JF Man & Woman Of The Year 2011 Competition

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696

NB: tafadhali Angalia Update 1 na
Update 2: Chni ya main Post.

Angalizo: Mods kwa hekima mnaombwa msiiamishe thread hii wala kuichanganya na nyingine yoyote.

Wanajamii; Wana JF

Mwaka 2010 tulifanya mchakato wa kumpata JF Man & Woman of The Year 2010. Shindano kama hili pia lilifanyika Mwaka 2009.

  • Washindi wa 2009 "JF SuperLady" au "Celebrity wa JF" alikuwa WoS (Woman of Substance)
  • Washindi wa 2010 "Regia Mtema" (RIP) - Kwa JF Woman of the Year 2010
  • na Nyani Ngabu alifungana na Asprin kama "JF Man of The Year 2010"

Mchakato wote mpaka mshindi kupatikana unaweza kuupitia hapa:

https://www.jamiiforums.com/complaint...ar-2010-a.html

Mwaka huu tunataka kuuboresha mchakato huu na tunapenda kupitia mchakato huu kupata washiriki wengi na kuipa taswira JF kuwa kuna watu wanafakubalika katika hii online community.
Mwaka huu 2012 tunafanya mchakato wa kuwapata Washindi wa 2011 (lakini michango yao ya sasa inakubalika iingizwe 2011).Tulichelewa kufanya kwa sababu zilizo nje ya uwezo. Categories za Mwaka huu ni:

  • JF WOMAN OF THE YEAR 2011 na pia JF MAN OF THE YEAR 2011 (Overall).

  • Lakini Pia Tutaongeza Category Moja: "JF QUEEN OF MMU" and "JF KING OF MMU"

Katika mchakato wa awali tutapendekeza majina mbalimbali katika category hizo mbili kulingana na unavyoona anakubalika na mwishoni tutachagua watatu kutoka katika kila category na kisha kuwapambanisha kupitia JF POLLS. Mwaka huu napendekeza tutoe zawadi yenye hadhi fulani kwa washindi ili kutoa changamoto za umakini katika mabandiko haba jamvini. Tutajulishana zawadi hizi tutakapoingia katika mchakato wa Kupiga kura.

Vigezo vifuatavyo vizingatiwe katika kutoa mapendekezo ya watakaoshindanishwa katika hizi KURA ZA MAONI:

1. Kama ni category ya WOMAN lazima uwe umemdhania kuwa unayempendekeza ni Mwanamke na una ushahidi wa Kimazingira. katika hali ya mashaka, uhakikisho wa jinsia kutoka kwa muhusika aliyependekezwa utafanya akubalike. Uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi - JEC (Superman) ya Shindano hili utakuwa ni Final. wote mnahakikishiwa hakutakuwa na Uchakachuaji.

2. Kama ni category ya MAN lazima uwe umemdhania kuwa unayempendekeza ni Mwanaume na una ushahidi wa Kimazingira. katika hali ya mashaka, uhakikisho wa jinsia kutoka kwa muhusika aliyependekezwa utafanya akubalike.

Katika 1 na 2: Uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya JF (JEC) wa Shindano hili utakuwa ni Final. wote mnahakikishiwa hakutakuwa na Uchakachuaji.

3. Anayependekezwa lazima kuwe na ushahidi unaoonyesha kuwa ni Mwana JF aliyebobea hasa kutokana na Threads alizozianzisha na pia post anazobandika. Vyote lazima viwe na impact chanya kwa wasomaji wa JF.

4. Awe ni mwenye uwezo wa kusimamia hoja zake na kuzijibu kikamilifu bila jazba na kwa umahiri wa hali ya juu pale ambapo anapata challenge toka kwa wachangiaji.

5. Awe ni mwenye ushawishi wa hali ya juu katika mabandiko anyochangia walau kwa muonekano wa wachangiaji kuunga mkono hoja zake.

6. Kwa Wanaogombea Overall tittle, asibobee kwenye Jukwaa moja tu. Walau awe mchangiaji mzuri wa majukwaa yasiyopungua mawili. Kwa wale wanaopendekezwa MMU basi akubalike katika jumuiya ya MMU

7. Asiwe mtu wa shari katika majibizano kiasi cha kupelekea Mods kumpa "BAN".

8. Aonekane wazi katika mabandiko yake anaweza akahisiwa kuwa Kiongozi Mzuri.

9. Awe Mchangiaji ambaye ni active walau mara moja kwa wiki. Ikiwa zaidi ni vizuri zaidi.

10. Awe ni mtu asiyeogopa kukemea mabandiko yenye lengo la kutukana, kudhalilisha, kubagua, kuleta mfarakano na kutokuelewana baina ya wanachama wa JF.

Sasa kila moja yuko huru kutoa mapendekezo yake ya nani wanastahili kuingia katika tatu bora katika kila category.

Nashauri kuwa mapendekezo ya majina yaambatane na maelezo mafupi.

Uwanja ni wenu. Karibuni sasa mto mapendekezo au NOMINATIONS.

Wasalaam
Superman-Logo.jpg

Signed Seal:

Superman

Mwenyekiti - Tume Ya Uchaguzi ya JF (JEC)

images

UPDATE 1:

Baada ya Mchakato wa Kura za maoni Kumalizika na Kusikiliza Rufaa zote, Tume ya Uchaguzi ya JF (JEC) imepitisha Majina ya Wagombea Watakaoingia Fainali na Kupigiwa Polls.. Washindi hawa sasa Watashindanishwa kwa Polls ili kupata Mshindi wa kila Category. Majina yaliyopitishwa baada ya Wagombea wengi sana kuchujwa ni:

Overall JF Man of The Year 2011
1. BAK – Kura 4
2. Aspirin – Kura 2
3. EMT - Kura 3

Overall JF Woman of The Year 2011
1. Ashadii – Kura 11
2. FaizaFox – Kura 3

King of MMU 2011
1. Mbu – Kura 5
2. The Boss – Kura 6

Queen of MMU 2011
1. Lizzy – Kura 8
2. Ashadii – Kura 7
Kwa kuwa hatujapokea rufaa nyingine. Sasa tutafanya upadate katika post Kuu. Na kisha kuelekea kwenye POLLS.

Signed & Sealed:

Superman-Logo.jpg

Superman
Chairman - JEC

Update 2:

MODS: Naomba Polls zikimalizika Threads zote hapa chini ziunganishwe:
https://www.jamiiforums.com/mahusia...n-and-woman-of-the-year-2011-competition.html

Kampeni na Upigaji wa Kura na Umeshaanza kwa Categories Zote:

Tafadhali Piga Kura Yako Hapa:

Sasa tunakaribisha Mapendekezo au Nominations . . . .
 
Halafu......Kwa nini umeiweka MMU?........Si ungeiweka kwenye CCA Forum?....

Mkuu Forum yake has huwa inakuwa kule Celebrities. Niejaribu kuiweka kule, naona imegoma kwenye New Post. Nimewaandikia Mods. Wote wamekula jiwe. I hope wanaweza kuhamishia Jukwaa husika.

Niweka hapa safari hii kwa kuwa pia tuna Washindi wa MMU. Its all about people, who know who etc.
 
Wewe Superman, kwanza bado nakudai hela zangu wewe. Na usilete uswahili wako hapa.

Pili, mimi nilikuwa mshindi pekee. Sikufungana na mtu. Nilikuwa Man of the Year mwenyewe. Kwanza Aspirin hakuwepo hata kwenye wale finalists wengine.

Wachuchu ndo walifungana. Alikuwa marehemu Regia na Gaijin.

Sasa vipi hela zangu?
 
hehe hapa patamu sasa
 
NN acha kuniadhirisha bila sababu bana! lol

Unakumbuka ulisema nimpe Maxence? Mbona nilimpa kama ulivyoagiza? Muulize au Mdai receipt.

Hata marehemu Regia (RIP) alisema ziingie mfuko wa JF nikamkabidhi Maxence. Mimi muadilifu bana si ndo maana dingi wa JEC.

Halafu mlifungana kisha ukatumia ID nyingine kujipigia. Safari hii kamati iko makini.

Lakini tuko pamoja. Huwezi kuchangia katika zawadi?
 
Sasa unatoa madai yasiyo na ukweli wowote. Sikutumia ID ingine kujipigia kura. Nilishinda kihalali kabisa. Ukiendelea kunipaka matope nitakushitaki.

Kuhusu pesa, mimi Mubyazi hakunipa risiti. Sasa sijui alizinywea bia au vipi. Ngoja nitamtafuta nimdai risiti.
 
hehe hapa patamu sasa

Kabanakabana usimsikilize huyu Nyani Ngabu. Unajua mimi ni mtu na heshima zangu. Hata JK, Obama, Mandela, Bill gates, Pope John nk ni jamaa zangu wa karibu na wananiheshimu. Nitamzikaje laki moja bana anataka kunihadhirisha tu?

Can you imagine rafiki yangu Queen Elizabeth au Mama Salma kikwete na Dr. Slaa wakisikia watanifikiriaje?

Ndo maana Mzee Sabodo na Mengi waliniambia NN si mtu Mzuri.
 
Niombe radhi kwa kunikashifu hadharani namna hii.
 
NN acha kuniadhirisha bila sababu bana! lol

Unakumbuka ulisema nimpe Maxence? Mbona nilimpa kama ulivyoagiza? Muulize au Mdai receipt.

Hata marehemu Regia (RIP) alisema ziingie mfuko wa JF nikamkabidhi Maxence. Mimi muadilifu bana si ndo maana dingi wa JEC.

Halafu mlifungana kisha ukatumia ID nyingine kujipigia. Safari hii kamati iko makini.

Lakini tuko pamoja. Huwezi kuchangia katika zawadi?

Aisee wewe ni mkali, yaani unakumbushwa deni, unapanguwa halafu unampamba kidogo then unampiga mziga kabisa!! teeh teteteteh!!
 
nakumbuka kama nadai elfu hamsini.... kweli siku zimeenda, nimekua mzee sasa, ni muda wa kuweka bakora chini na kurudi kufukuzia alawanzi,
 
Back
Top Bottom