Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Mighahawa kama hii huzua mangung'uniko kwa wahudumu kuwa na ubaguzi wa rangi
Utafiti nilioufanya hivi karibuni katika mighahawa inayoitwa ya kitalii hapa nchini nimebaini kwamba wateja wenye asili ya afrika hususan wenye rangi nyeusi hupata huduma duni ukilinganisha na wazungu.
Utafiti huu niliufanya katika mighahawa ya mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar. Nililenga mikoa hiyo kwa sababu ni miji ambayo hutembelewa na watalii kwa wingi na ina mighahawa mingi ya kitalii ukilinganisha na mikoa mingine.
Utafiti wangu ulijikita zaidi kwenye maeneo yafuatayo:
1. Mapokezi
2. Kukalishwa kwenye meza
3. huduma ya vinywaji
4. huduma ya vyakula baada ya kuagiza
5. Huduma ya kuletewa Ankara (Bill)
Nilikuja kugundua kwamba wakati wazungu wakifika kwenye mghahawa hupokelewa kwa bashasha na kuelekezwa kwenye meza na kukalishwa lakini wateja wenye ngozi nyeusi wanaweza kufika hapo kwenye mghahawa na wakabaki wakishangaa, hakuna mtu wa kuwapokea wala kuwealekeza kwenye meza. Ni mpaka pale watakapoulizia iwapo wanaweza kupatiwa meza.
Kwa upande wa huduma ya vinywaji vile vile wazungu watapelekewa menu na kuchukuliwa oda ya vinywaji wakati wanasoma menu, lakini wateja weusi kila kitu mpaka wafanye kuomba. Na hata baaada ya kuagiza wazungu wanaweza kuletewa oda yao mapema zaidi ukilinganisha na wale wateja weusi wenye asili ya Afrika. Kwenye swala la Ankara (Bill) nalo ni kizungumkuti, mzungu ataletewa bill yake mapema sana pale atakapoomba lakini mteja mwenye rangi nyeusi itamchukua muda kuletewa bill yake.
Nilijaribu kuongea na baadhi ya wahudumu (waiters) wa mighahawa hiyo lakini wengi walipinga kwamba hawahudumii wateja kwa kuangalia rangi lakini baadhi yao walikiri udhaifu huo wakisukuma lawama kwa baadhi ya wahudumu wenzao ambao hukimbilia wazungu kwa sababu wao baada ya huduma huacha bahashish (Tips) tofauti na wateja wenye rangi nyeusi wenye asili ya Afrika ambao hawana utamaduni wa kuacha bahashsh (Tips). Hata hivyo walikiri kwamba wapo wateja weusi wenye asili ya Afrika ambao wanaacha bahashish (Tips) baada ya huduma.
Lakini pia walidai kwamba wateja wenye rangi nyeusi ni wasumbufu na pia wana kitu kile kinachoitwa inferiority complex, kwamba wakifika kwenye mghahawa wanajiona kama wao wanachukuliwa na wahudumu kama wateja wa daraja la pili na hawathaminiwi na hapo ndipo utata unapoanzia kwani watakosoa kila kitu tofauti na wazungu ambao hata wakicheleweshewa oda zao huuliza kwa upole.
Mhudumu mmoja mbaye alijitambulisha kwa jina la Dullah anayefanya kazi katika mghahawa mmoja pale Sea Cliff alisema kwamba, kingine kinachosababisha kuzua manunguniko ni aina ya vyakula vinavyoagizwa na wateja .
kuna aina ya vyakula ambavyo havichukui muda mrefu kuandaliwa na kama mzungu kaagiza aina hiyo ya chakula ni wazi atalelewa haraka ukilinganisha na mteja mwingine aliyeagiza chakula kinachohitaji matayarisho maalum. Kwa mtu anayeelewa mapishi kama wenzetu wazungu hawezi kulaumu lakini kama ni mbongo lazima atalaumu . Alisema Dulla.
Hata hivyo nilipoongea na wateja mbalimbali niliokutana nao katika mighahawa hiyo walikiri kwamba kuna aina ya ubaguzi wa rangi katika mighahawa ya kitalii hapa nchini na sio mighahawa tu hata katika maduka makubwa kama supermarkets.