Kuumiza wateja wako siyo suluhisho la mgogoro wako na mwajiri

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,217
2,821
Niende moja kwa moja tu kwenye hoja yangu... Katika vitu sipendi kufumbia macho ni kuona mtu anaonewa (anaumizwa) bila kosa lolote.

Kuna wafanyakazi wengine bwana eti akiwa na mgogoro basi anatafuta suluhisho kupitia walewale anaowahudumia. Sasa bora iwe unawatumia kwa njia ambayo haiwaumizi lakini unakuta mtu anawaumiza kabisa

Kuna wahudumu wa afya aisee! Eti mtu ¹anaenda kazini saa anayojisikia yeye, wamama wa watu wamejazana kumsubiri halafu wala hajali. Wagonjwa wa dharura ndo kabisa hawana bahati yaani hata uende unavuja damu aisee ²unajibiwa dry kabisa "huu siyo muda wa kazi!"

Mgonjwa akienda Jumapili hata awe katika hali gani huwezi amini ³anarudishwa aisee eti siyo siku ya kazi. Jumamosi kadhalika huhudumiwi. Wengine hata hizo siku za kazi (kama wanavyoziita wenyewe wahudumu) ⁴wanahudumiwa lakini kwa kutanguliziwa kugombezwa sana na kusemwa vibaya;

mfano umeenda Jumanne unakaripiwa eti umechelewa wapi siku zote wakati huohuo ukienda kwa hali iliyokupata kwa siku hiyo hiyo au kwa kuona dalili fulani bado tena unakejeliwa kwamba muoga utasikia, "siyo kila kitu ni cha kukileta hapa vingine unameza panado tu unavumilia" (hapo sasa mtu anashindwa kujua kipi bora kuwahisha kuripoti ugonjwa au kuchelewa)

⁵Mwanamama akipeleka mtoto kliniki halafu mtoto huyo ana homa basi mtoto atahudumiwa kitu kimoja tu, sub-haanallah! Yaani hii ndo inanipaga alama ulizo sana

Ni hivi yaani akienda upande wa kliniki kisha akahamia upande wa matibabu anaambiwa rudi katafute siku ya kumleta kwenye matibabu vivyo hivyo akisema aanzie kwenye matibabu kisha ahamie kwenye kliniki basi mtoto huyo hatopimwa bali ataambiwa arudi siku nyingine kwa ajili ya kliniki (atarushwa tarehe-ataandikiwa tarehe nyingine)

Kuwatumia wapokea huduma kupata suluhu ya tatizo lako wewe mfanyakazi bila kuwadhuru au kuwaumiza yawezekana wengine hawanielewi ngoja nitoe mfano, mwalimu anaweza kuorganize na watoto au jamii wakafanya hata maandamano uchwara kudai jambo fulani, mhudumu wa afya aliyepelekwa sehemu asiyoipenda kwa mfano anaweza kuwachochea watu wa sehemu aliyotoka wakadai kwa nguvu zote mfanyakazi wao, matukio ni mengi mifano ni karibu kila sekta

Nimemfikishia mhusika na wenzangu wamefikisha pia, huku nimekuja tu kuweka kumbukumbu na kuwafikishia na wengine wenye tabia hizo. Badilika! Njia unayotumia inaweza kukutokea puani!
 
MmmmMm
 
Back
Top Bottom