Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,224
- 5,386
Leo hii Dar es salaam ina manispaa 5 ikiwa na watu milioni 5 lakini matazamio nikuwa na manispaa nyingine pale Mbagala hii yote ni katika kurahisisha na kuimarisha shughuli za kiutawala, huduma za kijamii na maendeleo ya watu kiujumla katika miji yetu.
Kwa muda sasa jiji la Mwanza limekuwa na halmashauri mbili tu, ambazo ni NYAMAGANA yenye hadhi ya jiji na nyingine ILEMELA yenye hadhi ya Manispaa.
Sasa kulingana na takwimu za hivi karibuni kuhusu idadi ya watu na makazi yao kunaipa nafasi gani Mwanza katika kinyang'anyiro cha kupewa manispaa nyingine mpya?
Mwanza mkoa idadi ya watu=3,699,872
Mwanza city (Nyamagana)= 594,834
Ilemela= 509,687
Jumla= Watu 1,104,521
Idadi ya makazi: Mwanza city=153,226 na ilemela=127,507
Jumla= Nyumba 280,733.
Jiji zima lina jumla ya kata 37 kwa maana ya Mwanza jiji 18 na Ilemela 19 na Kata zinazoongoza kwa idadi ya watu ndani ya Mwanza jiji ni;
Mahina=57,260
Igoma=57,263
Buhongwa= 67,254 na Kishili=63,054
Na kwa upande wa Ilemela: Buswelu=42,614 na Nyasaka=41,897.
Kwa upande wa kata zingine ambazo zipo katika halmashauri za wilaya za jirani yaani Magu na Misungwi ambazo tutegemee ikitokea kuundwa kwa halmashauri nyingine zitamegwa kuunda manispaa mpya ni pamoja na Kisesa(33,548), Bujora (31,787) Fella (11,346) Kanyelele (17,415) bulemeji(10,943) idetemya (25,095) Ukiriguru (11,903) na usagara (44,220)
Je, kwa mtizamo wako unaona kuna uwezekano hapo wa Mwanza kupewa halmashauri nyingine ya tatu hivi karibuni au mpaka tuipe tena miaka kumi mingine?