mwanzo tu wa kuelekea kule unakotaka kwenda. Safari ndio umeishaianza usirudi nyuma...hata ukikosa, tulia na ujipange kwa chaguzi nyingine naamin utapata tu.

WAKATABAHU!
 
Wewe W.J. Malecela vipi? this is a home of GTs. Badala ya kuomba NONDO wewe unaomba SALA, kwani unakwenda kugombea upadri, ukasisi, ushehe, uchungaji?

Mwenzako (CCM) aliwahi kuulizwa kirefu cha SADC na Tundu Lissu akapiga chini. Anyway kwakuwa huko ni CCM wenzako policy inayo aplly ni WHO KNOWS YOU and HOW MUCH UMEHONGA. Lakini kwakuwa manakwenda kuwakilisha Tanzania first yopu have to know the MISSION and VISION of EAC? What are the stand of Tz GOVT kwenye masuala kama common currency, Ardhi, common market, free labour movements visa vi other members States. Organogram of EAC how it functions kufikia mamuzi etc, SWOT of EAC

Hayo ni mambo machache ambayo inabidi uyafahamu kabla hujaingia kwenye intreview
 
Kwa wasiomuelewa William ni wa kwanza kushoto katika hii picha.

386456_289782994376454_100000342668655_1028823_1598867757_n.jpg
 
Sina hakika hata kama unafahamu la kufanya ukichaguliwa kuwa mbunge.

una uhakika na nani? wewe jike dume tulia kwani nikikuambia utaje hata watu wanne wanaogombea huwajui na huna mawasiliano nao, huyu williama any time ukiwa na maoni unaweza kumpa na yakamfikia au ushauri, acha unazi wewe nenda chit chat
 
Sidhani kama chama chako kinahitaji sala, hiyo si sera ya chama chako, chama chako kinahitaji uwe na fedha za kutosha za kutoa rushwa kuwashinda wengine, matusi, propanganda n.k ambavyo vyote hivyo hapa JF hawatoe hiyo huduma wala msaada huo. Wenye kuhitaji sala ni wale walianza na mungu na kumaliza huko Arumeru
 
Ccm walivyowezi kama huna hela za kuwahonga lazm wakuumize.kila lakheri
 
Atabadilika kuvaa mikufu ya nanga kwa nje, lakini ubongo wote umejaa nanga.
It does not make sense to me.

Tunataka watu wanaoweza kuongoza pamoja na mapungufu yao, huyu hafai kwa mchuzi ama kulumanga.

Kila la heri...badilika sasa mkuu ubaharia weka pembeni kuva mikufu ya nanga.
 
Mwanzo wa safari ni hatua; kwa kuwa umethubutu na kuvuka kigingi cha kwanza. Nakutakia ushindi!
 
una uhakika na nani? wewe jike dume tulia kwani nikikuambia utaje hata watu wanne wanaogombea huwajui na huna mawasiliano nao, huyu williama any time ukiwa na maoni unaweza kumpa na yakamfikia au ushauri, acha unazi wewe nenda chit chat
Usitukane watu usifikiri keyboard zetu hazina hizo herufi za matusi jiheshimu. Kama wewe ni mmoja wa wapambe wake basi hafai.
 
Asante, hii inadhihirisha ukomavu wako wa kujadili mambo ya msingi.
Wala sikushangai, wenzako wanaimba wewe unataka tuanze kulia hapa. Njoo chit chat tuongelee ya jike dume.

Back to my point, hana sifa na wala hajitambui kama kiongozi.

una uhakika na nani? wewe jike dume tulia kwani nikikuambia utaje hata watu wanne wanaogombea huwajui na huna mawasiliano nao, huyu williama any time ukiwa na maoni unaweza kumpa na yakamfikia au ushauri, acha unazi wewe nenda chit chat
 
Back
Top Bottom