Elections 2010 Jeshi la polisi weledi wao na siasa za igunga (Tanzania)

Mghaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
320
127
Mimi nasikia kichefuchefu na fedheha namna polisi wanavyofanya kazi yao katika kusimamia amani jimbo la uchaguzi Igunga. Kwa kweli si polisi tena bali ni chama cha siasa ambacho hakina usajili lakini kina uhalali wa kidola. Watanzania wenzangu nataka kuwakumbushia matukio kidogo ya namna polisi walivyoacha majukumu yao na kuendesha siasa.

Tukio la kwanza kabisa lililowapa taabu polisi ni lile la mkuu wa Wilaya Igunga kuvunja sheria, kanuni na taratibu za kuendesha siasa Igunga. Ikumbukwe DC ni raia wa kawaida kabisa anapokua amefanya tendo la kihalifu, CHADEMA walimshika wakamfungulia mashitaki ya kuendesha siasa kinyume na utaratibu na hasa pale ambapo sehemu ile iliandaliwa kufanyika mkutano wa chama kingine. Polisi hawa ndio waliobuni na kutafuta sababu za kumuepusha DC yule na fedheha ya kuingia kichwa kichwa katika siasa kwa kugeuza hoja ya uhalifu kuwa hoja ya kidini inayohusu kuvuliwa hijabu.

Kiongozi wa CUF amepigwa na wanachama wa CCM akiwapo kiongozi wa Umoja wa Vijana mpaka leo hakuna anaejua nini kinaendelea? Viongozi wa CCM wanatembea na silaha na wengine kuzitumia watakavyo hakuna kinachoendelea, wao polisi kimya kwa sababu tu anae wapa mkate ndiye anayeongoza kuvunja kanuni.

Mabango ya CHADEMA na picha za mgombea zimechanwa watuhumiwa wameshikwa polisi kimya! Vijana watatu wa CDM wamekamatwa huku wakitekeleza haki yao ya msingi ya kuwasikiliza wagombea ili wachambue pumba na mchele siku ya siku ikifika. Kukamatwa kwa vijana hawa kulichochewa na kiongozi wa serikali anaepaswa kuilinda haki hiyo kwa kuuliza kama watu na washabiki wa CDM wapo pale kwenye mkutano wao? Vijana kwa kujua ilikuwa haki na sheria kuwapo kwao wakajitokeza kuonyesha mikono yao, green guard wakawashughulikia, na kuwapeleka polisi, wale polisi badala ya kufanya uchunguzi na kuwambia CCM wakiwa kwenye majukwaa ya siasa ni mwiko kubaguana kwa kuanza kuulizana itikadi au chama cha mtu wamekaa kimya.

Unafanya hivyo kwa masilahi ya nani na kwa kitu gani kama si kutaka kuwatia muhuri watu wengine ili uwadhuru. Kosa kama hilo tena lilirudiwa na Magufuli, hivi CCM wanatupeleka wapi? tumeanza kuulizana itikadi ili kuwajua wasio wetu ili iweje? Kwa hili nahisi tumeanza kuulizana hata dini nje ya majukwaa na tunafanya hivyo kuwajua wasio wetu ili iweje?

Mlolongo mzima wa matukio ya kisiasa katika jimbo la Igunga polisi wanafanya kazi ya CCM. Sasa kubwa ni pale ambapo Mgulu na jeshi hili lilivyokosa weledi kwa kwenda katika vyombo vya habari na kuwambia eti Mh. Esther Bulaya ameliomba msamaha jeshi la polisi, kwanza nani amemuuliza hizo habari, na anazisema ili kumfurahisha nani? Na kwa masilahi ya nani? Tumeona CCM ikidhalilisha watumishi wa jeshi la polisi mara ngapi na jeshi hilo likitulia kama ng'ombe anayepewa mashudu ili akamuliwe? Watanzania wanajiuliza hivi makosa haya yangefaywa na viongozi au washabiki wa vyama vingine hatua hizi zingefanana?

Polisi muogopeni Mungu na simamieni haki katika misingi yake ya haki kwani hapo mlipo ni fedha za kila mtanzania zinatumika kuwalisheni na kuwavalisheni. Bahati mbaya ama kwa kutokuelewa au kwa makusudi mumeamua kujitambulisha katika upande unaominya demokrasia na haki za msingi za raia kwa masilahi ya wakubwa wenu. Kwa kufanya hivyo mnaiandalia nchi vurugu ambazo si za lazima, na niombe niwakumbishe katika philosofia ya uvumilivu kuwa kama kuwa hai na mauti hakuna tofauti basi kifo huwa ndio chaguo la mwanadamu. Tanzania ninayoifahamu na watanzania hawa bado hapo ni mbali sana lakini vitendo vyenu vinachochea kasi ya mwendo kuelekea hapo mnapopaona ni mbali. Si ajabu tukafika katika muda mfupi ujao. Ni wahakikishie kuwa wakati huo ukifika hata maghala yenu ya silaha mtayakimbia, magari ya upupu mtayatelekeza na silaha zenu mikononi zitakuwa mzigo wakati mkikimbia kujisalimisha. Katika Busara ya kawaida ebu isaidieni CCM kutowapeleka kusiko kwa kulinda haki na kutoa usawa mbele ya macho ya umma.

Mungu ibariki Tanzania, alibariki jeshi la polishi na vyama vya siasa kwa kuwaaangazia nuru ya amani na upendo, ili Tanzania tuitakae ije bila kutoana ngeu na jasho jingi.


Bwana awe nanyi
 
Si ajabu tukafika katika muda mfupi ujao. Ni wahakikishie kuwa wakati huo ukifika hata maghala yenu ya silaha mtayakimbia, magari ya upupu mtayatelekeza na silaha zenu mikononi zitakuwa mzigo wakati mkikimbia kujisalimisha. Katika Busara ya kawaida ebu isaidieni CCM kutowapeleka kusiko kwa kulinda haki na kutoa usawa mbele ya macho ya umma.

Mghaka, asante kwa wazo la leo. Tumetafakari na tumekuelewa asante kwa kuwaelimisha ndugu zetu wa polisi
 
Wanasiasa ndio wanaotugawa,,,,tulitambue kwanza hilo,,,,wao ndio wanahubiri UDINI,UKABILA NA HATA UMAJIMBO,mbona raia tunaish kwa amani,,,huko Igunga wanasiasa ndio waliopandikiza miche ya chuki na vurugu,,,,,raia wanahisi upinzan ni CHUKI,,,,,,,,
 
Back
Top Bottom