Jeneral Ulimwengu: Huu ni utawala wa milipuko! Wafanyakazi wanafanya kazi kwa uoga

Nilichojifunza kwa jpm ni kwamba kuomba kuongoza nchi kunahitaji maandalizi ya muda mrefu,yaani unaingia tu tayari unakuwa ulishajipanga hivyo unaelewa kuwa unaanzia wapi na unaishia wapi.Sasa kwa huyu raisi wangu inaonekana alikuwa hana maandalizi, anaonekana alikuwa hajajipanga hali iliyosababisha mikakati yake mingi kiuongozi kuwa ya dharula ndharula,matamko- tamko na tumbua- tumbua. Mbinu hizi zote ndio zimetufikisha hapa kwenye maisha magumu,benk kufilisika,viwanda kupunguza wafanyakazi,biashara kufungwa,mizigo bandarini kupungua,watalii kupungua,maroli kusitisha safari,ajira kusitishwa,stahiki za wafanyakazi za kwa mujibu wa sheria kuzuiwa nk
 
biashara zaidi ya 2000 zimefungwa dooooh
we unasema 2000 nchi nzima?
labda useme m2
Akiwa katika mahojiano na kituo cha radio cha DW leo 31.12.2016 Jenerali Ulimwengu ameeleza ni kwa jinsi gani utawala huu ulivyo wa milipuko, kwamba inatokea matamko yanatolewa asubuhi kisha jioni yanabadilishwa.

Amebainisha wazi pia wafanyakazi wengi wa umma wanafanya kazi kwa uoga bila kujiamini ili wawafurahishe watawala kwa kuogopa kutumbuliwa.

Ameeleza pia jinsi ambavyo JPM alivyokiri hapo awali kuwa ameshindwa kwani alitamani muhula wa uongozi upunguzwe lakini baadaye akabatilisha na kusema ataaendelea.

Hii ni dalili tosha kwamba kwa yanayotokea kwa sasa hayataleta ufanisi mkubwa kama ilivyokuwa ikitarajiwa na wengi na kwamba itachukua muda sana kuweza kupata mustakabali wa hali iliyopo kwa sasa!
 
Mkuu viwanda sio uyoga useme Kesho uamke tu uvikute, na hakuna Rais duniani anayejenga viwanda peke yake hivyo kumlaumu Magu unakua unamuonea tu, kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na kushawishi potential investors waje kuwekeza, hilo linafanyika. Mkuu kaamua kufanya viwanda kama moja ya vipaumbele vyake nadhani atafanikisha tu with time.

Vile vile katika maelezo yako umeshindwa kuonesha uhusiano was moja kwa moja baina ya maamuzi ya Magu na kupanda kwa bei ya umeme kama unavyodai!
Una roho ngumu
 
Bila kusahau matamko yasiyotekelezeka kama lile la uhakiki wa mwezi mmoja au miwili na haitazidi miwili leo mwezi wa sita hakuna jipya serikalini.
Na Jana nmeona salary sleep ya November ya mfanyakazi aliefariki miaka minne iliyopita...zoezi Ni gumu Sana .linahitaji kuelimisha watu na kujenga urafiki na wananchi kwanza na sio kua mbabe kihivyo.
 
Mkuu viwanda sio uyoga useme Kesho uamke tu uvikute, na hakuna Rais duniani anayejenga viwanda peke yake hivyo kumlaumu Magu unakua unamuonea tu, kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na kushawishi potential investors waje kuwekeza, hilo linafanyika. Mkuu kaamua kufanya viwanda kama moja ya vipaumbele vyake nadhani atafanikisha tu with time.

Vile vile katika maelezo yako umeshindwa kuonesha uhusiano was moja kwa moja baina ya maamuzi ya Magu na kupanda kwa bei ya umeme kama unavyodai!
Khahahaaaa hovyo!
 
Akiwa katika mahojiano na kituo cha radio cha DW leo 31.12.2016 Jenerali Ulimwengu ameeleza ni kwa jinsi gani utawala huu ulivyo wa milipuko, kwamba inatokea matamko yanatolewa asubuhi kisha jioni yanabadilishwa.

Amebainisha wazi pia wafanyakazi wengi wa umma wanafanya kazi kwa uoga bila kujiamini ili wawafurahishe watawala kwa kuogopa kutumbuliwa.

Ameeleza pia jinsi ambavyo JPM alivyokiri hapo awali kuwa ameshindwa kwani alitamani muhula wa uongozi upunguzwe lakini baadaye akabatilisha na kusema ataaendelea.

Hii ni dalili tosha kwamba kwa yanayotokea kwa sasa hayataleta ufanisi mkubwa kama ilivyokuwa ikitarajiwa na wengi na kwamba itachukua muda sana kuweza kupata mustakabali wa hali iliyopo kwa sasa!
Huyu Jeneral Ulimwengu ana mchango gani kwa taifa hili??

Kweli haoni Elimu bure, kufufuka kwa Atcl??

Vipinzani vya Tanzania vimejaa unafiki na upumbavu mtupu
 
Huyu Jeneral Ulimwengu ana mchango gani kwa taifa hili??

Kweli haoni Elimu bure, kufufuka kwa Atcl??

Vipinzani vya Tanzania vimejaa unafiki na upumbavu mtupu
Wewe mchango wako katika hili taifa ni upi?
 
Nimeusikiliza "Utumbo"wote alioongea Ulimwengu, ndipo nilipogundua kuwa watu wengine huwa hawana hoja na ni pointless, amedai kuwa tangu miaka ya nyuma watawala wa Tanzania wamekuwa na uongozi wa milipuko, alianzia kwa Mwinyi, Mkapa,Kikwete na hatmaye Magufuli, ametoa malalamiko yake bila kubainisha milipuko anayoiongelea ni ipi "specificaly",hakutoa mifano yeyote toka kwa Mwinyi na hadi Magufuli. Hivyo Ulimwengu ni mfa maji na mtu ambaye aliwahi kupewa uongozi akashindwa vibaya sana, tena nadhani ulikuwa U-Dc tu kama sikosei,lakini hakuna cha maana alichofanya kwenye uongozi wake. Sasa iweje leo awe bingwa ktk kukosoa wenzake? Tena viongozi wa kitaifa? Ulimwengu kwanza ni Mkimbizi na alisamehewa tu. Hata hivyo hatushangai kwani watu wa asili yake kutoka kule alikotoka, wanatabia za kujiona wao ni bora sana tena siku zote wao ndiyo "the best", hata yule kiongozi wa kule amelazimika kubadiri katiba ili atawale maisha kwa kutowaamini wengine. Ulimwengu hafai na hatafaa kamwe.
 
Sheria za kazi zilikuwepo wafanyakazi wakazipuza, mtu anaingia kazini saa mbili saa tatu anaelekea kwenye shuguli zake binafsi. Kama mfanyakazi hato jirudi, nguvu ya ziada itatumika kumrudisha kwenye mstari.
 
Back
Top Bottom