Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Una imani na utendaji wa Jeshi la polisi?

  • Total voters
    111

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,798
12,240
Jeshi la polisi limekuwa likikabiliwa na tuhuma nyingi kwa kushindwa kuchukuwa hatua stahili na kwa wakati kudhibiti na kuzuia jinai mbalimbali. Mifano michache ni kama ifuatayo:
  1. Sakata la mmoja wa wabunge kufanya vitendo vya kishirikina ndani ya ukumbi wa bunge ;
  2. Tuhuma kuwa vyombo vya dola vinafanya njama za kuwaangamiza viongozi na watu mashuhuri;
  3. Kutoa pongezi na zawadi kwa watuhumiwa wa rushwa na ujambazi walioko ndani ya jeshi hilo;
  4. Kutoa siri za wanaotoa taarifa nyeti
  5. Kutumia nguvu kubwa kupita kiasi kukabiliana na raia; nk
Je nini imani yako kwa Jeshi la Polisi?
 
Hiyo kada sitakikabisa kuisikia. Ni waonevu sana, pata tatizo halafu uende kutoa taarifa,utajionea mwenyewe.
 
Nawakubali kwa sababu bila wao leo usalama wa nchi ungekuwa pabaya, licha ya mapungufu waliyonayo bado wanahitajika nao ni watanzania lazima tuwakubali kwa sababu wengine ni baba na ndugu zenu.
 
Nawakubali kwa sababu bila wao leo usalama wa nchi ungekuwa pabaya, licha ya mapungufu waliyonayo bado wanahitajika nao ni watanzania lazima tuwakubali kwa sababu wengine ni baba na ndugu zenu.

Hatuwakatai kama ni ndugu zetu, yaani baba, mama, watoto, wajomba, shangazi nk. Tunachokijadili hapa ni matendo yao wanapokuwa wanatekeleza wajibu wao, je wanazingatia sheria na utu au la?
 
Sitaki hata kuwaona....ukipata tatizo hawana msaada kwao linakuwa dili. Anachukua hela kwa mshtaki na mshtakiwa vilevile. Kifupi ni wanafiki na wala rushwa wakubwa. Binafsi sina mpango wa kuwa na urafiki nao. Mara kibao wanaomba lifti nawatolea mbavuni.
 
Najua kama halijakupata,unaweza sema watu wanawasema vibaya polisi.Mimi mwenyewe ninao ndugu ambao ni polisi,lakini kutokana na waliyonifanyia polisi mwaka 2000 sina hamu na hawa watu.Polisi walivamia nyumba yangu usiku wa manane eti nyumba hiyo wanaishi majambazi.wakavunja mlango(sio wote)walitoboa tundu ambalo aliyeingia ndani alitakiwa aingie kwa kutanguliza kichwa kisha kiwiliwili chote.Sasa tunajiuliza kama kweli nyumba ile ilikuwa ni ya jambazi mwenye silaha,unaingiaje nyumba hiyo kwa stahili hiyo?.Lakini baada ya yote wenyewe waligundua wamewinda ndege asiye liwa!.lakini sana hamu na hawa vimbe!!!
 
Jeshi la polisi limekuwa likikabiliwa na tuhuma nyingi kwa kushindwa kuchukuwa hatua stahili na kwa wakati kudhibiti na kuzuia jinai mbalimbali. Mifano michache ni kama ifuatayo:

  1. Wizi wa EPA, Dowans, Kagoda, Meremeta, Tangold nk.;
  2. Sakata la mmoja wa wabunge kufanya vitendo vya kishirikina ndani ya ukumbi wa bunge ;
  3. Tuhuma kuwa vyombo vya dola vinafanya njama za kuwaangamiza viongozi na watu mashuhuri;
  4. Kutoa pongezi na zawadi kwa watuhumiwa wa rushwa na ujambazi walioko ndani ya jeshi hilo;
  5. Kutoa siri za wanaotoa taarifa nyeti kwa vyombo vya habari na mafisadi;
  6. Kutumia nguvu kubwa kupita kiasi kukabiliana na raia; nk
Je nini imani yako kwa jeshi la polisi?

Jamani wana JF swali hili ni gumu sana siyo kukimbilia kulijibu kwa vile tu tunawachukia hawa jamaa...
Siku zote katika nchi yeyote polisi ni kielelezo cha ustaarabu wa wananchi na pia uadilifu wa viongozi wa nchi
Katika kujibu hapo juu chunguza kipengele kimoja kimoja
1. Wizi wa EPA, Dowans, Kagoda, Meremeta, Tangold...mtakumbuka kuwa mambo hayo yote yapo juu ya uwezo
wa Jeshi hilo kutokana na mfumo uliopo, EPA - Rais aliwasamehe warudishe fedha, Dowans/Richmond baraza la mawaziri lilianguka, Kagoda imejaa siasa nyingi, Meremeta na Tangold Mh. Pinda aliapa hawezi kuzitaja,
2.Vitendo vya kishirikina alivyofanya yule mmoja kati ya wale mapacha inajulikana hata gamba limewashinda kumvua
3.Kuangamiza viongozi mashuhuri kuna siasa nyingi hapo!!
4.Kipengele No.4 USHAHIDI UNAHITAJIKA ZAIDI(kila anayetuhumu analo jukumu la kuthibitisha)
5. Tatizo la kutoa siri ni kubwa sana hapa TZ, siku hizi siri nyigi zinavuja serikalini ndiyo maana hata habari za EPA
na nyiginezo ziliibuka hadharani( hili ni tatizo la maadili japo wakati mwingine limesaidia kufichua maovu) ila halipo kwa polisi peke yao, madaktari nao wamekuwa wakitoa siri za wagonjwa ndiyo maana watu wanaogopa kupima ngoma jirani
na wanapoishi...katika CCM, CDM,CUF zipo siri zinavuja huko kenye vyama Polisi hawapo...hili ni tatizo kubwa la kijamii linaakisi tabia zetu Watanzania kwa Ujumla. HATA HIVYO POLISI HAWANA BUDI KUONDOKANA NA LAWAMA HII WANATIA AIBU...JIREKEBISHENI HARAKA...MAKAMANDA ACHENI KUAJIRI WATOTO WENU HAWANA MAADILI
6. Hapa lipo tatizo la mafunzo wanayopata, somo la haki za binadamu liingizwe kwenye mitaala yao, aidha nafasi ya IGP iwe inathibitishwa na Bunge na aongezewe security of tenure ili asipokee maelekezo toka kwa wanasiasa bali afuate sheria bila kujali nani kakosea hata kama ni walipo madarakani washuhulikiwe kikamilifu kama wengine...
 
Nawakubali kwa sababu bila wao leo usalama wa nchi ungekuwa pabaya, licha ya mapungufu waliyonayo bado wanahitajika nao ni watanzania lazima tuwakubali kwa sababu wengine ni baba na ndugu zenu.

Kwahiyo unawakubali kwa vile ni baba na ndugu zako na siyo kwa mambo wanayoyafanya siyo?
 
Sina Imani na Jeshi la Polisi kwasababu muundo wake unawapa mamlaka wanasiasa kuwatumikisha.IGP ni Presidential Appointee, Wale Makamishina ni Presidential Appointee, Sasa hawa watu hawana uwezo wa kuwakamata wakubwa zao ambao wengine wana kinga za kushitakiwa(wateuzi), utamkamataje au kumchunguza kama anatuuma!
 
Kwa mambo yao wanayoyafanya siyapendi na wala sitotaka kuyasikia, wamekuwa wakipokea hongo siku nyingi wakaona hakuna anaewafuatilia sasa wameamua kudili na roho zetu, J e nazo tutawaachia?
 
Nawakubali kwa sababu bila wao leo usalama wa nchi ungekuwa pabaya, licha ya mapungufu waliyonayo bado wanahitajika nao ni watanzania lazima tuwakubali kwa sababu wengine ni baba na ndugu zenu.

Punguza unafiki!!!!!
 
Jamani wana JF swali hili ni gumu sana siyo kukimbilia kulijibu kwa vile tu tunawachukia hawa jamaa...
Siku zote katika nchi yeyote polisi ni kielelezo cha ustaarabu wa wananchi na pia uadilifu wa viongozi wa nchi
Katika kujibu hapo juu chunguza kipengele kimoja kimoja
1. Wizi wa EPA, Dowans, Kagoda, Meremeta, Tangold...mtakumbuka kuwa mambo hayo yote yapo juu ya uwezo
wa Jeshi hilo kutokana na mfumo uliopo, EPA - Rais aliwasamehe warudishe fedha, Dowans/Richmond baraza la mawaziri lilianguka, Kagoda imejaa siasa nyingi, Meremeta na Tangold Mh. Pinda aliapa hawezi kuzitaja,
2.Vitendo vya kishirikina alivyofanya yule mmoja kati ya wale mapacha inajulikana hata gamba limewashinda kumvua
3.Kuangamiza viongozi mashuhuri kuna siasa nyingi hapo!!
4.Kipengele No.4 USHAHIDI UNAHITAJIKA ZAIDI(kila anayetuhumu analo jukumu la kuthibitisha)
5. Tatizo la kutoa siri ni kubwa sana hapa TZ, siku hizi siri nyigi zinavuja serikalini ndiyo maana hata habari za EPA
na nyiginezo ziliibuka hadharani( hili ni tatizo la maadili japo wakati mwingine limesaidia kufichua maovu) ila halipo kwa polisi peke yao, madaktari nao wamekuwa wakitoa siri za wagonjwa ndiyo maana watu wanaogopa kupima ngoma jirani
na wanapoishi...katika CCM, CDM,CUF zipo siri zinavuja huko kenye vyama Polisi hawapo...hili ni tatizo kubwa la kijamii linaakisi tabia zetu Watanzania kwa Ujumla. HATA HIVYO POLISI HAWANA BUDI KUONDOKANA NA LAWAMA HII WANATIA AIBU...JIREKEBISHENI HARAKA...MAKAMANDA ACHENI KUAJIRI WATOTO WENU HAWANA MAADILI
6. Hapa lipo tatizo la mafunzo wanayopata, somo la haki za binadamu liingizwe kwenye mitaala yao, aidha nafasi ya IGP iwe inathibitishwa na Bunge na aongezewe security of tenure ili asipokee maelekezo toka kwa wanasiasa bali afuate sheria bila kujali nani kakosea hata kama ni walipo madarakani washuhulikiwe kikamilifu kama wengine...

Umeeleza vizuri ila nimemuuliza jamaa yangu yeye ni muajiriwa huko, darasani wanafundishwa Human rights, law of evidence, arrest na search pamoja na vitu vingi sana.

Kimsingi nimepata uelewa kuwa kumbe elimu wanaipata tatizo linakuja katika utendaji kwa kila mmoja wao.

Nadhani jeshi kama jeshi mie nina imani nalo kwa maana askari wanafundishwa miiko ya kazi, tatizo ni wao kwa maana ya watendaji baadhi wanakiuka miongozo ya kazi na elimu waliyoipata. Amini nakuambia sio kwamba hawafundishwi mambo ya HUMAN RIGHTS AND USE OF FORCE, elimu wanayo. Ni hao wanaokiuka miiko ndio wanafanya jeshi la polisi lionekane katika taswira nyingine.
 
Jeshi letu la polisi lina matatizo makubwa sana na haya matatizo ni tokea jeshi hili lilipoundwa.

Muundo wa jeshi lolote la polisi utapekea jeshi hilo kuwa la kitaalam na kujitambua kuwa ni chombo pekee chenye kuaminika kulinda usalama wa raia na mali zao.

Pia muundo wa jeshi hilo utalifanya jeshi hili kutunga sera zake na namna ya kuzitekeleza, pia kutoa maamuzi kulingana na chagizo mbalimbali zinazotoka kwenye jamii ambayo ndio inawategemea.

Ntatoa mfano wa sehemu za muundo wa jeshi hilo na mojawapo ni idara ya habari. Idara ya habari ni tofauti na idara ya uhusiano au (directorate of public affairs) ambayo kazi yake ni kuelimisha jamii na kuishirikisha jamii kwenye mambo mbalimbali ambayo yanahusu uhusiano mwema kati ya chombo hicho na raia wake.

Idara hii au (Directorate of information) ina kazi ya kuelezea kitaalam namna uchunguzi au upelelezi wa kesi kama ya Dr Mwakyembe unavyoendelea na sio bwana Manumba kuja na taarifa mbovu kabisa ambayo ina lengo la kuwachanganya wananchi. Pia katika taarifa ambayo Manumba alitoa, palipaswa pia kuwepo mmoja wa wataalam ambao wanamshughulikia Dr Mwakyembe ambae nae angekuwa anamsaidia Manumba kufafanua mambo kadhaa kuhusu ugonjwa wa ngozi ambao unamsumbua Dr Mwakyembe.

Idara ingine ambayo inaundwa na mfumo imara wa jeshi hilo ni ile ya uendeshaji au (directorate of operations). Hii idara ni muhimu sana katika jeshi la polisi na uendeshaji wowote wa operesheni katika tukio lolote lile, ndio utatoa hasa picha halisi ya jeshi hilo kama limeundwa kukung'uta watu na hata kuua tu au la.

Kwa matukio ya taarifa mbovu ya DCI Manumba, vurugu za kule Songea na matokeo yake ambapo kuna raia wameuawa na mambo mengi tu yatayoweza kujaza sehemu hii inaonekana kabisa kwamba imani kwa jeshi hili inakuwa ni vigumu kujengwa au kufanyiwa ukarabati.
 
Back
Top Bottom