Jengo Maarufu Zanzibar kwa utalii, Beit Al Ajaib laporomoka

Duuh! Inasikitisha sana kwa kushindwa kutunza vivutio vyetu. Nilibahatika kuingia hapo mjengoni mwaka 2010. Palikuwa na mvuto wa ajabu hasa zile ngazi zake ambazo zilikuwa very steep.
 
dr husein mwinyi kwa ari aliyonayo namfahamu sana hakika muda siyo mrefu litarudi katika hali yake ya awali inshaallah
 
Habari Wana Bodi,

kutokana na taarifa/picha nlizopata kutoka Zanzibar (Kwa Rafiki Alie Kwenye Mapumziko Ya Xmass) muda huu jengo la Baytul Ajaab Zanzibar limeanguka upande mmoja, inasememkana watu 6 wamefukiwa na kifusi cha mnara pamoja na upande wa nyumba ulioanguka.

Wana bodi mliopo Zanzibar, tupeni updates kadri zitakavyo patikana juu ya majeruhi na waliopoteza maisha.

updates
20201225_153232.jpeg
20201225_153153.jpeg
20201225_153007.jpeg
20201225_153148.jpeg
 

Attachments

  • 20201225_153149.jpeg
    20201225_153149.jpeg
    54.1 KB · Views: 1
Sasa tokea mwaka 18 na ngapi sijui.Acha lianguke. Walikuwa hawafanyi rénovation?Majengo ya mwarabu hakuna uimara.
Nasikia mwarabu mwaka juzi alitaka kuleta wakandarasi toka nje waje kulikarabati kisasa, serikali ikagoma, wakasema wapewe wao hela ili walikarabati.

Mwaka jana 2019 waliandikishana mkataba wa makubaliano na nchi ya oman (Nakumbuka kwenye habari alioneshwa Waziri Wa Utamaduni Wa Oman alikuja na bonge la meli la mfalme wao) ya ukarabati wa jengo hilo, waziri wa utamaduni wa oman alivyofika huko zanzibar alisema "ZANZIBAR NI KATI YA NCHI 10 ZILIZOBAKIA TU DUNIANI, KWA KUWA NA URITHI WA KALE WA MAKASRI YA WAFALME (Akiashiria Kasri hilo la maajabu)" hivo wameamua kuikarabati nyumba hio ili iendelee kuwepo.

Mwarabu huyo wa oman akamwaga mabilioni mengi sana ya pesa ili ifanyike hio renovation kuiweka zanzibar katika nchi 10 zilizobakia kuwa na urithi wa kale, ila watu wamekula mshiko.
 
Sasa tokea mwaka 18 na ngapi sijui.Acha lianguke. Walikuwa hawafanyi rénovation?Majengo ya mwarabu hakuna uimara.
hebu nitajie umri wa hili jengo kesha tuone kama limekuwa historia au ni la miaka mi2 kama unavohisi majengo ya warabu sio imara🐸🐸
 
Sasa tokea mwaka 18 na ngapi sijui.Acha lianguke. Walikuwa hawafanyi rénovation?Majengo ya mwarabu hakuna uimara.
Jumba hilo maarufu kama Beit-al-Ajaib kwa lugha ya Kiarabu lilijengwa mwaka 1883 ambapo ni miongoni mwa vitu vya kipekee vinavyopatikana katika visiwa vya Zanzibar na limehifadhi kumbukumbu na historia ndefu kuhusu ubunifu na maendeleo ya Zanzibar.
 
Lilikuwa likifanyiwa ukarabati.

Nilikuwa naenda kuangalia movies Zanzibar International Film Festival hapo.

Inasemekana Sultani alivyolijenga, kuna nguzo fulani katikati aliweka maiti za watumwa.
 
Back
Top Bottom