Jeshi la Kenya lililopelekwa nchini Congo linatia aibu

Akilihuru

JF-Expert Member
May 20, 2022
1,447
2,838
Kwema wakuu,

Wengi tulijua tu kwamba jeshi la Kenya halitaweza hata kurusha jiwe kwa kundi hilo la waasi wa M23, kutokana na jeshi hilo kuliogopa vibaya kundi hilo. Sasa hali inazidi kuwa mbaya na kundi hilo linazidi kuteka maeneo mbele ya macho ya jeshi la Kenya huku Wakenya wakiangalia tu.

Screenshot_20230127-200538.jpg


Waasi wa M23 wanadai kuuteka mji wa Kitshanga/Kitchanga katika eneo la Masisi nchini DR Congo baada ua siku tatu za mapigano makali.

Mashirika ya Kiraia na Majeshi ya Umoja wa Mataifa nchini DRC yamelaani mashambulizi ya kijeshi ya M23, ambayo sasayamesukuma zaidi ya raia laki nne kuyakimbia makazi yao.

Redio ya Okapi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa iliripoti kuanguka kwa Kitshanga kwa waasi.
 
Kwema wakuu,

Wengi tulijua tu kwamba jeshi la Kenya halitaweza hata kurusha jiwe kwa kundi hilo la waasi wa M23, kutokana na jeshi hilo kuliogopa vibaya kundi hilo. Sasa hali inazidi kuwa mbaya na kundi hilo linazidi kuteka maeneo mbele ya macho ya jeshi la Kenya huku wakenya wakiangalia tu.

Kwan ni wakenye peke yao wanaolinda?
 
Tusiwalaumu lakini hua nafikiri pengine hayo majeshi ya kulinda amani hua Wana maelekezo maalum, kwa sababu haiwezekani m23 waendelee kusonga mbele na wakati jeshi la kulinda amani Lina silaha bora kuliko wao
Mbona Tanzania tulipopewa hadhi ya kuongoza hiyo oparation ya kikanda tuliwaangamiza M23 wote mpaka wakakimbilia Rwanda na Uganda
 
Kwema wakuu,

Wengi tulijua tu kwamba jeshi la Kenya halitaweza hata kurusha jiwe kwa kundi hilo la waasi wa M23, kutokana na jeshi hilo kuliogopa vibaya kundi hilo. Sasa hali inazidi kuwa mbaya na kundi hilo linazidi kuteka maeneo mbele ya macho ya jeshi la Kenya huku wakenya wakiangalia tu.
Wana familia zinawasubiri nyumbani kwenye amani tupu tofauti na wenzao
 
Back
Top Bottom