Je ulifika third floor (30's) ukiwa huna unachomiliki wala kujivunia kama Mimi?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,675
Umaskini unatesa, umaskini unaaibisha sana, hakukosea aliyesema umaskini ni wa kuchukia na kukimbia, hakuna atakaye kujali mpaka utakapokua tajiri wazee.

Ukiwa maskini kwenye ukoo watakuona kama mpiga kelele tu, imagine mtu mzima 30's napata kipato cha laki nne kwa mwezi, sina kiwanja wala mke wala mtoto, najua kukata tamaa ni Mwiko lakini nawaza niingie vijiji vya mbeya huko labda naweza kupata mawazo mapya hata ya kilimo.

Sielewi kabisa, natembea kilometers moja kulifata kanisa, watu wamepaki magari nje mimi nipo nipo tu, kutoa zaka yenyewe ni mgogoro, watu wanajadili mipango na maendeleo ya kanisa, hawakushiriki kwa sababu wanajua huna uwezo wa kutoa. Mtaani napo watu wanakuchukulia poa tu, hasira zote hizi nimezipata baada ya mtu kunidharau waziwazi kwamba sina mbele wala nyuma Dah.

Kiukweli umaskini sio wa kuchezea, maisha haya yenyewe ni mafupi utajikuta unaishi kwa shida na stress sio poa.

N.B, kuna million 15 nataka niikope sehemu hebu nipeni ramani nianzie wapi niishie wapi, sina elimu yoyote ya biashara sijawahi kufanya biashara yoyote ile, nifanyaje kidogo niingie 40's nikiwa na kibanda?
 
Hizi mada zenu za kupanda ngazi tumezichoka sasa

Tunakatishana Tamaa

Mwishowe mtu anajiona kama amechelewa maisha...

Unataka uondoke kwenu? ...Komaa hapo hspo kwa baba ako ...

Kama Yesu alirudisha mpira kwa kipa na hataki kabisa kurudi Duniani ..wewe ni nani sasa
 
Huo mkopo utaweka asset gani kama huna hata kiwanja?
Tuachane na hayo,ukipata wekeza katika kilimo huku Mbeya katika wilaya zake fursa zipo katika kilimo cha tumbaku kama zao la biashara (si mpaka uvute),viazi mviringo,chai,kahawa,karanga na maharage. Karibia huku.
 
Umaskini unatesa, umaskini unaaibisha sana, hakukosea aliyesema umaskini ni wa kuchukia na kukimbia, hakuna atakaye kujali mpaka utakapokua tajiri wazee.

Ukiwa maskini kwenye ukoo watakuona kama mpiga kelele tu, imagine mtu mzima 30's napata kipato cha laki nne kwa mwezi, sina kiwanja wala mke wala mtoto, najua kukata tamaa ni Mwiko lakini nawaza niingie vijiji vya mbeya huko labda naweza kupata mawazo mapya hata ya kilimo.

Sielewi kabisa, natembea kilometers moja kulifata kanisa, watu wamepaki magari nje mimi nipo nipo tu, kutoa zaka yenyewe ni mgogoro, watu wanajadili mipango na maendeleo ya kanisa, hawakushiriki kwa sababu wanajua huna uwezo wa kutoa. Mtaani napo watu wanakuchukulia poa tu, hasira zote hizi nimezipata baada ya mtu kunidharau waziwazi kwamba sina mbele wala nyuma Dah.

Kiukweli umaskini sio wa kuchezea, maisha haya yenyewe ni mafupi utajikuta unaishi kwa shida na stress sio poa.

N.B, kuna million 15 nataka niikope sehemu hebu nipeni ramani nianzie wapi niishie wapi, sina elimu yoyote ya biashara sijawahi kufanya biashara yoyote ile, nifanyaje kidogo niingie 40's nikiwa na kibanda?
Hii ndiyo third floor(30's)! Na hii 3rd. ni ngapi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom