kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,666
- 4,368
Kuna mwanamke ambaye tayari nimeshamuwekea mahari lakini bado yupo kwao. Kulingana na mila za ukoo wao ukioa katika ukoo wao kabla ya wewe kumchukuwa mke wako lazima familia Yao wa kutane wacheze Ngoma zao za asili na kufanya baadhi ya mambo Yao mengine ya mila na desturi zao Baada ya hapo ndipo utakaporuhusiwa kuchukuwa mke wako na kuanza kuishi naye.
Yote hayo niliyakubali. Lakini cha ajabu na cha kuchukiza, jana mke wangu aliniita na kuniambia kuwa kulingana na mila zao anayegharamia sherehe hizo ni muoaji yaani mimi tena nitoe pesa za kugharamia sherehe zao hizo
kulipia baadhi ya ndugu zake nauli za kwenda na kurudi kugharamia chakula.
Mavazi na mambo mengine mengi pesa za sherehe ni nyingi kuliko hata mahari yenyewe.
Angekuwa wewe ungefanyaje kwenye situation kama hii.