Je yupo wa kusaidia Tanzania kuondokana na bidha feki?

panya john

New Member
May 6, 2009
1
0
Bidha feki zinauzwa kila duka Tanzania. Ni imani hakuna Mtanzania ambaye hajalizwa. Mimi leo hii nimeenda dukani kununua betri za kamera. Najua zile za kintazania yaani national hazina nguvu ya kuendesha kamera yangu. Mara zote nanunua duracel nikijua ni imara. Kumbe sikujua kuwa tayari wajanja mafisadi wameshaingia kwenye duracel. Jamani ni hatari. nimenunua betri 2 kwa Tsh. 4000. Hiyo ndio bei ya huku mikoani. Nilichopewa ni duracel feki tena wamefunga kwenye mifuko ya plastic. zamani duracel zilikuwa kwenye mifuko ya karatasi.

mimi nalia na duracel, ila ukweli asilimia 80 ya bidha zilizopo madukani zipo chini ya kiwango cha ubora. Je kikwete uko wapi. Tusaidie wananchi wako. Tunaibiwa sisi. Weka basi wakaguzi wa bidha feki. Wachina watatuua. wanatuibia tu. Hao uliowapa dhamana - namaanisha tbs wamelala usingizi. kwanini usifute hili shirika. Linamaliza pesa ya kodi ya wantazania tu.

Chonde chonde tusaidie wanao. Tunaibiwa humu humu nchini kwetu. mzee tunataka vitendo.


John Panya.
 
mimi nalia na duracel...
Sio duracell tu, wimbi la bidhaa bandia liko hata kwenye madawa. Wahindi wanabadilisha 'lable za expiry dates' za madawa kwenye maghala yao na kisha kuyarudisha tena madukani. Polisi wanalijua sana hilo lakini wako kimya kwa kuwa wako kwenye payrolls za wadosi hawa, twafa kwa madudu mengi jamani...
 
Back
Top Bottom