Je, upo uwezekano wa jiji la Mwanza kuongezewa manispaa nyingine?

Kwanza stand haikutakiwa nyegez, wangeiweka usagara,, then waweke manispaa ingine kisesa,,
Kumbuka hapo kwa Nyegezi stendi kuna maslahi ya wilaya ya Nyamagana na kule Nyamhongolo pia ni kitega uchumi cha ilemela, lazima halmashauri mpya ianzishe stendi zake japo lazima ziwe ndogo ndogo ili vituo vikuu vibakie hivyo hivyo vilivyopo hili wasiingiliane kimaslahi.
 
Asante kwa uchanganuzi mzuri lakuongezea hapa ni kuwa mimi nafikiri kuwa katika suala la mapato bado kuna uwezekano wa kuweza kutengeneza na kuboresha miundo mbinu na vitega uchumi na mambo yatakuwa mazuri tu.

Mfano kata za usagara, kisesa, kishiri na buhongwa kijiografia zimepakana sana na kwa ujumla wake zina idadi ya wakazi zaidi ya 140k ukiachilia kata zingine nyingi ndogondogo kumbuka kuna mapato ya stendi za kona ya kayenze-kisesa, usagara stendi, nyashishi na Kishiri ambapo kinachoitajika hapo ni ujenzi wa stendi zenye hadhi na mapato yakusanywe serious.

Kuhusu Nyamhongolo tusahau tu ndio backbone nyingine ya uchumi wa Ilemela na wameshawekeza pale stendi mpya hivyo si rahisi wakaiachia labda nyamagana aweze kusurrender Igoma hii itabust mno manispaa mpya kupata eneo dogo la viwanda na biashara kugenerate mapato.

Kuhusu barabara ukiacha mradi wa tactics ule wa Bango-Kishiri to Buhongwa kuna njia ya muhimu ya kipande kidogo cha kishiri-sosoka to Igoma nacho kinahitaji lami hili kuboost uchumi wakati huo njia kadhaa zitakapoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami kurahisisha usafirishaji.

Pia naona kutahitajika ujenzi mpya wa masoko ya kisasa na makubwa katika maeneo machangamfu kibiashara ndani ya Mwanza ya Buhongwa,Kishiri na Igoma. Kwani hata sasa manispaa ya ilemela nayo ipo mbioni kuanza project ya kujenga soko kubwa kama la mjini kati pale kirumba hili kujiongezea mapato.

Pia wakazi hawa watahitajika kuwa na hospitali ya wilaya, mashule, vyuo, idara ya maji, tanesco, mahakama, n.k ambapo kulingana na wakazi wa maeneo haya kuwa wengi kwa idadi na wengi ni wa kipato cha kati itaongeza ukusanyaji mapato kwa kiasi kikubwa.

Huku ndiko mji unapotanukia hivyo ikiwepo mipango mizuri eneo la Kisesa ukishavuka ilipojengwa kuku-poa mbele ya makazi ya wafanyakazi house kuna viwanda vinaporomoshwa sana njia ya kuelekea magu hivyo hii ni advantage kubwa kwa manispaa mpya kuja kuipiku hata ilemela siku za usoni wakimegewa hii sehemu ya up coming industrial area.

Pia uwekezaji katika utalii,michezo, starehe na mahoteli katika maeneo ya Bujora, busisi(kama jiografia inaruhusu) na usagara pale highway itabusti pia uchumi kwa kiasi chake japo inahitajika waibie-ibie wamege sehemu yote ya Igoma(kulia na kushoto)

Ila wakifika malamala Mpaka wao unyooke na upande wa kulia ukitokea mjini, bango,kijiweni, nanenane na watanue miliki wakikaribia kuvuka kwa mangushi kabla ya mpando wa kanyama hapo kuna faida kubwa ya viwanda na shell za kutosha ila sijajua kama ilemela atakubali kuwapatia kirahisi ukitegemea nae anafight kuwa jiji.
Vizuri kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom