Je wewe ndivyo unavyoishi hivi?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Kila mtu ni mbaya kwako, kila mtu anakuchukia, wewe tu, kila mtu hakutendei haki, kila mtu ana kasoro?
Je wewe ndivyo unavyoishi hivi? Kama jibu ni ndiyo au kama una mtu wako wa karibu ambaye anaishi katika mtindo huu wa maisha, unapaswa kujua kwamba, una mtu ambaye ana matatizo makubwa.

Kwa nini?

Ni kwa sababu haiwezekani kila mtu akawa kama mwingine, yaani akikuchukia huyu na yule ni lazima atakuchukia, ni lazima hatakutendea haki na mengine ya aina hiyo. Kwa nini sasa wote wawe na tabia za aina moja, yaani wafikie kukuchukia?

Kwa kuwa watu hawafanani kitabia, kimwenendo na kimtazamo, ni wazi ukiona wote wanakuchukia wewe, tatizo haliko kwao, kwa sababu hawawezi wote kuwa na mkabala wa aina moja. Ina maana kwamba wewe ndiye ambaye hujipendi na kutojipenda kwako kunaonekana kwa watu hao.

Tunaposhindwa kujipenda, hasira dhidi yetu huwa tunazitolea kwa watu waliotuzunguka. Kwa hiyo kama unahisi kwamba watu wanakuchukia, jitahidi kujiuliza kuhusu jambo hilo. Ni wazi haliwezi kuwa jambo la kweli hata kidogo. Kama ni
kuchukiwa, hivi inawezekana ukachukiwa na kila mtu kweli?
 
ni kweli mkuu ila unaweza ukawa wewe ni kero kwa watu hivyo lazima watu wakuchukie ... ila wengine huchukiwa kulingana na utendaji wao kama walimu wa hesabu huchukiwa na wanafunzi wale wanaolichukia somo
 
Back
Top Bottom