Je, Watanzania mlio nje ni vibarua na wabeba maboksi?

Nikisoma hizi comments napata picha kuwa inaonekana kuna beef kubwa kati ya wabongo waliobahatika kutoka na kuendelea na shughuli zao ughaibuni V/S waliojaribu kuondoka na kugonga ukuta, walionyimwa visa, na wanaotamani kuondoka lakini inawawia vigumu, ama wanaoendelea kupigika bongo na waya mkali.


ongera sana wewe umenena, ila umesahau kidogo au umetumia neno la kistaarabu. Hawa hawana kingine zaii ya wivu na husda.
 
Je wanaotuma vitu kama magari makontena ya vifaa vya ujenzi, vifaa vya ujenzi wa barabara , vifaa vya mahospitalini, magari ya hospitalini , helicoter? inakuaje hamuoni kuwa wote wanaonunua vitu hivyo na kuvituma nyumbani wametumia dollar zao au mnafikiri wamepewa bure, hamuoni kuwa wanapeleka ajira pia kwa ndugu zenu na kupata ridhiki kila siku. maana mfano ukipeleka dollar 1000 kwa baba yako atakula peke yake lbda na mama yako au wadogo zako lakini ukipeleka kitu kinchozalisha watu wengi watapata ajiri mfano ukipeleka basi hapo utakuwa uimesaidia dereva , condacta , na utingo. sasa naona ni bora wasitume pesa kwa weatern union watume vitu ambavyo vina generate income kwa watu wengi. Hivyo basi wewe mtoa hoja jua kuwa hata wabeba box wana pesa na wanafanya mambo mengi fuatilia utayapata.
 
Fareed,

Unasema "Pesa hizi zinatumika kununua nyumba, kulipa ada za shule, matibabu, nk"

Hivi wewe kuna Ndugu au Jamaa yeyote aliepo nje ya Tanzania anaweza kukuamini kukupa pesa umnunulie nyumba,au ukalipie ada ya shule?Ni wangapi?

Tatizo kubwa la watanzania popote pale tulipo ni uaminifu....
Nimeshasikia watu wametuma pesa kujengewa nyumba hawajengewi,Ada ya shule hailipwi ...na wengine wanajidai wanauguza kumbe kamba tu..wengine wanachangisha michango ya harusi na harusi zenyewe Hazifanyi....

Kabla ya kuanza kulalamikia watanzania walio nje..embu tafuta kwanza Mzizi wa tatizo ni nini..... OK?

Concord
 
Ukiwa nje siku hizi huasaidii ndugu zako, unasaidia mafisadi. Ni bora uisaidie nchi inayokupa hata kibarua cha kubeba boksi, hapa nyumbani wapi unaweza kwenda kubeba boksi? Serikali inawakatisha tamaa, kama ingekuwa na mpango mzuri watanzania pia wanaweza kufanya vizuri.

Mkuu hapo umesema, ukituma dola Tz zinaingia BoT halafu zinatafutiwa mpango hewa kama vile Dowans and the like then mafisadi wanazitoa na kuzipeleka offshore. Kitu Kingine Tanzania tunachoharibu ni kodi, yaani hata ukiingiza box la pipi kama zawadi unapigiwa hesabu za kulipa kodi. Mtu anachuma kimtaji chake Ulaya/Marekani akifika bongo na assets zake anaanza kusumbuliwa utafikiri Serikali ndiyo imempatia hivyo vitu. Kitu kingine ni kwamba gharama za kutuma assets bongo ni kubwa sana kwa ajili ya insurance yaani vitu au hela hazina uhakika wa kumfikia mlengwa.

Kwa nini mtu asisubiri jirani yake akiwa anasafiri anampatia bahasha yenye cash kwa nduguze?
 
Swali zito sana hili!!

Labda Mhe Nyalandu anaweza akatusaidi ufafanuzi kwani wao na akina Lau Masha ndio tumepata kuwasikia hivi karibuni kwamba huko Ma-Mtoni ni kama nyumbani kwao tu.
 
Watanzania wanatumia money on "envelop system" sababu kutuma kwa njia zinazofahamika kama Western union, Money Gram kwetu bongo bado tuko gizani. Ukisikia mshikaji anakwenda bongo basi unampatia dollar kadhaa akawape nduguzo kwenye bahasha. Envelop system huwezi ingiza kwenye hizo takwimu nina amini watanzania wanasaidia zaidi ya wakenya na waganda. Kuna jamaa fulani waliacha kufanya kazi kabisa wakitegemea mafuba toka kwa kaka yao aliyekuwa Greece.


Hilo ni kweli kabisa Mkuu, pia idadi ya Watanzania walio nje ukilinganisha na majirani zetu wa Kenya na Uganda ni ndogo sana. Na pia inawezekana kabisa uwekaji wa takwimu hata za wale wanaotumia Western Union na mabenk mengine una walakini kiasi ambacho BoT hawana takwimu ambazo ziko sahihi.
 
Ni hoja nzuri lakini nakushauri ungeuliza balozi za Tanzania katika hizo nchi ambazo ndiko kuna wabongo wengi. Labda wataweza kukupatia data zenye usahihi.
Mfano;Cheki na ubalozi wa bongo palee DC, sababu tulipokuwa tunabadilisha passport mwaka 2006 walichukua personal info zetu wabongo wote tuishio US.Naamini watakupa picha halisi ni watanzania wangapi wanaishi nje ya nchi, asilimia ngapi tunapiga boksi na wangapi wanapiga white collar schedule.
Halafu you be the judge.Halafu kama bado unakerwa na hizo data then cheki na balozi za Kenya, uganda au hata Nigeria uliza idadi ya watu wao wanaoishi nje, na details zao nyingine halafu linganisha usahihi wa hizo takwimu.


Mzee si ungetoa kabisa hizo details kama unazo kuliko kutoa homework ambayo hamna mtu ataifanyia kazi.
 
Hizi takwimu lazima zina walakin, haiwezekani Waganda warudisha nyumbani kwao $850 million halafu Tanzania iwe $17m tu. Yaani pesa wanazorudisha Waganda kwao ni mara 50 ya pesa ambazo Watanzania walio nje wanazileta Bongo.

Basi onesha walakini ulipolalia, kwani kiasi cha pesa kwa kawaida hakiendani na idadi ya watu - mtu mmoja anaweza kutoa shilingi 1000 na wengine watano wakatoa 100 kila mmoja na kupata 500; je scenario hii utaikataa?. Pia umekwisha ambiwa limitation kuwa BoT haina mpango wa kuliangalia hilo!
 
Kuna mtu aliwahi kusema kuwa wengi wa Watanzania waishio US hasa wanawake kazi yao ni kuosha nyuchi za wamarekani!!! Sasa hawa wata-remit nini?
 
Hahaahaa!

I love your laughter: I once visited London and I took a very early morning walk and found only people of African origin (I belive there is no black or white people in this world) were picking gabbage from roads. In the hotel I stayed located at the heart of London most of dish washers, waiters/ waitresses and room cleaners were of African origin.

I am tempted to generalise that it is true that most of Tanzanians who live abroad are regarded as cheap labour and do unskilled jobs even though they highly educated!!!!!!!!!
 
Hatimaye Dual Citizenship mwakani,habari njema kwa adventure loving Tanzanians, Set to sail on my way ,my head is turning around ,i had to leave a little girl in Manzense!
 
Ni kweli wenzetu nje hawachagui kazi kama sisi kwani kupata kazi ya maana nje ni ndoto. Hii sio kwa Waganda na Wakenya tu bali hata Watanzania pia. Tuje kwenye hoja ya msingi mimi nadhani swala kubwa hapa ni utunzaji wa takwimu kwani kama kawaida sidhani kama BOT inatilia swala hili mkazo sana. Pia nakubaliana na hoja iliyotolewa na mmoja wa wachangiaji humu kuwa watanzania wanaaminiana sasa na hupenda kutumia zaidi njia za kutumana na kupeana mabulungutu ya dola hivyo ni vigumu fedha hizi kuingia kwenye record za BOT.
 
Hizi takwimu lazima zina walakin, haiwezekani Waganda warudisha nyumbani kwao $850 million halafu Tanzania iwe $17m tu. Yaani pesa wanazorudisha Waganda kwao ni mara 50 ya pesa ambazo Watanzania walio nje wanazileta Bongo.
Kaka hizi takwimu nizaukweli kabisa mimi kaka yangu tangu aende marekani miaka ya 80, mpaka leo hajawahi kutuma hata dolla1.
 


Watanzania wanaoishi nje wanapeleka wapi pesa zao


WaKenya ambao waaishi huku Tanzania na kwingineko duniani, mwaka uliopita walirudisha nyumbani kwao zaidi ya dola za Marekani $640 million. Wauganda nao walirudisha kwao $850 million mwaka jana. Pesa hizi zinatumika kununua nyumba, kulipa ada za shule, matibabu, nk na zinachangia sana kwenye pato la kigeni la nchi hizi jirani zetu.

Huko Kenya, pesa zinazotumwa na raia walio nje ndiyo chanzo kikubwa cha nne cha mapato ya kigeni baada ya mauzo ya nje ya chai, mauwa na utalii.

Benki Kuu ya Tanzania wala haijishuhulishi na pesa zinazotumwa nje na Watanzania na wala haitoi takwimu zake. Kwa mujibu wa makadirio ya Benki ya Dunia, Watanzania wanaoishi nje (diaspora) wengi wenu mkiwa wachangaji wakubwa wa mada humu JF, mwaka jana walitarajiwa kurudisha nchini kwao $17 milion tu?!

Hii ina maana mbili. Watanzania walio nje ni wachache sana au ni wengi lakini siyo skilled workers wanaoweza kupata kipato kizuri kutokana na taaluma zao. Pengine wengi wenu mnafanya kazi za kibarua, hourly shifts kubeba maboksi and flipping burgers MacDonalds na KFC hivyo hamna pesa za kutuma kwenu nyumbani kwa ajili ya maendeleo na kusaidia ndugu zenu. Si mrudi basi Bongo?

Au maana nyingine ni kuwa pesa hizo zinatumwa kwa wingi lakini Benki Kuu haifanyi utaratibu wowote wa kuzirekodi. Au zinatumwa kienyeji kwa kufichwa kwenye barua na mizigo mingine. Ama Watanzania mnaendekeza anasa tu huko majuu wakati Wakenya na Waganda wanajenga nchi zao? Nawaza sipati jibu.

Kazi za ubebaji wa maboksi siku hizi zimepungua sana Ulaya, kutokana na maendeleo ya kisayansi na sheria kali za ILO za usalama kazini. Hakuna mtu anayeruhusiwa kunyanyua mzigo uliozidi kilo 15.

Hizi takwimu mimi zimenistua sana. Kitu nachodhani hapa ni kwamba waTZ walioenda nje, wengi wao ni watoto wa wakubwa. Actualy wengi wao wanatumiwa pesa na wazazi wao walio bongo ili wa-survive huko majuu. Kuna mahali nilisoma wakenya wanalaumu sana waTZ walio nje jinsi wasivyojishughulisha na utafutaji wa pesa huko majuu.

Kinyume na hii hali, Wakenya na Waganda wa kawaida wanamuamko wakuwafanya wafunge safari wenyewe kwenda nchi za ughaibuni kutafuta maisha. Hawa wa kawaida ndiyo wanaotuma pesa nyumbani.
 
Katika hili, kuna ukweli unaotokana na mambo mawili makubwa:

(1) Ni kweli, wakenya wanatuma sana kuliko watanzania, kwa sababu kuna wakenya wengi sana huko nchi za nje kuliko watanzania (zaidi ya mara nne). Unaona hata hapo Tanzania kuna wakenya wengi sana walioshika kazi nzuri wakati hakuna watanzania wengi namna hiyo huko Kenya. Hata hivyo hivyo tofauti hiyo ya pesa iliyowekwa hapo nadhani ni kubwa sana kupita kiasi.

Vile vile wakenya wako mbele sana katika kufanya frauds za hela nyingi nyingi mno kama:

A Kenyan National Charged on Tax Fraud

A Kenyan Arrested on Tax Fraud

Kenya Man sentenced for scamming



(2) BoT haina data za kutosha kuhusu pesa zinazotumwa kwa njia za westernuion na Moneygram; wao wana rekodi za wire tu. Watanzania wengi wanatumia njia za Moneygram na Westernunion kuliko njia za wire
 
Ni kweli wenzetu nje hawachagui kazi kama sisi kwani kupata kazi ya maana nje ni ndoto. Hii sio kwa Waganda na Wakenya tu bali hata Watanzania pia. Tuje kwenye hoja ya msingi mimi nadhani swala kubwa hapa ni utunzaji wa takwimu kwani kama kawaida sidhani kama BOT inatilia swala hili mkazo sana. Pia nakubaliana na hoja iliyotolewa na mmoja wa wachangiaji humu kuwa watanzania wanaaminiana sasa na hupenda kutumia zaidi njia za kutumana na kupeana mabulungutu ya dola hivyo ni vigumu fedha hizi kuingia kwenye record za BOT.
Unafahamu tafsiri ya hilo neno mabulungutu ya dollar? unaijuwa dollar wewe?
 
Back
Top Bottom