Je serikali imebadili nembo ya taifa kimyakimya bila kufuata utaratibu wa Kikatiba na kisheria?

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
208
462
Na Yericko Nyerere

Rais wetu Samia anatumia hii nembo ya taifa gani katika nchi ya TANZANIA? Je watu wanaelewa kweli hatari ya jambo hili? Nani katwaa Urais wa Rais Samia? Tunamtaka aliye twaa Urais wa Samia aurejeshe haraka sana!

Kwamjibu wa Sheria ya Nembo ya Taifa ya Mwaka 1971 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977, Nembo ya Taifa hi hiyo inayoonekana kwenye picha ya Hayati Rais Magufuli, ambapo Sheria inasema Nembo ya Taifa itakuwa na Picha mbili za bibi na Bwana walioshika oembe za Ndovu huku wakiwa wamegeukiana mbele yao wakifunika alama ya Mwenye, Jembe na Nyundo.

Lakini hiki kinachoonekana katika hotuba nyingi za Rais Samia sio Nembo ya TANZANIA, ni nembo mpya ambayo haifahamiki ni ya taifa gani, inafanana kiasi na nembo ya Rais japo haina bendera ya Taifa pia rangi hazifanani, Tunahitaji ufafanuzi wa kina katika hili.

Rais Samia ni rais wa Tanzania, anatakiwa na Katiba ya Nchi na sheria zake kuzitii kwakuzitumikia. Sharia ya Nembo ya Taifa inamtaka kutumia nembo halisi ya taifa, na sio nembo bandia.

ifahamike kuna "Nembo ya Rais" ambayo iko tofauti na nembo ya Taifa, hii inapatikana katika Bendera ya Rais, Hakuna sheria inayosema Rais atumie nembo ya Rais katika mimbari za Hotuba, Na kwakuwa hakuna Sheria hiyo inayomlazimisha, Basi ni wajibu tuheshimu sheria ya Nembo ya Taifa ya 1971. Hii ndio inatuongoza!

Utaratibu wa Kiprotokali tangu taifa lipate Uhuru, Rais anapo Hutubia kinachotakiwa kuwa mbele yake kwenye mimbari ni Nembo ya Taifa, na Pembeni yake (kulia na kushoto) inasimama Bendera yenye Nembo ya Rais.

Natoa changamoto kwa Wanasheria na Wakuu wa itifaki ya Rais, Je Matumizi ya "Nembo ya Rais" ni Takwa la Kisheria? Ni Wapi Rais atatumia Nembo ya Taifa kwenye mimbari, na Ni wapi atatumia Nembo ya Rais kwenye mimbari?" Kaka yangu Gerson Msigwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Tunaomba ufafanuzi wa jambo hili zito.
1691775275394.jpg
 
Aliyeandika anachanganya mambo, nembo ya Taifa na nembo ya Rais.
Aende ku dig more
Leo umenipa kitu kipya kuhusu alama za taifa. Kumbe huwa kuna nembo ya rais.

Siku zote najua kuja nembo ya taifa tu. Kwa upande mwingine kuna bendera ya rais na bendera ya taifa.
 
Huyo jamaa ni mpuuzi ina maana hajui kwamba hiyo ni nembo ya Rais? Hata gari yake inakuwa na hiyo nembo. Kuna events anawekewa bendera na meza yenye hiyo nembo na kuna event nyingine anawekewa ile ya serikali.
 
Huyo jamaa ni mpuuzi ina maana hajui kwamba hiyo ni nembo ya Rais? Hata gari yake inakuwa na hiyo nembo. Kuna events anawekewa bendera na meza yenye hiyo nembo na kuna event nyingine anawekewa ile ya serikali.
Ameuliza ni nembo ipi itumike wapi na ipi itumike wapi, toa ufafanuzi kama unajua, nikuelimishana tu.lkn ukiona mtu kaulizwa swali anayetakiwa kujibu akafoka jua kuwa hajui au elimu yake ni ya kuungaunga.
 
Back
Top Bottom