Manispaa ya Kahama itakuwa kama Jiji la Mwanza miaka 10-15 ijayo

Dig the EA

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
279
270
Ni ukweli usiopingika miji miwili hii ya Kanda ya Ziwa inakuwa kwa kasi sana Jiji la Mwanza na Manispaa ya Kahama. Lakini kasi ya ukuaji na maendeleo ya Manispaa ya Kahama inaleta projection ya kuwa Kama Jiji la Mwanza baada ya miaka 10 ikichelewa miaka 15..

Mwaka 2002 nilifanikiwa kufika Wilaya ya Kahama, ikiitwa Halmashauri ya wilaya ya Kahama ikiwa na eneo kubwa la utawala lakini mji ukiwa mdogo sana. Eneo la mji ilikuwa ni Nyihogo, Uhindini, Malunga, Mungura(kidogo) , Majengo (padogo) na Nyasubi ndo walikuwa wanaanza kugawa viwanja na kujenga. Mhongolo, Igomelo, Masaki, Phantom, Mbulu nk kote hapakuwepo.

Baadaye mabadiliko na maendeleo yakaanza, mji ukapewa hadhi ya mji mdogo, haikuchukuwa muda ikapandishwa hadhi ya kuwa Halmashauri ya mji, na sasa miaka mitatu sasa ni Halmashauri ya Manispaa.

Mwaka 2003 nilifanikiwa kufika Mwanza. Kiwango cha Maendeleo ya Mwanza ya miaka hiyo ndiyo maendeleo ya Kahama ya leo. Mwaka huo 2003 stand katika mji wa Mwanza ilikuwa mjini katikati--- Sahara. Na Barabara ya lami iliishia Mkuyuni. Mwaka huo huo 2003 mwishoni ikawa inaanzishwa stand ya Nyegezi. Maeneo ya Mkolani na Buhongwa hayakuwa na watu. Wakati stand inaanzishwa pale Nyegezi watu walilalamika na kufoka kwa kupelekwa porini na kwenye mivumbi.

Kwa kasi inayoonekana Manispaa ya Kahama kwa watu kuongezeka kwa kuhamia, kuzaliana, mzunguko wa biashara na pesa, maghorofa kujengwa kama uyoga nk. Kuna uwezekano mkubwa Mwanza ya leo 2023 ikawa Kahama ya 2033 au 2038. Jiji la Mwanza miaka hiyo sijui itakuwa kama miji gani ya leo.

Changamoto iliyopo kwenye miji hii ni kukosa kuzingatiwa (upendeleo) support kubwa kutoka Serikalini. Imagine jiji lile la Mwanza hakuna University hata moja ya serikali. Barabara za njia nne hakuna ukiacha Ile ya Ilemela tu, hakuna hospital kubwa ya rufaa ya serikali (Ile ya Bugando ina mkono na mguu wa Wanatoloki).

Ebu imagine jiji la Mwanza, serikali itupie na kujenga Chuo Kikuu Kama UDOM na hospital nyingine kama Mloganzila au Benjamin Mkapa.... ? Ebu fikiria barabara ya kutoka Usagara hadi Mjini iwe njia nne au sita na Ile ya mjini hadi Kisesa iwe nayo njia nne. ..... Wakati huo huo pata picha zile barabara za Kahama mjini zote zipigwe lami, na serikali ipeleke miradi pale hata Chuo cha VETA tu!!! Hapa nasema kuwa maendeleo makubwa ya jiji la Mwanza na Manispaa ya Kahama mengi ni wananchi/wafanyabiashara. Serikali ikipeleka miradi kadhaa miji hiyo, tutaijua vzr lake zone. Hongerni wana Kahama na Wana Mwanza.
 
Asant ila kiukwel Kahama ina mbingu ya pekee yani unakuja huna hata 100 ila unarud Bilgate

Sent from my SM-G950U using JamiiForums mobile app
 
Wewe jamaa bwana! Kwa hiyo maendeleo ya sehemu yanaletwa na majengo ya taasisi za serikali, na sio huduma zinazopatikana. Yaani hospitali ya Bungando na chuo cha SAUT vikitoweka na serikali akajenga vyake hapo ndio kutakuwa na maendeleo ya haraka?
 
Kahama pia ina kiwango kikubwa sana cha Maambukizi.

Huku mkutafuta hela, chukueni tahadhari.
Ni kweli, lakini maambukizi makubwa yako na yanaongozwa na mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, na Dsm. Lakini hata maeneo mengine Kuna maambukizi. Ni kuwa makini tu !
 
Wewe jamaa bwana! Kwa hiyo maendeleo ya sehemu yanaletwa na majengo ya taasisi za serikali, na sio huduma zinazopatikana. Yaani hospitali ya Bungando na chuo cha SAUT vikitoweka na serikali akajenga vyake hapo ndio kutakuwa na maendeleo ya haraka?
Serikali na miradi yake ikiwemo majengo au taasisi za serikali zina mchango mkubwa sana kwa maendeleo. Taasisi hizo na majengo ya Serikali vinakuja na watu, vinakuja na pesa, vinakuja na mipango. Ukitaka kujua hilo nenda pale Dodoma, uondoe majengo ya Serikali, taasisi za serikali uone kama Dodoma itakuwa vile. Ebu fikiria kile Chuo Kikuu cha UDOM hakipo pale, yale majengo ya Wizara yote hayapo, uone Dodoma itakuwaje!

Na sikumaanisha Bugando hospital na SAUT vitoke; nilimaanisha serikali inapaswa kupeleka na kujenga taasisi zake Mwanza kama ilivyopeleka Dodoma, Dar es salaam, Morogoro na Arusha.
Utakuwa huelewi vzr faida za hizo taasisi !
 
Uzi mzuri sana ila umetupiga kamba sehemu moja tu et lami iliishia mkuyuni 2003!??

Vingine vyote ni kweli
Siyo kamba kaka! Huwezi amini ilikuwa hivo, Mimi nilikuwepo Mwanza miaka hiyo. Na nilisafiri kwenye hiyo barabara!
 
Serikali na miradi yake ikiwemo majengo au taasisi za serikali zina mchango mkubwa sana kwa maendeleo. Taasisi hizo na majengo ya Serikali vinakuja na watu, vinakuja na pesa, vinakuja na mipango. Ukitaka kujua hilo nenda pale Dodoma, uondoe majengo ya Serikali, taasisi za serikali uone kama Dodoma itakuwa vile. Ebu fikiria kile Chuo Kikuu cha UDOM hakipo pale, yale majengo ya Wizara yote hayapo, uone Dodoma itakuwaje!

Na sikumaanisha Bugando hospital na SAUT vitoke; nilimaanisha serikali inapaswa kupeleka na kujenga taasisi zake Mwanza kama ilivyopeleka Dodoma, Dar es salaam, Morogoro na Arusha.
Utakuwa huelewi vzr faida za hizo taasisi !
Naamini kuna taasisi za serikali nyingi tu mwanza mfano jengo kubwa kuliko yote mwanza pale kapripoint nila nssf hata bugando serikali inamkono pale, kuna chuo cha uhasibu kule buswelu naamin ni cha serikali, chuo Cha fisheries nyegezi, chuo DIT na cha wanyama pori pale pasiasi vyote ni vya serikali.
 
Kahama inajengwa na wananchi na serikali ni kama kidogo kuwekeza sababu ni hizi.

hakuna mpango maalumu serikali kuwekeza sehemu zinazokuwa ili usababisha endapo mji ukitaka kutanuliwa au kuboresha wanaingia tena kulipa fidia.

Kosa kubwa la serikali sio kivutio cha uwekezaji na mipango ndio maana kunafeli vitu vingi.

Mfano mpaka sasa kahama kuwa sehemu ya kati kwa wanaopita wasafiri hakuna stendi,uwanja wa ndege unategemea wa mgodi na idadi kubwa ya wanaopenda ndege hata takwimu zinadai abiria wengi ni wakahama.

Kahama kuna kituo kimoja cha polisi akisaidii kwa sasa mji wote wa kahama.

Swala la barabara ni changamoto
 
Ni kweli Lile Jengo Hotel lipo, na mwezi juzi hapa Rais aliienda kuliona, lkn halijakamilika na halijaanza kutumika. Ebu fikiria umeona jengo la kusema hilo tu,ina maana Kuna changamoto. Hivyo vyuo vingine ulivyotaja ukiacha cha fisheries vyote ni matawi, main campus zake ziko DSM. Licha ya hivyo hivyo ni vyuo vidogo, vinaitwa vyuo vya kati.
 
Shida yetu wabongo huwa tunakimbilia kwenye matusi. Toa hoja ni kwa namna gani swala la Chuo na Hospital siyo issue. Eleza, dadavua na chambua ueleweke
Kwani kupeleka chuo cha serikari na hospital ndio maendeleo. Mbona mwanza kitambo imeendelea bila hivyo . Kuna uhusiano gani chuo cha serikari na maendeleo
 
Kahama inajengwa na wananchi na serikali ni kama kidogo kuwekeza sababu ni hizi.

hakuna mpango maalumu serikali kuwekeza sehemu zinazokuwa ili usababisha endapo mji ukitaka kutanuliwa au kuboresha wanaingia tena kulipa fidia.

Kosa kubwa la serikali sio kivutio cha uwekezaji na mipango ndio maana kunafeli vitu vingi.

Mfano mpaka sasa kahama kuwa sehemu ya kati kwa wanaopita wasafiri hakuna stendi,uwanja wa ndege unategemea wa mgodi na idadi kubwa ya wanaopenda ndege hata takwimu zinadai abiria wengi ni wakahama.

Kahama kuna kituo kimoja cha polisi akisaidii kwa sasa mji wote wa kahama.

Swala la barabara ni changamoto
Kuna ukweli fulani. Mimi nadhani ni ushawishi wa Wawakilishi yaani Wabunge na uwezo wao wa kuweka mipango, kushawishi serikali ikiwa ni pamoja na ukaribu walionao na Makatibu wa Wizara, wenye taasisi. Watu wa maeneo hayo waliopo kwenye Wizara husika .
 
Kwani kupeleka chuo cha serikari na hospital ndio maendeleo. Mbona mwanza kitambo imeendelea bila hivyo . Kuna uhusiano gani chuo cha serikari na maendeleo
Kuna uhusiano mkubwa sana Kaka shetani. Ukipeleka Chuo Kama UDOM inayochukua watu zaidi ya elfu30, maana yake ni kwamba hao wote ni pesa. Watahitaji kula, kulala, kuvaa, mawasiliano ya simu, kunywa nk. Huo wote ni mzunguko wa pesa. Hapo hujazungumzia wale walimu wao ambao watahitaji viwanja na kujenga. Watu au wenyeni wanapata kazi au vibarua. Vivyo hivyo kwenye afya mahospitalini, hospitalini ni watu, watu ndo pesa. Hizo taasisi ni watu, watu ndo pesa, pesa ndo maendeleo. Huo ndo uhusiano wa taasisi na maendeleo
 
Back
Top Bottom