Jengo Maarufu Zanzibar kwa utalii, Beit Al Ajaib laporomoka

silent lion

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
1,164
1,544
Jengo hili lilikua ndio sura ya mji Mkongwe Zanzibar na kivutio Kiki kikubwa cha utaliii, lakini serekali imeshindwa kulitunza.

Serekali ya Oman 🇴🇲 ilikua tayari kulikarabati lakini inaonekana wamefanyiwa urasimu na watendaji wenye tamaa.

===

Jengo la Beit al Ajaib lilijengwa na sultan wa pili wa Zanzibar, Barghash bin Said mwaka 1883 likilengwa kuwa jengo la kasri la sherehe na sehemu maalum ya mapokezi kwa wageni

Liliitwa Jumba la Ajabu, kwa kiarabu Beit Al Ajaib kwa kuwa lilikuwa ni jengo la kwanza kuwa na umeme Zanzibar, la kwanza Afrika Mashariki kwa kuwa na 'elevator'

Jengo hilo limeonekana kuporomoka, Leo Desemba 25, Mtu mmoja ameokolewa katika tukio hilo.

1.jpg
2.jpg
3.jpg
4.jpg
5.jpg

 
Likitakiwa matengenezo makini ili liwe kumbukumbu ya muda mrefu zaidi. Kwakuwa lilishachoka na halikukarabatiwa, wacha liporomoke. Wafanye usafi tu, yabaki mgofu.
 
Pia naona ni sehemu tu ya jengo ndio imedondoka, kuna wataalam wa restoration hapo Zanzibar waliopikwa vyema toka Ardhi University, waonyeshe sasa makali yao hapo
Unanichekesha wewe, eti kutoka Ardhi University. Haha. Wataalam waliochomekwa chomekwa kutokana na kuibiwa nasafi za wengine na kuwadhulumu. Hakuna kitu watanzania tunaweza zaidi ya majungu na roho mbaya.
 
Back
Top Bottom