Mila na desturi nchini Ghana zinavyowatesa wajane

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
10,258
16,498
Kwa kawaida kifo cha mtu uliyefunga nae pingu za maisha huwa kinasikitisha sana, lakini baadhi ya taratibu za kimila zinazofanyika katika maeneo mbalimbali duniani zinaweza kumfanya mjane kuumia hata zaidi hususan inapokuja katika suala la vyakula.

Katika baadhi ya tamaduni, wajane hutengwa wakati wa muda wa chakula, wanazuiwa kula vyakula vitamu, na hata kulazimishwa kushiriki katika ulaji wa vyakula unaowadunisha na wa mila au ibada hatari.

Nchini Ghana, mara nyingi ni wajane maskini sana wanaoumizwa zaidi. Wakati nchi imejaribu kumaliza mila zinazowadunisha na kuwadhuru wanaoomboleza kwa sheria, baadhi ya wajane bado wananyimwa makusudi vyakula vyenye virutubisho-au hata kufanyiwa mambo mengine mabaya zaidi.

Kuna taratibu za kimila ambapo wajane wanalazimishwa kunywa msupu ambayo ina sehemu ya miili ya waume zao.

Katika baadhi ya maeneo nchini Ghana, wajane wanalazimishwa kunywa supu ambayo ina kucha na nywele za marehemu waume zao.

"Nywele na kucha za marehemu hutumiwa, mfu huoshwa na maji yaliyotumiwa kumuosha hutumiwa kama kinywaji ambacho analazimishwa kunywa mwanamke mjane" anasema Fati Abdulai, mkurugenzi wa vuguvugu la Wanawake wanajane na yatima, ambalo ni shirika la misaada Ghana.

Baadhi ya wajane wanaweza kuepuka mila hizi zinazowakandamiza lakini wengi walio maskini hawawezi kuziepuka. BBC imeripoti Juni 23, 2020.

Katika tamaduni hizo mjane hauna haki ya kurithi mali za marehemu mumeo hadi ukubali kuolewa tena katika familia hiyo hiyo.

Inakadiriwa kuwa kuna wajane takriban milioni 285 na karibu mmoja kati ya wajane 10 ni maskini sana. Katika nchi nyingi ujane ni aibu-na Umoja wa Mataifa unauita unyanyasaji wanaokabiliana nao wajane kama moja ya ukiukaji mkubwa zaidi wa haki za binadamu.
 
Africa tuna mambo ya ajabu sana ujio wa wazunguvulituletea ustaarabu sana japo huwa tunawasengenya na kuwapiga vijembe.
 
Bado hayo yatafanyika Karne hii?

Ingekuwaje kama Wakoloni wasingelitawaka bara la Afrika?
 
Back
Top Bottom