Jenerali Ulimwengu kanena: Huwezi kujadili katiba mpya bila kuujadili muungana

mi naona huu muungano una matokeo matatu kwanza serikali tatu, pili serikali moja, tatu usiwepo.
turudi kwenye tanganyika yetu kwanini tunaiogopa hata kuitamka tu naona viongozi wanaita tanzania bara kwani znz iliungana na tanzania bara?? tukae chini tujadiliane Tuamue moja mapema tuokoe muda na mawazo yetu tuyapeleke kwenye maendeleo tusipotezeane wakati kwa vitu vilivyo wazi
 
Wakati mataifa makubwa ya ulaya wana fanya juhudi ili muungano wao wa EU uweze kushamiri na huku sisi waafrica tuna fikiria kubomoa hiyo miungano iliyopo. Je tutafika.......?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa ni kikwazo cha maendeleo hata ya EAU. Yatupasa tusahau tofauti zetu na tutafute mbinu ya kuudumisha huu muungano ajili ya maedeleo na usalama wa taifa letu.

Utakapo vunjika faida itakuwa kwa mabeberu na hasara itakuwa kwa watanzania.

Ni juu ya viongozi kukubaliana na wananchi juu ya aina ya muungano utakao tuwezesha kukabiliana na mafisadi.
Muungano wetu haueleweki-ndo maana hakuna mtu anayeweza kukupa faida za muungano-hata mukulu kukupa.
EU,USA wao wana terms zao zinazoeleweka ndio maana husikii minong'ono ya malalamiko-huu muungano na zenji ni sawa tumewapa ruksa wazenji washee mali na kuacha wazawa hapa tunataabika-SIJUI TUNA VIONGOZI WA MTINDO GANI.
 
Back
Top Bottom