Je, ni sahihi Steven Mbazi kusimamia mali za Bilionea? Tumpe ushauri DC Jerry Muro katika utatuzi wa sakata hili la mali

Marias

Member
Apr 6, 2018
61
158
Umofia kwenuuu wanabodi!

Awali ya yote ningependa sana kumpongeza Dc Jerry Muro kwa jitihada zake za kuingilia Kati sakata hili la mali za marehemu .Naomba tuutumie uzi huu kama njia ya kumpa ushauri mheshimiwa DC wa namna ya kushighulika na sakata hili!

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana hili sakata la bilionea Msuya, lakini nimeshtushwa kumbe hatimaye kwa miaka hii ambayo mke wa erasto yupo gerezani mali zimekuwa zikisimamiwa na kaka wa mwanamke huyo!

Nimejaribu kuestablish in summary vitu vichache ambavyo vitarahisisha katika kutoa ushauri:-

1. Bilionea Msuya alikuwa mfanyabiashara wa madini aliyeuwawa kwa kimiminiwa risasi maeneo karibu na KIA miaka ya 2013, wauaji walikamatwa na kuhukumiwa kunyongwa.

2. Dada wa bilionea Msuya kwa majina ya Anathe Msuya aliuwawa mwaka 2016 nyumbani kwake Kigamboni. Alichinjwa na wauaji walikamatwa ambapo mmoja wao ni mke wa marehemu bilionea Msuya kwa majina ya Miriam Mrita. Mke huyu wa marehemu Erasto Msuya alikiri kuhusika katika mauaji ya wifi yake kwa madai kuwa alikuwa anamtukana na kumtumia picha za wanawake wenye maumbo makubwa kwa kumkebehi (nadhani walilumbana kuhusu mali pia) kesi inaendelea na mke yupo Segerea.

3. Wazazi wa marehemu Erasto Msuya wote wawili wako hai na inasemekana bilionea huyu utajiri wake aliupata kutoka kwa wazazi ikiwepo kupewa mali kama kitalu cha mgodi na hoteli ya SG etc etc.


4. Marehemu Erasto Msuya aliacha watoto wanne ambapo mtoto wa kwanza kwa majina ya Kelvin ana umri wa miaka 23 kwa Sasa! (Kwa mtoto wa kiume wa familia ya kitajiri ndo muda wa kula bata kama zote)


5. kikao cha familia kilimteua Miriam Mrita kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu Erasto Msuya, na baadaye alipokamatwa kwa tuhuma za mauaji ya wifi yake alimteua ndugu yake Steven Mbazi kuwa msimamizi wa mali hizo bila kuhusisha wahusika wote wa mirathi ya Erasto.


6. Mjomba Mbazi analalamika ndugu wa Erasto wanamtishia maisha, mjomba Mbazi ndo anasimamia SG Hotel, Mjomba Mbazi amekataa kumlipia ada Glory mtoto wa Erasto anayeishi Canada kwa madai kwamba hajatuma matokeo.

7. Mtoto wa marehemu Kelvin alitokea mbele ya vyombo vya habari mapema wiki iliyopita akiomba msaada wa Rais Magufuli kuingilia kati sakata hilo kwani wanateseka, alitoka mbele ya vyombo vya habari akiwa na mjomba wake ambaye ni Mbazi huku akiwa na vielelezo vya RB alizochukua baada ya kutishiwa na ndugu wa Erasto.

8. Ndugu wa Erasto wanacholalamika ni namna mali za kaka yao zinavyotapanywa na ndugu hao wa mwanamke. Inasemekana mwanzo walikuwa wanafika kwenye nyumba aliyokuwa akiishi marehemu na mkewe na wanatoka na bahasha, lakini pia licha ya kuwa wao wanasimamia mali, bado hawawezi ata kuwalipia ada watoto na ndugu wanapolalamika wanaushia kutukanwa! Wanasisitiza hawahitaji mali ila hawataki zichezewe na ndugu wa mke sababu baadae watoto watateseka! Na wanafanya kwa upendo.

9. Kelvin amesikika leo wakisema anajua ni ndugu wapi wana upendo na wao watoto, akasema ndugu wa mama ndiho wana upendo nao na siyo ndugu wa baba, kama ndugu wa baba wanaupendo wanaousema basi wawe na upendo na mama yake pia aliye gerezani (salaleeeee hapa dogo kasahau kuwa mama yake kamuua ndugu yao?🤷🏼‍♀️)

10. Chini ya DC Muro leo wamekubaliana kuondoa mashauri yote yaliyo mahakamani ili wasuluhishe jambo hili la mali za marehemu nje yamahakama!

Naomba niishie hapa. Kwa niliyosahau, wengine mtaongezea. Tushushe ushauri hapa kusaidia jambo hili kuisha salama.
 
Dogo kalishwa matangopori na mjomba, kisasi cha dogo ukiangalia kwa makini ni juu ya kesi ya mama yake kushikiliwa kidedea na ndugu wa upande wa baba..... Kwa 80% mali zina milikiwa na upande wa mama ambapo ndio upande dogo alipo egemea...

Mjomba nasikia kaporomosha jumba la ghorofa hapo sakina kwa hela anazo chuma hapo hotelin
 
Dogo kalishwa matangopori na mjomba, kisasi cha dogo ukiangalia kwa makini ni juu ya kesi ya mama yake kushikiliwa kidedea na ndugu wa upande wa baba..... Kwa 80% mali zina milikiwa na upande wa mama ambapo ndio upande dogo alipo egemea...

Mjomba nasikia kaporomosha jumba la ghorofa hapo sakina kwa hela anazo chuma hapo hotelin
Baada ya miaka kadhaa ndo dogo ataelewa kelele za mashangazi zina maana gani
 
Dogo kalishwa matangopori na mjomba, kisasi cha dogo ukiangalia kwa makini ni juu ya kesi ya mama yake kushikiliwa kidedea na ndugu wa upande wa baba..... Kwa 80% mali zina milikiwa na upande wa mama ambapo ndio upande dogo alipo egemea...

Mjomba nasikia kaporomosha jumba la ghorofa hapo sakina kwa hela anazo chuma hapo hotelin

du hatari sana.
 
Kwa familia za kiafrika ubilionea ni laana,nadhani tunakumbuka tunzi nyingi kuhusu wana ndugu wanapogombania mali,hapo kenya familia za kitajiri ambazo wenyewe wamefariki zimeacha magomvi makubwa kati ya wanandungu na kubaki hizo mali zikiliwa na wapambe,kuna familia za Karume,Kirimi,Michuki na wengineo hadi sasa wanashinda mahakamani huku mali za mamilioni ya pesa zikiwa zinaharibika na nyingi kuibiwa na wajanja. Wakati mwingine naona aheri umasikini kwani hausumbuliwi na yeyote kuliko huo utajiri unaleta mifarakano
 
Back
Top Bottom