Je rukhsa kuoa mdogo wake marehemu mke wangu?

Waungwana nisaidieni, kama mke wangu amefariki na kaniachia watoto wawili bado wadogo, mdogo wa mke wangu akaja kunisaidia kwa muds kuangalia watoto, ikatokea tukapendana na tunahaja ya kufunga ndoa, je imekaaje hii wa jameni?

oa mjukuu wangu..na siku ya harusi nialike nije kutia fatihaah kidogo
 
najua yakua mmefanya matusi na inategemeana ni jinsi gani mlivo kubaliana ibnawezekana mlitamaniana tu lakini haijalishi kuwa uwe unampenda sababu ya wanao bali upendo wako utoke moyoni mwako na si hivyo tu bali pia Muheshimu mungu funga ndo ili hata wanao wawe kwenye safe side na hata marehem huko aliko atafurahi ila endapo tu kifo chake hakikua cha utata
valex
 
Hata kama kaanza kula baada ya kifo ina maana walikuwa wanatakamaniana tangu zamani, it was just a matter of time and space.

Ila hapa mimi nasema inategemea jinsi ambavyo upande wa mke watavyoichukulia, na pia na mila zao zinasemaje. Kuna dada mmoja mwenye asili ya Kusini mwa Tanzania aliwahi kuniambia kwamba, huko kwao endapo mwanaume atakwenda ukweni halafu akakuta mkewe hayupo labda amekwenda kijiji cha jirani (kumbuka enzi hizo hakukuwa na simu) basi mwanaume huyo hupewa mdogo wake na mkewe kwa usiku huo alale naye mpaka kesho yake mkewe akirudi.

Sasa kwa mila kama hizo kuoa mdogo mtu wala haina shida!

Kwa upande wangu nachukulia kuwa suala la kuoa/kuolewa ni la kibinafsi zaidi. Kwa hiyo kama wao wamekubaliana hakuna neno. Ila pia inabidi kuangalia mila. Kwa sababu wanandoa wanaishi katika jamii na kuna vitu ambavyo wanajamii hawategemei kuviona. Kama mila zao zinaruhusu basi hakuna neno.

Jambo moja ambalo linatia shaka kwa ndugu wa upande wa marehemu na wengineo (hata mimi) ni suala la muda toka msiba ulipotokea. Kama jamaa alipoteza mke miezi 9 iliyopita na sasa anataka kuoa, tena shemeji yake basi hapo kuna tatizo. Ina maana hakupata hata muda wa kuomboleza kifo cha mke wake kwa sababu alikuwa anatumbua na shemeji. Kuna maswali mengi hapo!
 
Kwa kawaida ya masuala ya mapenzi, mtu huja kutaka ushauri baada ya kuwa amependa kupindukia!...Anauliza huku akitegemea positive responce tu!...Hapa, kisheria hakuna utata, ila kijamii, inategemeana na koo zenu, na mila na dasturi za kwenu!..Kwetu hakuna kitu kama hicho...Hata kama ulishalamba ndo mwisho hapohapo!
 
Hilo ni suala la muhimu mkuu,

Kwetu kulikuwa hakuna neno kabisa na walikuwa wanashawishi watu wafanye hivyo kabla ya haya mambo ya Ukimwi. Kuna babu mmoja alioa mtu na mdogo wake na hata watoto walikuwa wananyonya kwa mama yeyote.
 
kwa kawida mi sioni tatizo. but tukiingia kwenye imani ya dini, hasa yakikristo
it is forbiden.
 
Are theuy sure that they real love each other? Isijekuwa ni upweke tu wa kuishi nchi za watu umewafanya waanze kubanjuana! Wakishaoana wanaweza kuja kugundua kwamba hayakuwa mapenzi, ila tamaa ya kutimiza haja zao za ngono!

Kijana wa kiume anaishi UK na mwanamke anaishi Bongo. Hata kama wote wangekuwa wanaishi ughaibuni mapenzi yanashamiri popote pale na kama kijana katangaza nia yake ya kuoa basi wanapendana. Kama ingekuwa kutimiza ngono tu sidhani kama hawa vijana wangeamua kufuatilia kwa wakubwa wa pande zote mbili zinazohusika kuulizia kama wakiamua kuoana kutakuwa na matatizo. Wangeendelea kumegana kimya kimya.
 
Are theuy sure that they real love each other? Isijekuwa ni upweke tu wa kuishi nchi za watu umewafanya waanze kubanjuana! Wakishaoana wanaweza kuja kugundua kwamba hayakuwa mapenzi, ila tamaa ya kutimiza haja zao za ngono!
Masaki~~~..hili nalo neno
Wajua huku nje bana dah...sometimes unakuwa unapembua chuya kutafuta mchele badala ya kupembua mchele kutafuta chuya,hatimaye unakuta chuya iliyochunika kidogo ukaanza kusisitiza kuwa ni mchele...baadae ukirudi ukirudi Bongo ndio waja gundua kuwa ile ni chuya tu bali ilikuwa ni afadhali kuliko chuya zingine.
Kwa hiyo ni sahihi kuuliza kama kweli kuna true n sincere love..asije mshikaji akarudi Bongo,akaona varieties ya Bantu figures ambazo zilikuwa out of his visual field kwa muda mrefu akaanza kujuta.
 
...aaaaaaaaaaah bana, umeanza vizuuuuuri halafu huku mwisho unaanza kuharibu. Be responsible bana, kama ni wewe tukujibu wewe...ukisema ni jamaa yako utaulizwa msimamo wako. Anyway,...

Mimi, ningewapa somo Nia, Sababu na Uwezo wa kumuoa mdogo mtu.
Mazingira ya kifo yapo wazi, huwezi wapendezesha ndugu wote, jali lililo na faida kwako,...
Bi mdogo na watoto wenu.

Kwakweli nimecheka sana, hata mimi nimemstukia ni yeye mara aseme si yeye. Muoe haina neno, ila una TABIA MBAYA SANA, kutembea na mdogo wa mkeo wakati mkeo alikuwa hai. Na ndiyo chanzo cha ndugu zake kukukataa manake wanajua utamuuwa ndugu yao na mambo yako ya Uzinifu. Umeboa sana wewe, na huyo mkeo mtarajiwa ategemee utam cheat hivyo hivyo na mdogo wake mwingine na hausigeli, na wengineo, Lol!!!
 
Mkuu isikuumize sana kichwa kama ni mimi au la, ni namna tu ya kuwasilisha hoja, eidha ni mimi au la point yangu ilikuwa ni rukhusa?,
By the way nashukuru kwa ushauri wako, ingawa umeuwa sana mkuu, hata hivyo uhusiano ulianza baada ya mkewe kufariki
 
Ruksa mkuu, tena muoane haraka iwezekanavyo. Suala la msingi ni kwamba mnapendana na hakuna kizuizi katika hilo. Mdogo wa marehemu anaelewa vizuri mazingira aliyokuwemo dadake tofauti na kuoa mtu baki.
 
Kwa upande wangu sioni tatizo la swali kama hili ni zuri sana tu na sijui wapi panaonyesha tunaelekea kubaya kwenye swali hili....

Mkuu thanx for your comment, Avatar yako inanikumbusha enzi hizo sikosi jarida la Sani
 
Mkuu point noted,
kama nilivyoeleza awali, jamaa anaishi Dar na kunawakati mdogo wa mkewe alitoka kwao Moro na kufikia kwa jamaa kwa mada wa miaka 2 akisoma kisha akarudi Moro, Baada ya kifo ndungu zake wenyewe wakamwambia aje kumsaidia huose girl wa mshkaji kusimamia watoto kwa muda hadi hapo atakapo kaa sawa. Ndani ya miezi tisa aliyokaa pale wakaanza kamchezo kachafu, baadae wakaamua wfanye kweli ndipo balaa likaanza hapo,
wanahisi tu kuwa pengine jamaa alikua anakula toka zamani ndio maana.
Hata hivyo nadhani point ya kutumia wazee wa busara ninzuri pia maana jamaa kakolea sana
kama washabanjuana mimi naona waachwe tu waoane, it doesnt make any sense kuwakataza coz for sure wataendelea tu kula tunda. bora aende alee watoto wa dada ake kwa upendo kupunguza headache za mama wa kambo wa ukweli.
 
Usimuonje kwanza.........kapime maana hujasema mkeo kafaje.....tahadhari tu,isije ikawa ni ''kanyesha'' halafu utamwambukiza na huyo binti....ukipima na kukuta umekwaa ni vema usimguse huyo binti ili wanao wapate mtu wa kuwaangalia utakapokuwa haupo tena...usichukie lakini ni mwawzo yangu tu
 
Hata kama kaanza kula baada ya kifo ina maana walikuwa wanatakamaniana tangu zamani, it was just a matter of time and space.

Ila hapa mimi nasema inategemea jinsi ambavyo upande wa mke watavyoichukulia, na pia na mila zao zinasemaje. Kuna dada mmoja mwenye asili ya Kusini mwa Tanzania aliwahi kuniambia kwamba, huko kwao endapo mwanaume atakwenda ukweni halafu akakuta mkewe hayupo labda amekwenda kijiji cha jirani (kumbuka enzi hizo hakukuwa na simu) basi mwanaume huyo hupewa mdogo wake na mkewe kwa usiku huo alale naye mpaka kesho yake mkewe akirudi.

Sasa kwa mila kama hizo kuoa mdogo mtu wala haina shida!
usikute huko alikoenda ameenda kumegwa wanakupa ili usifikirie vibaya watu wa zamani walikuwa wajanja sana kulinda ndoa
 
Ruksa mkuu, tena muoane haraka iwezekanavyo. Suala la msingi ni kwamba mnapendana na hakuna kizuizi katika hilo. Mdogo wa marehemu anaelewa vizuri mazingira aliyokuwemo dadake tofauti na kuoa mtu baki.
kizuizi kipo ni kwamba ndugu hawataki huwezi kuoa bila baraka za ndugu/wazazi au walezi ndio maana ameomba ushauri na kama wakwe hawataki achana na huyo binti tafuta mke mwingine dunia imejaa wanawake kibao kuwa ndg wala sio kisingizio kuwa atalea watoto vizuri lile suala la kulea linatoka moyoni unaweza kuoa yoyote na akalea watoto vizuri au laa

achana na huyo m/mke tafuta mwingine uoe hapo hakuna tofauti na kuoa HG
 
Mkuu kwani kuoa HG ni noma, mbona kuna watu wameoa HG na wanaishi vizuri tu
 
Back
Top Bottom