Je, toyota IST inafaa kwa safari za mkoani?

Ili kudumisha maisha ya Gari yako, nashauri pumzika Singida then Ingia Mwanza kesho yake utafika poa kabisa. Mi Ki Ipsum changu nilitoka Iringa nikalala Tabora kesho yake Mwanza tena Sengerema sikuona utofauti wowote mpaka sasa nadunda tu hapa Iringa.
Tumia huu ushauri mkuu
Inatoboa ila sina hakika kama ni moja kwa moja
Huu pia unafaaa mkuu
Inatoboa mwanza mapema sana mkuu hata usiwaze kabisa mwanza mapema sana bila touch mwanza masaa 9
Huu pia mkuu
 
Mimi nilisafiri na Passo Piston3 kutoka Dar mpaka Mwanza nilitoka Dar saa 9 kama na nusu nikaingia Mwanza saa 2 usiku wala sikupata tatizo lolote njiani wala sikupigwa Tochi ilikuwa mwaka jana mwezi wa 10 na niliendesha mwenyewe muda wote wa safari.
Saa 9 ulikuwa unamaanisha saa tatu asubuhi au saa tisa alasiri?
 
Napingana nawewe kwenye swala LA 70kph kwann kwanza kabisa hizo gari wasingetoa na speed limit ya 160.wangetoa speed 90 kama ilivyokuwa kwa Volkswagen na Peugeot za zaman.2.barabara Japan na nchi za wenzetu zilizoendelea hatuwezi jifanananisha hata kidogo.cc tunatembea30. 50. Ukibonyeza kidogo 50 hiyo.wenzetu kunamahali huruhusiwi kuendesha chini ya 120kph.

Hili LA kuzima gari baada ya kutoka safari ndefu nakubaliana na wewe.ila nakuuliza MFANO nimetoka mbeya nakuja dar nimefika chalinze gari haItembei tena ule mwendo niliokuwa nao kutoka mbeya -chalinze, sasa natembea 70, 60,20 nafika kimara sasa ndio kusimama na kusogea he nikifika sinza kuna haja ya kuacha gari silence?
Nikueleweshe zaidi mkuu wangu suala la speed kuwekwa 160 au 180 haimaanishi ndio uendeshe kwa mwendo huo pili kwa nchi za wenzetu high way kuendesha ni speed 100 kuendelea au kama huendeshi mwendo huo unatakiwa kuendeshea service road na pia ni mara chache kukuta unaweza kundesha speed 100 au zaidi kwa km 50 au zaidi katika nchi za wenzetu. Lazima utakuta kuna taa,vizuizi nk ila nchini kwetu unaweza kuendesha speed 150 hata km 100 na bila kukuta hizo sheria na vizuizi. Hivyo wenzetu wakiendesha speed 100 akiona gari yake imezidiwa anasogea service road anaendesha mwendo anaotaka kuipimzisha gari yake. Huwa Ninakwenda mara nyingi kununua magari ya wateja wangu wanaponiagiza au magari ya kuweka yard kwangu kuyauza na ninapokuwa nayatest mfano yokohama au tokyo ndipo ninapokutana na hizo sheria za uendeshaji nilizokuambia hapo juu.pia speed ya gari toyota landcruiser mkonga iliyotengenezwa japan original ukiendesha ukiwa speed 100 na gari aina hiyo hiyo toyota landcruiser mkonga iliyotengenezwa afrika kusini ukiendesha speed 100 unaweza ukashangaa toyota original na hii toyota under licence utakuta zinapishana haziendi speed sawa moja itakuwa mbele zaidi ya nyingine Kwa mfano huu naimani utakuwa umenielewa au basi la abiria utakuta lina dashboard ina speed 100 tu ila basi hilo likiwa speed 80 unatashaangaa wewe unaendesha raum uko speed 120 lakini basi linakupita Hivyo dasboad speed sio kipimo tosha cha kujua mwendo unaoendesha ni ule uliooneshwe kwenye spedometer ya gari yako. Au utakuta unaendesha sehemu kuna kibao cha 50 kmph na dashboad yako inasoma 50 kmph ila utapigwa tochi na ukipewa picha ya gari yako utaona inasoma 65 kmph au 70kmph unapigwa fine.hivyo volkswagen akiwa speed 70 utashangaa wewe toyota uko speed 100 na bado mnaenda sawa. Kuna mambo mengi ya kujifunza bado kuhusu gari mkuu

. Nikujibu swali la pili kulingana na foleni haswa unapokuwa unaingia dar kuanzia mlandizi hadi kufika ubungo ni sawa na kuipooza gari yako kama nilivyotoa maekekezo hapo juu kwani foleni na gari iko silence injini inapoozwa vyema unaweza ukafika na kuizima gari yako mkuu.
 
Habari wanajamvi,

Nimetokea kuipenda sana gari toyota IST. Kilichonifanya niipende ni ulaji wake wa mafuta, haina gharama kwenye mafuta. Sasa swali langu je mtu akiamua kusafiri na IST kutoka DAR kwenda Mwanza atatoboa?

Nisaidieni please. Kama kuna mwenye ushauri pia niambieni
Kuna moja nilisafiri nayo aisee me sio mpenzi wa toyota ila kapo vzuri bana ndani kapo very smart..kanatoboa ukikalazimisha ila uckaoverload. Ila kapo fresh sana yan maana ckutegemea kama kangekua vile..
 
Unaenda tena vzr tu, Mim ninayo hua natoka Mwanza saa mbili asubh naenda Dom saa kumi Au kumi na moja Nipo dom vzr kabsa. Cha msing Fanya service ya oil vzr, hakikisha coolant iko vzr na break. Njian Utakua unapita Kama risasi tu
 
Tuambie inakula lita ngapi kwa kilometa . Then Mwanza ni kilometa 120, na utueleze ujazo wa tank lako la mafuta, hapo ndo utajua kama utatoboa ama hutatoboa ukiweka mafuta kiasi gani. Kama ni masuala ya mechanical mcheki fundi kwanza akufanyie safari checkup. Otherwise sijui kama una uzoefu wa sfari ndefu pia.
Lakini la mwisho jiuluze hizo IST zilizopo mwanza zilibebwa ama zilipaa? Fikiri kabla hujauliza.
Toka Dar to mwanza ni km 120?????

Dunia imezungukaje hivyo????
 
Habari wanajamvi,

Nimetokea kuipenda sana gari toyota IST. Kilichonifanya niipende ni ulaji wake wa mafuta, haina gharama kwenye mafuta. Sasa swali langu je mtu akiamua kusafiri na IST kutoka DAR kwenda Mwanza atatoboa?

Nisaidieni please. Kama kuna mwenye ushauri pia niambieni
Hiyo gari ni nzuri sana ,wewe ndo utachoka siyo gari.

Unajua kwa sisi tuliozoea safari Mwanza napaona karibu yaani ni kama vile kutoka home kwangu kwenda sokoni tu.
 
hpo unatoboa mzee vizur kabsa,lkn mi kwa safar za mkoan gar nzur zile zilizojuu,gar zilizochin sana bn huwa zinachosha sana hasa miguu na kiuno,
 
Usimwogopeshe. Ist kwa safari ndefu ndio mahala pake. Nimeenda Mwanza na kurudi na Ist zaidi ya mara 20 haina kuchemsha wala pancha.
Gari ni service tu. Hizo ulizotolea mifano zilikuwa hazipo sawa kwa sababu zingine za kiufundi lakini sio sababu ya aina ya gari.

Nimezunguka na Ist katika njia mbaya za migodini lakini imehimili.
Uimara wa gari ni service tu.

Kwa upande wa matumizi ya mafuta Ist zinatumia vizuri sana. Mfano mie nikijaza hapa Dar lita 42(full tank ya Ist cc1498) huwa yanafikisha Dodoma. Muda ninaotumia huwa natoka Dar saa 9 alfajiri na ninafika Dom 1.30 asubuhi.
Nikijaza Mafuta Dom lita 35(kwa sababu kunakuwa kuna mafuta kidogo kwenye tank) yananifikisha Shinyanga. Hapo naongeza lita 10 tu na yananifikisha Mwanza na mizunguko ya siku inayofuata bila wasiwasi.
Unaenda hadi mwanza bila kupumzika njiani ???
 
Back
Top Bottom