ruhi
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 3,736
- 5,425
Inafikirisha sana kusikia kila leo kumetokea ajali na vifo vya abiria vikiwa vingi sana hadi unajiuliza, je serikali inashirikiana na madereza pamoja na wamiliki wa mabasi kutengeneza ajali?
Je, mabasi haya kabla ya kusafiri/kuanza safari zinakaguliwa na chombo gani na kuruhusu waendelee na safari?
Utakuta kwa mfano gari linatoka Dodoma linafika Dar es salaam then linashusha abiria na kupakia abiria kwa ajili ya kuanza safari ya kurudi...ni chombo gani inajiridhisha na uhimara wa gari ili ianze safari tena?
Wamiliki wa mabasi jaribuni kuwashauri madereva ambao mmewapatia jukumu la kuendesha magari yenu kuwa waache kujiona kuwa wao wenyewe ndiyo wenye haki ya kuendesha magari wanavyojisikia. Ukiwa unaendesha gari ndogo alafu basi la abiria anavyo Overtake gari yako au magari mengine inasikitisha sana.
Swali la msingi, kwanini mabasi ya abiri yanayofanya safari zao nje ya nchi yanaendeshwa kwa utaratibu bila kutokea ajali za mara kwa mara kama mabasi yanayofanya safari za ndani ya nchi?
Nitoe wito pia kwa abiria, msiwe kama kondoo wakati mnapokuwa safarini; mwambieni driva ukweli kama anakeuka taratibu za uendeshaji.
Utakuta pale mbele kwa dereva pako open kabisa na amejaza staff wake wanapiga stori na simu pia anatumia kitu ambacho kinampunguzia umakini lakini abiria wamekaa kimya kabisa bila kumkanya.
Traffic wanaokaa barabarani acheni tabia ya kufika mlango kwa mabasi then unahamasisha abiria kufunga mkanda bila kuwabana wenye gari kabla ya gari kuondoka stendi mmekagua gari kama mikanda yote ni salama kwa ajili ya matumizi. Utakuta mkanda wa Gari ni chafu alafu haifungi vizuri mpaka unajiuliza SUMATRA wao kazi yao ni nini?
Serikali iingilie kati na kuangalia namna bora ya kupunguza ajali hizi zinazoleta umasikini kwa wananchi wake na kuwaachia wengine kilema za kudumu kwa sababu ya uzembe ya watu wachache.