Jeshi la polisi - na leseni mpya za class c

terabojo

JF-Expert Member
Aug 3, 2010
215
45
Wana JF napongeza uamuzi wa waziri wa mambo ya ndani kutoawiki moja zaidi kwa watu na hasa madereva wa mabasi na magari makubwa ili waweze kupata hiyo leseni mpya. Wasi wasi wangu ni kwamba hiyo wiki haitoshi kwa kuwa kama mtu hana inabidi akapate mafunzo ktk chuo cha usafirishaji - si chini ya wiki 2, akifaulu aende TRA aandikishe na aende traffic waka mpe road test ndio aende tra kupata leseni. Mzunguko huo si chini ya siku 30.
Suali ni je waziri hajui mlolongo huo?? Nawakilisha
 
Jamani mwaka 2012 Uwe ni mwaka wa kutokuwazoesha Trafiki kupata rushwa, mimi binafsi huwa nalipa faini kwani mi nina ugonvi na askari wa bongo, nadhani hii issue ya Class C ni issue ya kutaka kuwaumiza jamaa zetu madreva.

Hebu jitahidi kutokuwazoesha rushwa hawa wang'ang'anizi wa rushwa.
 
Tusikurupuke kulaumu wakuu, hii notisi ilikuwapo toka mwaka jana June. Vichwa ngumu tu vya hawa madereva hakina kingine.

Kwa kutotaka kufuata deadlines na hulka yetu ya kutotaka kufanya yatupasayo timely kwa mara nyingine inawapa ulaji Traffic police. Moshi unaipata kwa 200,000
 
Back
Top Bottom