Jenerali Ulimwengu kanena: Huwezi kujadili katiba mpya bila kuujadili muungana

KALABASH

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
493
206
Katika kipindi cha majadiliano leo saa kumi na mbili jioni kilichorushwa na Sauti ya Ujerumani kikishirikisha jopo la watu wanne Jenerali Ulimwengu amekuwa muwazi na kusema kuwa huwezi kujadili katiba mpya bila kujadili muungano kwa uwazi. mwandishi Salim kutoka Zanzibar kasema haiwezekani mtu atoe amri kuwa lolote mnaweza kujadili isipokuwa uwepo wa muungano. Kwa maoni ya wana jopo mjadala wa kitaifa ufanyike na watu waulizwe kama wanautaka muungano au la na kama wanautaka uwe wa muundo gani.
Na wana JF mnasemaje?
 
Hayo ndiyo maneno! Muungano faida zake ni kiduchu sana, japo ni muhimu kuwepo. Lakini mimi ninaitaka Tanganyika yangu, iwepo na Zanzibar, kisha serekali ya shirikisho yenye wizara chache!
 
Wakati mataifa makubwa ya ulaya wana fanya juhudi ili muungano wao wa EU uweze kushamiri na huku sisi waafrica tuna fikiria kubomoa hiyo miungano iliyopo. Je tutafika.......?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa ni kikwazo cha maendeleo hata ya EAU. Yatupasa tusahau tofauti zetu na tutafute mbinu ya kuudumisha huu muungano ajili ya maedeleo na usalama wa taifa letu.

Utakapo vunjika faida itakuwa kwa mabeberu na hasara itakuwa kwa watanzania.

Ni juu ya viongozi kukubaliana na wananchi juu ya aina ya muungano utakao tuwezesha kukabiliana na mafisadi.
 
G. Ulimwengu amesema kuwa pamoja na kuwa na hamu ya Katiba mpya lakini kwanza tuangalie ninini chanzo hii nchi iitwayo Tanzania, ambapo utaona ni muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar.

Kwakuwa kunamalalamiko mengi ya muungano wenyewe kutoka kila upande, na hii ni kwasababu muungano wenyewe tokea ulipoasisiwa una TENGE (haukukaa sawa) huwezi kuandika katiba mpya bila ya kuwepo mjadala wa wazi wa muungano wenyewe ikiwa tuna nia njema ya hiyo katiba.

Na na ni lazima kutoa fursa kwa wananchi kuujadili huu muungano ikiwa wanauhitaji au hawauhitaji, na ikiwa unahitajika uwe wa aina gani ? Na pia amesema huwezi kujifanya mtawala na kuwaamulia wananchi nini wanataka na kuwalazimisha kuwa wasijadili muungano na umakamo wa raisi (na hapa kazungumza kwa hisia kali unataka kuandika katiba ya nani ikiwa muungano usijadiliwe), kufanya hivyo ni kupoteza pesa na kuwapotezea Watanzania wakati wao na kuwachezea akili zao kwa7bu matatizo yaliopo bado yataendelea kuwepo huenda yakawa makubwa zaid.
 
Kama hatuwezi kuupiga chini basi tuwe na serikali 3...vinginevyo tuachane na usumbufu wa muungano huu feki
 
somehow, somewhere this is true....... Ilipaswa kupiga kura ya maoni pande zote mbili kujadili mustakabali wa muungano, maana chokochoko zimezidi. Ili ijulikane kama kuujenga upya au kuuvunja then tuje kwenye swala la katiba....
 
Mimi naona hizi taaasisi zetu zituunganishe ili tuweze kumlazimisha JK kuitisha kura ya maoni dhidi ya huu muungano feki, nina hamu ya Tanganyika yetu, wala tusione aibu kuiga Wazenji kutia sindikizo la kura ya maoni kupitia taasisi zao.
 
Wakati mataifa makubwa ya ulaya wana fanya juhudi ili muungano wao wa EU uweze kushamiri na huku sisi waafrica tuna fikiria kubomoa hiyo miungano iliyopo. Je tutafika.......?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa ni kikwazo cha maendeleo hata ya EAU. Yatupasa tusahau tofauti zetu na tutafute mbinu ya kuudumisha huu muungano ajili ya maedeleo na usalama wa taifa letu.

Utakapo vunjika faida itakuwa kwa mabeberu na hasara itakuwa kwa watanzania.

Ni juu ya viongozi kukubaliana na wananchi juu ya aina ya muungano utakao tuwezesha kukabiliana na mafisadi.

Katika hicho kipindi cha majadiliano Ulimwengu kaizungumzia EU kwa mtizamo tofauti na wa kwako ambao nami naafiki ni sahihi: kwamba katika EU kila nchi imebaki na identity yake na mamlaka yake isipokuwa kuna mambo ambayo wamekubaliana kushirikiana kimkataba. Akaendelea kusema Zanzibar inapokuwa na malalamiko yanayohusu muungano haina mwenza wa kumlalamikia maana Tanganyika waliyoungana nayo haipo. Haina mantiki kwa Za nzibar kuilalamikia serikali ya muungano maana si patner wake kwani Zanzibar ni sehemu ya serikali ya muungano.
 
Wakati mataifa makubwa ya ulaya wana fanya juhudi ili muungano wao wa EU uweze kushamiri na huku sisi waafrica tuna fikiria kubomoa hiyo miungano iliyopo. Je tutafika.......?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa ni kikwazo cha maendeleo hata ya EAU. Yatupasa tusahau tofauti zetu na tutafute mbinu ya kuudumisha huu muungano ajili ya maedeleo na usalama wa taifa letu.

Utakapo vunjika faida itakuwa kwa mabeberu na hasara itakuwa kwa watanzania.

Ni juu ya viongozi kukubaliana na wananchi juu ya aina ya muungano utakao tuwezesha kukabiliana na mafisadi.

TAMBUA muungano wa Tanzania ni tofauti na EU maana wa tanzania ni kama nchi moja lakin wa ulaya ni kama EAC. pia muungano haupaswi kuundwa na viongozi bali uundwe na hisia za ndani za wananchi wa nchi husika.
 
Zanzibar wana bendera yao, wimbo wao wa taifa, katiba yao, rais wao, mahakama yao(ingawa ni kinyume na Katiba ya JMT), jeshi lao (kmkm na jeshi la kujenga uchumi), ZFA. Muungano wa jinsi hii ni for conveience only. Tusipobadili aina ya muungano uliopo tutajikuta tukiimba wimbo wa muungano wakati tukiwa na nchi ya Zanzibar na Serikali ya muungano isiyo na muungano.
Tanzania Bara ni lazima tuwe na serikali yetu. Hivi sasa tunaendelea kui-finance serikali ya Zanzibar ili tuendelee kuita muungano ambao Wazanzibari hawautambui. Kwa wale wanaofuatilia mijadala ya Bunge liitwalo la muungano watakubaliana nami. Kuendelea kuwa na muungano wa namna hii ni sawa na kuanza kusafiri juu ya maji kwa miguu. Siupendi kabisa muungano wa namna hii. Tanganyika lazima iwepo.

Hali ya kisiasa na kijamii imebadilika sana na ni tofauti kabisa ilivyokuwa mwaka 1964. Kuendelea kuwa na muungano ulivyokuwa 1964 ni kukalia bomu.
 
Ukweli mtupu..Nakuomba Prof.Baregu na wana tume wengine waona mbali jitoeni hiyo kamati ni unafiki mtupu.Hamko huru kupokea kile wa TZ wanataka. Mtakuwa remote controlled. Mnakuja kukusanya maoni wanayotaka magamba tu.
 
Rais Alichosema wakati akiipisha wajumbe wa tume:

Alisema kuwa Watanzania wanataka Katiba ambayo itakuwa na maslahi kwa wananchi wote na kwamba huo sio mchakato wa kuvunja Muungano ama kutokuwepo kwa Muungano.
"Huu sio mchakato wa kuvunja kuwepo kwa muungano au kutokuwepo kwa muungano ieleweke huu ni mchakato wa kupata maoni ya katiba mpya ya nchi ambayo itajali mustakabali wa nchi na watu wake," alisema Rais na kuongeza kuwa watu wanaweza kujadili jinsi ya kuboresha muungano.

Sheria ya Mabadiliko ya katiba inazungumza nini kuhusu swala la Muungano:
Ibara ya 9, ambayo yote inaeleza majukumu ya Tume lakini Ibara hiyo ya 9 Fasili ya (2) fasili ndogo ya (a) inasisitiza

(2) In the implementation of the provisions of subsection (1), the
Commission shall adhere to national values and ethos and shall, in that
respect safeguard and promote the following matters:
a) the existence of the United Republic;
 
Katika kipindi cha majadiliano leo saa kumi na mbili jioni kilichorushwa na Sauti ya Ujerumani kikishirikisha jopo la watu wanne Jenerali Ulimwengu amekuwa muwazi na kusema kuwa huwezi kujadili katiba mpya bila kujadili muungano kwa uwazi. mwandishi Salim kutoka Zanzibar kasema haiwezekani mtu atoe amri kuwa lolote mnaweza kujadili isipokuwa uwepo wa muungano. Kwa maoni ya wana jopo mjadala wa kitaifa ufanyike na watu waulizwe kama wanautaka muungano au la na kama wanautaka uwe wa muundo gani.
Na wana JF mnasemaje?
Sawasawa kabisa. Akili timamu
 
Muungano umo kwenye katiba hivyo ni muhimu kujadili katiba in its totallity. Kama hujadili muungano ina maana itakuwa ni kuweka viraka kwenye katiba kwa kuwa Ibara inayohusu muingano haitaguswa.
 
Mtoa mada angalia matumizi ya jina huyo ni Jenerali Ulimwengu na siyo General Ulimwengu.

Mawazo ya watanzania wote ni kupata katiba mpya na si viraka kwenye katiba. Kwa kutokujadili muungano ambao umo ndani ya katiba ina maana tutaishia kuwa na katiba ambayo si mpya bali ni ile ya zamani ambayo itarekebishwa.
 
Katika kipindi cha majadiliano leo saa kumi na mbili jioni kilichorushwa na Sauti ya Ujerumani kikishirikisha jopo la watu wanne Jenerali Ulimwengu amekuwa muwazi na kusema kuwa huwezi kujadili katiba mpya bila kujadili muungano kwa uwazi. mwandishi Salim kutoka Zanzibar kasema haiwezekani mtu atoe amri kuwa lolote mnaweza kujadili isipokuwa uwepo wa muungano. Kwa maoni ya wana jopo mjadala wa kitaifa ufanyike na watu waulizwe kama wanautaka muungano au la na kama wanautaka uwe wa muundo gani.
Na wana JF mnasemaje?
Mbona huu ndio ukweli wenyewe. Huwezi kuacha kujadili huu muungano kama tutatengeneza katiba mpya kwa kuwa umezungumzwa kwenye katiba hii ya sasa tunayoitupa. Ila muungano hauwezi kuongelewa iwapo tutakuwa na lengo la kuweka viraka tu na kuendelea kubaki nayo hii ya sasa.
 
Muungano ufe alafu ufufuke katika hali inayoeleweka isije kuwa mgogoro kwa vizazi vijavyo! Walio ushuhudia hawatakuwepo na wajao watataka kuona maandishi - hati ya makubaliano.
 
Mi nazani wakati wa kutoa maoni ndo mahala sahihi kwa kujadili muungano kwamba uweje ( kama twautaka ) au kuuvunja kama hatuutaki
 
Back
Top Bottom