Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Una imani na utendaji wa Jeshi la polisi?


  • Total voters
    111
Wanafiki wakubwa hawa, ukiingia kwenye reli zao ndo utawajua kuwa nao ni wachumia tumbo wabaya! Sipendi tabia yao wa kuwalalia walala hoi na kuwabeba vibosile.
 
Kwako akija POLISI ni matatizo,akija KAKA JAMBAZI ni matatizo!

Kwa hali ya matukio mbalimbali ambayo polisi wamehusika nayo inaonyesha kuwa kunatakiwa kufanyike mabadiliko makubwa katika muundo mzima wa jeshi la polisi. Idara ya intelijinsia hovyo! Uchunguzi na upelelezi wa makosa ya jinai haufanyiki kwa weledi! Ulinzi wa raia unafanywa kwa jazba na wakati mwingine kupelekea vifo! Ubabe umekuwa mwingi! Amri zisizotekelezeka nyingi! Maadili ziro! Rushwa kibao!

Ah! Maisha gani haya!
 
Kwako Mh. Nchimbi,
Salaam! Natumaini umzima wa afya na unaendelea vema na shughuli zako za kuiongoza Wizara Nyeti ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambayo Jeshi la Polisi liko chini yake. Mheshimiwa, inawezekana kabisa kuwa Dr. Slaa, Mnyika na Lema wamezusha madai kuwa kuna mpango wa kuwadhuru ambao unasukwa na Vigogo wa vyombo vya usalama. Siwezi kusema ni kweli au la mpaka uchunguzi utakapokamilika.

Ila Mheshimiwa kwa kuwa tuhuma zimetolewa hadharani na wewe ukatoa kauli hadharani itakuwa vema uchunguzi ukikamilika taarifa nayo iwekwe hadharani.

Ningependa kukufahamisha kuwa wananchi walio wengi (mimi nikiwa mmoja wao) hawana imani na Jeshi la Polisi. Kuna viashiria vingi tu vya kukuonyesha kukosa imani kwa wananchi na chombo hiki muhimu ambacho kiesemwa na Katiba na sheria kuwa kina jukumu la kuwalinda raia na mali zao.

Moja ya viashiria Mheshimiwa ni kuongezeka kwa wimbi la kile kinachoitwa "raia wenye hasira kali" kutoa hukumu ya kipigo kikali na pengine hata kifo kwa watuhumiwa wa makosa ya udokozi na ukwapuaji wa mali za raia wenzao. Hujawahi kujiuliza kwanini raia wanapowakamata watuhumiwa huwa hawawapeleki Polisi na badala yake wanatoa hukumu wao wenyewe???

Kwa taarifa Mheshimiwa, wananchi walio wengi wanaona kupeleka mashauri yao polisi wakati mwingine ni sawa na kupoteza muda na hata fedha. Mara nyinigi utatakiwa kununua au kutoa fedha za jalada la kufungulia shauri lako na utatakiwa kutoa fedha au kununua karatasi za kuchukulia maelezo yako.

Hapo upelelezi haujaanza. Upelelezi ukianza utatakiwa kutoa fedha za usafiri kwa askari aliyepangiwa kufanya upelelezi wa shauri lako na wakati mwingine kuvunja shughuli zako na kuambatana nao wakati wa kile wanchokiita kumtafuta mtuhumiwa wako.

Wakati mwingine utatakiwa kutoa fedha za mawasiliano (kununulia muda wa maongezi) na posho ya kuwalipa watu wanoitwa informers wa Polisi ambao wengi wana record Mbaya katika jamii halafu upelelezi unaweza kuendelea milele hasa inapotokea mtuhumiwa naye anakuwa na uwezo wa kuwapooza wapelelezi.

Mheshimiwa, katika mazingira haya bado utasema kuwa mtu asiyeliamini Jeshi la Polisi kwa maana ya askari Polisi wanaotekeleza majukumu ya Ki-polisi ana matatizo? Ningekushauri ufanye uchunguzi uone ni mashauri mangapi yaliyofunguliwa polisi ambayo walalamikaji wameamua kumwachia Mungu matatizo yao baada ya kuona wamegeuzwa ng'ombe wa maziwa na wapelelezi wa polisi, kesi zilizotupiliwa mbali na mahakama baada ya wapelelezi kupeleka ushahidi wa kitoto kwa lengo la kutengeneza mazingira ya watuhumiwa kuachiwa huru na mahakama.


Nawasilisha hoja!
 
1.Waliomteka ulimboka?
2.Waliomuwekea vinasa sauti dodoma Dr.slaa kwenye gesti ni nani?
3.walio mmwagia tindikali said kubenea nani?
4.walio muwekea sumu mwakyembe ni nani?
5.waliokuwa wakishuhudia machemuli na H.kiwia wakikatwa katwa mapanga ni nani?

Hayo maswali yanatosha kulituhumu jeshi la polisi kuhusika na unyanyasaji dhidi ya wapinzani wa serekali.
 
Hebu nchimbi,uuwe unafanya mishtukizo kama mwakyembe,hawa POLISI hujui dhambi zao au UNAZUGA????
JANA MWENZIO KAWASHUSHUA SUMATRA HAPO BUS TERMINAL
 
Kusema huna imani na jeshi la si sawa. Ila huna imani na baadhi ya watendaji wa jeshi la polisi, lakini pia huna iman na serikali iliyowatelekeza askari poli na kuwaacha kufanys kazi katika mazingira magumu.

Kuna baadhi ya askari wanafanya kazi mpaka unakubali kazi zao, lakini wengine ni waovu. Tatizo si chombo, balli ni watu na serikali yao dhaifu
 
Kusema huna imani na jeshi la si sawa. Ila huna imani na baadhi ya watendaji wa jeshi la polisi, lakini pia huna iman na serikali iliyowatelekeza askari poli na kuwaacha kufanys kazi katika mazingira magumu.

Kuna baadhi ya askari wanafanya kazi mpaka unakubali kazi zao, lakini wengine ni waovu. Tatizo si chombo, balli ni watu na serikali yao dhaifu
Kama asilimia kubwa ya askari hawatendi kazi yao ipasavyo moja kwa moja wanalipaka jeshi lote matope, sisi raia hatuna muda wa kuanza kuchambua askari moja msafi kati ya 1000 wachafu, wote watakuwa wachafu tuu na Nchimbi analijua hili vizuri sana tatizo la viongozi wetu hawapendi kutibu magonjwa wao ni kutafuta visingizio kila siku. Dawa ya jibu ni kulikamua tuu hata kama linauma!!!!
 
yuko sahihi.... jaribu kusema huna imani na chadema hapa JF kama hujaonekana una matatizo???

Mwamba ngoma huvutia kwake.

Mwambie Dk. Slaa huna imani na chama chake atasema una matatizo ya akili ... ndivyo nchimbi kasema.
 
Jeshi la polisi lipi? Hili lililotaka kumbambikia madawa ya kulevya mtoto wa Mengi Airport! Au hili ambalo Dr. Mwakyembe alilolipelekea taarifa ya mpango wa kuuawa kwake na kumhoji Sitta na kisha uchunguzi kuishia hewani!
 
Jeshi la Polisi hili lililoua watu Mwembechai, Zanzibar, Arusha, Tarime, Pande nk?
 
mh.nchimbi nafikiri amelewa madaraka maana watu kutoamini na kuwatilia shaka jeshi la pilisi nchini Tanzania ni kitu cha kawaida maana hawa jamaa hawaminiki kabisa na mtu yeyete pengine hata polisi wenyewe hawaaminiani je Nchimbi yeye yuko wapi?
 
Huyu ana tuzuga tu mbona report ya mwakyembe hajaitoa?
Alaf una lazimisha watu wawe na imani na usalama wa taifa

Alaf nchimbi kwa mdomo wake ana sema cdm ni wachonganishi wakati hajafanya uchunguzi.
 
Okmnaya na wa JF, imani hailazimishwi, hata Mwenyezi Mungu hawalazimishi watu kumwamini. Ni hiari ya mtu kuwa na imani au kutoamini. Ikifika mahali binadamu wa kawaida au chombo chochote kutaka watu wakiamini kwa nguvu ni udikiteta unaopita uwezo wa Mungu. Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo.
Kwa polisi yetu tunaamini haitatenda inayojidai kuwa na uwezo nayo. Achilia mbali polisi, Serikali inayodanganya mchana kweupe kuwa Madaktari wamerudi kazini kwa picha za kuchakachua, inawezaje kuaminiwa? Kupima kuaminiwa kwa kigezo cha kura tena za kuiba ikisaidiwa na polisi haohao wanaodaiwa kuaminiwa ni busara? Kuaminiwa ni jambo jema tena la heshima kwa anayeaminiwa lakini kama anayeaminiwa hajiheshimu kwa heshima aliyopewa mwenye kuamini anaweza kuacha kumwamini na kamwe asilazimishwe kuendelea kumwamini. IMANI HESHIMA ni vitu vya bure haviji kwa shurti.
Iweje sasa serikali ianze kulazimisha kuaminiwa. Hili linawezekana tu kama serikali iliwalazimisha watu kuiweka madarakani kwa uwazi au kwa kisirisiri au mbinu chafu.
 
Jeshi la polisi lipi? Hili lililomfananisha Kombe na jambazi? Hili lilitaka kumbambikia mtoto wa Mengi madawa ya kulevya?
 
Back
Top Bottom