Je, teknolojia ya roboti wanaoongea ilikuwepo wakati wa Musa na Haruni kama Kurani?

Wewe sio wa kwanza kupinga Uislam na Muhammad na hautakuwa wa mwisho asilani. Tunaojua hizo dini tunakuangalia halafu tunasema hiiiiiiiiiiiii ( kwa sauti ya Mkulu). Unatumia nguvu nyingi kutaka kurekebisha dini ya wenzio.....tumia nguvu nyingi kueleza dini yako. Pengine hilo lina manufaa zaidi. Hizi ni pang'ang'a tu hazina hoja. Unawaona wenzio wanapiga pesa kupitia dini...wakina Lusekelo na wengineo? Kafanye kama vile, ina manufaa zaidi kuliko huu upuuzi wako humu. Hupati kitu na unapoteza time na bundle lako bure kabisa. Umewasikia wakina Lusekelo wanaponda Uislam. They are busy making money. Shame on you.

Sent using my NOKIA torch
Kaka nimekukubali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KABLA HATA SIJAZIELEKEA HIZO HOJA ZAKO...NAOMBA MUONGOZO UFUATAO...

UKIACHANA NA HIZO AYA ULIZOCHOMOA KWENYE BIBLE...

TUPE EVIDENCE ZINAZOTHIBITISHA USAHIHI WA HIZO STORY NA POROJO ULIZOSHUSHA NA KUJENGEA HOJA...?
 
1. Kwa hiyo,kwa kuwa Ismaili(Ishamaeli) ndiye aliyetakiwa kutolewa sadaka,kwa hiyo yeye ndiye aliyempa Muhammad habari za Roboti wa Ndama kuundwa na msamaria?

2. Kurani imekuja miaka 500 baada ya Biblia,je inakuwaje Kurani ndio iwe inasema ukweli katika kile inachokisema Biblia na kwa ushahidi gani hasa?Ni kwa ushahidi tu wa kule pangoni tu? Na kama ni kwa ushahidi huo tu, ni kwa nini hata Muhammad mwenyewe hakuuamini ushahidi huo hadi akaenda kwa mjomba wake,Khadija,Mchungaji wa Ki-nestorian, ku-clear doubt? Je,katika mazingira kama hayo. ina maana Muhammad alikuwa anamuamini zaidi mchungaji Waraqahal kuliko malaika Jibrili aliyekuwa ametumwa na Mungu kwake?
Hivi ni kwanini yule aliyemkaba Mohamad kule Pangoni hakujitambulisha ?
Na je, yule Padri Walaqa, aliyetabiri kuwa Muhamadi ni mtume, yeye aliambiwa na nani kwamba amwambie Muhamadi kuhusu kuwa mtume ?
Ivi Waraqa naye alishushiwa Wahayi ili atambue utume wa Muhamadi ?
Au naye Waraqa alitokewa na Jiburiri ?
Duh.. hadi niko hoi kwa hii sintofahamu.
 
Hivi ni kwanini yule aliyemkaba Mohamad kule Pangoni hakujitambulisha ?
Na je, yule Padri Walaqa, aliyetabiri kuwa Muhamadi ni mtume, yeye aliambiwa na nani kwamba amwambie Muhamadi kuhusu kuwa mtume ?
Ivi Waraqa naye alishushiwa Wahayi ili atambue utume wa Muhamadi ?
Au naye Waraqa alitokewa na Jiburiri ?
Duh.. hadi niko hoi kwa hii sintofahamu.
Kwanini unakaaa na maswali mepesi haya hautuulizi wataalam
1. aliemkaba Mohamadi alijitambulisha kuwa ni JIbril
2.kwani kuna ubaya gani waraqa kumtambua Mohamadi kuwa ni mtume? mbona watu wengi tu walimtambua Yesu lakini walikuwa sio wanafunzi wake
3.kwani kutambua jambo mpaka uwe na wahayi? ni elimu juu ya jambo lile ndio linaleta utambuzi sio wahayi
 
Ukiona mtu hajibu hoja hata moja,anatoa maneno ya hovyo tu,ujue Hana Cha kujibu.Yaan anachokiamini hakina uwezo wa kujitetea.Quran ni hadithi za paukwa pakawa,Hilo halina ubishi.
Hoja zote zimejibiwa wacha kelele wewe , labda wewe utuambie wapi ujaelewa
 
Hakuna kitu kama hicho katika Quran (Surati Twaha 20:85-95). Umepotosha na kuongopa.
Umeshindwa kuelewa na hutaelewa kwa kuwa lugha iliyotumika huielewi. Kwa kuwa title yako
ndio imebeba maudhui yote ni kama bandiko lote linakosa uhalali.

Kurani na yenyewe katika Sura Ta Ha 20: 85-96,inasimulizi lile lile, ila ambalo inaonekana limefanyiwa editing kidogo.Tofauti na inavyoelezwa katika Biblia,katika Kurani Muhammad, anasema aliyewatengenezea Waisrael sanamu ya Ndama huyo ni Msamaria mmoja,ambaye hamtaji jina.Kitu kingine ambacho Muhammad anakisema kuhusiana na kisa hicho, ni kwamba sanamu hiyo ya Ndama ilikuwa na uwezo wa kuongea!Jambo la tatu, ni kwamba eti Mungu ndiye aliyewatega waisrael kuona kama ni wavumilivu,hasa baada ya Musa kuwa amewaacha Waisraeli na kaka yake Haruni,kwa muda mrefu bila kurudi.
 
Wanazuoni wa kiislamu wanadai iliandikwa na Mungu na kisha akampatia malaika Jibrili(Gabrieli?) bila kufanya editing yoyote ile akampasia Muhammad na Muhammad akiisha kuipokea, hakuwahi kuichezea na hata leo waislamu hawajaichezea aslani.
Hahahahahahaha....Mudy bana!
 
Naona wametukomalia sana Uislam ila hawatuwezi katika dini ambayo ni imara ndio hiii nyie level yenu pambana na wasabato kwanza....kwanza nyie kila dhehebu lina biblia yake malizaneni kwanza nyie hii ngoma kubwa hutaweza narudia hutaweza
 
Kwa hoja hii naonna kabisa kuwa mpuuzi ni WEWE, eti mwislam haiamini biblia wakati tunamtambua nabii ISSA wa biblia kuwa nabii kamili wa mwenyezi Mungu!huku uislam huo huo ukimtambua Ibrahim wa biblia,huku tukifundishwa kuwa Biblia ndiyo iliyoutabiri ujio wa Mtume wetu mtukufu? Acha kuukufuru uislam!
Tunaamini injili ndio kitabu sahihi cha Yesu
 
Surah ya 15(All hijr) verse 26

Allah alimuumba binadamu kwa udongo unaotoa sauti..

Na yeye aliumba roboti nn huo ndio uandishi wa Quran bana yaaan raha tupu
 
Mada za kuleta mgawanyiko! Anyway ndo uhuru wa kujieleza mlioutaka
 
Wanabodi:

Baadhi ya Wanazuoni wa Kiislamu hawataki kukubali kwamba Kurani ina maelezo au masimulizi ya visa ambavyo ama havikuwahi kutokea katika historia ya maisha ya mwanadamu au kwamba visa hivyo haviko kama vinavyoelezwa na Kurani yenyewe.

Leo,ninacho kisa kingine kinachomuhusu Musa na Kaka yake, Haruni, wakiwa na wanaisrael.Kisa hicho, tunakikuta katika Biblia,Agano la Kale,Kutoka Kitabu cha Kutoka 32:1-10:

“1Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.2 Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee.3 Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni.4 Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.5 Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Haruni akatangaza akasema, Kesho itakuwa sikukuu kwa Bwana.6 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze.7 Bwana akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao,8 wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.9 Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu10 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.”

Kurani na yenyewe katika Sura Ta Ha 20: 85-96,inasimulizi lile lile, ila ambalo inaonekana limefanyiwa editing kidogo.Tofauti na inavyoelezwa katika Biblia,katika Kurani Muhammad, anasema aliyewatengenezea Waisrael sanamu ya Ndama huyo ni Msamaria mmoja,ambaye hamtaji jina.Kitu kingine ambacho Muhammad anakisema kuhusiana na kisa hicho, ni kwamba sanamu hiyo ya Ndama ilikuwa na uwezo wa kuongea!Jambo la tatu, ni kwamba eti Mungu ndiye aliyewatega waisrael kuona kama ni wavumilivu,hasa baada ya Musa kuwa amewaacha Waisraeli na kaka yake Haruni,kwa muda mrefu bila kurudi.

SASA, Wasamaria ni akina nani?

Wasamaria wanatajwa kuwepo baada ya utawala wa Israeli kwa upande wa Kaskazini katika Palestina kuangukia mikononi mwa dola ya Assyria mnamo mwaka 722KK na hiyo ni kama karne saba baada ya Musa kuondoka duniani.

Wasamaria ilikuwa ni jamii ya watu waliokuwa wakiishi katika Dola ya Kaskazini mwa Israeli(Northern Kingdom of Israel).Samaria ni jina la mji uliokuwa makao makuu ya Dola hiyo (Ufalme huo) na hivi watu walioshi katika dola hiyo ya Samaria waliitwa Wasamaria.Mji wa Samaria, ulikuwa katikati ya mji wa Galilaya (kwa upande wa kaskazini) na mji wa Yudea(kwa upande wa Kusini).Wasamaria kwa rangi walikuwa mchanganyiko wa Wayahudi na uzao wa wapagani(racially mixed society with Jewish and pagan ancestry).

Kiimani pamoja na kwamba,wasamaria walikuwa wakimuabudu YAHWEH(Mungu, kama Wayahudi walivyokuwa wakimuita), sawa na wayahudi walivyofanya,dini yao haikuwa dini kuu ya Kiyahudi(mainstream Judaism).Wasamaria walikuwa wakivikubali vitabu vitano tu kati ya orodha ya vitabu viliyokuwa vikikubaliwa, na Hekalu lao lilikuwapo katika Mlima Gerazimu(Gerazim) badala ya lile Hekalu la Kiyahudi lililokuwa katika Mlima Sioni,kule Yerusalemu kama tusomavyo katika Injili ya Yohana 4:9,20-21:

“9Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia. 21Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.”

Wasamaria wa nyakati za Yesu walikuwa wakiamini kwa dhati juu ya Mungu mmoja kuliko hata Wayahudi wenyewe na namna fulani walikuwa wameshika sana sheria za Musa kuliko hata Wayahudi,kwa namna ya pekee,suala la Sheria za Sabato.Tofauti ya Wayahudi na Wasamaria ilikuwa ni kwamba wayahudi hawakuruhusiwa kutamka jina takatifu la Mungu “YAHWEH” katika viapo, isipokuwa aliyeruhusiwa kufanya hivyo alikuwa Kuhani Mkuu tu,tena akiwa huko patakatifu pa patakatifu,tena mara moja kwa mwaka na hiyo ilikuwa katika siku ile ya toba ya taifa (ndiyo,Yom Kippur). Wasamaria wao kutamka jina takatifu “YHWH” (soma “YAHWEH” ) kwa sauti au kimya kimya halikuwa tatizo hata kidogo.`

Kwa hiyo, Wayahudi wote wa kawaida hawakuwa na ruhusa na hata leo bado hawaruhusiwi kusoma, si kwa sauti tu wala kimya kimya,herufi za jina takatifu la Mungu, YHWH, kwa sababu ya utakatifu wa jina la Mungu wao. Kwa nini? Kwa sababu kuzisoma bure bure kungelingana na utovu wa heshima kwa Mungu mkuu na kuivunja amri ya Mungu ya kutolitaja bure jina lake, DECALOGUE. Ndiposa, ilikuwa marufuku na bado ni marufuku kabisa Myahudi wa kawaida kuzisoma na kuzitamka herufi hizo.

Kwa hiyo,kutokana na wasamaria kuonekana hawashiki sawa sawa dini ya Kiyahudi na kwamba walikuwa na vinasaba vya damu ya kipagani,basi walikuwa wakidhauriwa na kutengwa na wayahudi wa Kawaida.Na ndiyo maana utashangaa kwa nini wayahudi walipokuwa wakisafiri kutoka Yudea kwenda Galilaya au Galilaya kwenda Yudea,walilazimika kuvuka mto Jodani kisha kuambaaambaa ng’ambo ya Jodani na kisha kuvuka tena mto Jodani walipokaribia kufika Galilaya au Judea ili kukwepa kupitia ardhi ya Samaria kwa kukwepa wasije wakanajisika. Kwa hali hiyo,wayahudi hawakuchangamana na wasamaria na walijengeana chuki au uhasama dhidi ya Wayahudi wa kawaida. Ni kutokana wasamaria na ni kwa mazingira haya,ndiyo kisa hata Yesu alinyimwa sehemu ya kulala katika Kijiji kimoja walipokuwa wakiishi Wasamaria, kwa sababu tu ya Uyahudi wake na wala si kwa sababu hakuwa na uwezo wa kulipia sehemu hiyo.Soma Luka 9:51-56:

“51 Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu;52 akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali.53 Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu.54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa.Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.”


Maswali ya Kujiuliza:

  • Je,Muhammad anaposema kuwa Msamaria alimshika Unyayo,anataka kuieleza na kuiaminisha jamii ya Kiislamu kwamba wakati sanamu ya ndama huyo inatengenezwa yeye alikwisha kuzaliwa, hata iwezekane kwa huyo msamaria kumshika unyayo kabla ya kumuunda ndama huyo?

  • Kwa namna inavyosimuliwa katika aya hiyo nukuliwa ya Kurani,mbona inatoa tafsiri kuwa yeye Muhammad alikuwa sehemu ya mchakato wa kuwezesha kuundwa kwa sanamu hiyo baada ya kuwa ameguswa unyayo wake? Na kama ndivyo,je,Muhammad haoni kama na yeye alikuwa ni sehemu ya kumkufuru Mungu sawa na yule msamaria?

  • Je,ikiwa Muhammad ni mtume wa mwenyezimungu (na msamaria aliwaundia waisrael sanamu iliyochukua nafasi ya Mungu, jambo ambalo ni kufuru),iliwezekanaje kwa Muhammad kukubali kushikwa unyayo na msamaria ambaye alikuwa na nia ovu ya kuwapotosha waisrael kwa kuwaundia kikaragosi cha Mungu?

  • Je, simulizi la Kisa hiki nalo limetumia lugha ya picha kama ilivyo katika kisa cha ndege na mchwa kutumika kama wanamgambo, kama tulivyoelezwa na wanazuoni wa Kiislamu katika mjadala uliopita, wa Ndege kutumika kama maaskari katika vita?

  • Je,kwa kuchukulia kweli kwamba msamaria ndiye aliyeunda roboti ya ndama iliyokuwa inaongea,msamaria huyo alikuwa na nguvu za kutenda miujiza? Na kama msamaria hakuwa na uwezo huo wa kimiujiza,je, alitumia tekinolojia gani wakati huo kuweza kuunda sanamu iliyokuwa inaoongea?

  • Historia inaonyesha Muhammad alizaliwa mwaka 570BK na kufariki dunia mwaka mnamo tarehe 8 Juni 632BK. Na Musa na Haruni(pamoja na huyo msamaria aliyetengeneza roboti la Ndama), waliishi miaka mingi sana kabla ya Yesu. Je,iliwezekanaje kwa huyo msamaria kuweza kumshika mtume unyayo katika mchakato wa kuliunda lile roboti wakati Mtume(Muhammad) hakuwa amezaliwa bado?

  • Je,kwa kadri ya historia ya uhasama kati ya Waisraeli na Wasamaria,na iwapo tukizingatia maelezo ya Muhammad, iliwezekanaje kwa Waisraeli kuweza kuchangamana na huyo msamaria, hata waweze kukubali kutengenezewa sanamu(roboti) na adui yao?

  • Kwa kuwa Kurani ni maneno ya Mungu yaliyoshushwa moja kwa moja kwa Muhammad(bila editing yoyote) toka kwa Mungu,je, kwa kisa hiki ambacho imeonekana ni uongo wa kihistoria,ni nani muongo?Ni Mungu anayedaiwa kumpelekea Muhammad Kurani au ni Muhammad tu ndiye alijisingizia kuwa Kurani ni maneno ya moja kwa moja,ambayo hayahaririwa,toka kwa Mungu?
Kwa maswali haya pamoja na mengineyo munayoweza kuongezea,nawakaribisheni,sasa kwa mjadala.

Kwani hasa tatizo lako ni lipo juu ya huu uislaam.
Waache waislaam na uislaam wao,wayahudi na uyahud wao na Makafiri na ukafiri.
Kipi hasa kinakuuma dhidi ya uislaam?
Surat 109:1-6)
Wewe kaa na ukafiri wako tuache sisi na dini yetu
 
Back
Top Bottom