Majaliwa: Suala la Picha ya Rais Samia kuwekwa kwenye fedha litajadiliwa

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Akijibu hoja ya Ng'wasi Kamani kuhusu kuwekwa kwa picha ya Rais Samia kwenye fedha zetu Bungeni leo, PM Majaliwa amesema suala hilo litajadiliwa kwa kina.

"Maamuzi ya kuweka picha kwenye noti mara nyingi yanafanywa na kiongozi mwenyewe kwa kushauriana na Benki Kuu, kwa kuwa umelileta hili na sisi tunatambua mchango mkubwa wa Rais Samia Hassan kwenye Taifa hili, niseme tu tunapokea ushauri wako na litaingia serikalini na litajadiliwa pale ambapo watafanya maamuzi taarifa rasmi zitatolewa,"- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Kama ulipitwa ni kwamba Ng'wasi Kamani alisimama Bungeni leo na kutoa hoja ya kuweka picha ya Rais kwenye fedha za Tanzania.

"Mhe Waziri Mkuu mwaka 2006 Bunge hili lilipitisha sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya kuipa mamlaka benki hii kudizaini fedha kwa kuweka nembo na material mbalimbali, mwaka 2021 nchi hii imepata Rais wake wa kwanza mwanamke anayefanya kazi nzuri na anatambulika katika Bara la Afrika na duniani kama Rais madhubuti na wa mfano, Je serikali haioni sasa kuna haja ya kuweka kumbukumbu ya kudumu kwa Rais Samia kwa kuweka picha yake katika fedha za nchi hii?," - Ng'wasi Kamani

Written by Mjanja M1 ✍️
 
Back
Top Bottom