Je, ni sahihi kuruhusu wajinga wengi kuchagua viongozi au wachache wenye akili kufanya hivyo?

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,016
12,302
Ipi ni njia bora ya kupata waliobora ?

Je, ni kuruhusu wajinga wengi wasiojua chochote kuhusu masuala ya siasa na maendeleo kuchagua viongozi?

Au watu wachache/ kijikundi kidogo kijuacho kuhusu siasa na maendeleo kuchagulia watu uongozi makini wa nchi?

Demokrasia ya wengi wape hata kama ni kundi la wajinga na wapumbavu limeamua ina afya kwa taifa au upuuzi ?

Kwa kutumia mtazamo wa kidunia sio kitaifa pekee.
 
Bahati mbaya Mungu hakunyimi vyote. Wajinga wamenyimwa akili, ila wamejaliwa ujasiri. Na ndiyo maana hawa watu huwa wanajiamini sana.

Wakati watu wenye akili/werevu wakiamua kukaa pembeni na kujitenga dhidi ya mambo kama hayo ya kupiga kura, kushiriki kwenye siasa, nk! Hao wajinga utawakuta mstari wa mbele!!
 
Na ndiyo wanatuamulia mambo kila siku
 
Wewe una akili?
 
Kwani Tanzania kuna Uchaguzi? Au kuteuana?
 
Ipi ni njia bora ya kupata waliobora ?

Je, ni kuruhusu wajinga wengi wasiojua chochote kuhusu masuala ya siasa na maendeleo kuchagua viongozi?

Au watu wachache/ kijikundi kidogo kijuacho kuhusu siasa na maendeleo kuchagulia watu uongozi makini wa nchi?

Demokrasia ya wengi wape hata kama ni kundi la wajinga na wapumbavu limeamua ina afya kwa taifa au upuuzi ?

Kwa kutumia mtazamo wa kidunia sio kitaifa pekee.
"Changamoto kubwa iliyopo katika ulimwengu wa sasa ni kwamba, watu wenye akili nzuri hawataki kujihusisha na Siasa, hivyo, watu wasiokuwa na akili wamepewa mamlaka ya kuwatawala watu wenye akili na watu wasiokuwa na akili."
Donald Trump, aliyekuwa Rais wa Marekani.
 
Ni jambo nzuri endapo sheria itapita kwamba mpiga kura na mpigiwa kura wote wawe na elimu kuanzia degree moja. Hapo utapata kundi maalum la wasomi ambao wanaweza kupembua uongo wa wanasiasa na wakafanya uamuzi sahihi kwenye sanduku la kura.
 
Ipi ni njia bora ya kupata waliobora ?

Je, ni kuruhusu wajinga wengi wasiojua chochote kuhusu masuala ya siasa na maendeleo kuchagua viongozi?

Au watu wachache/ kijikundi kidogo kijuacho kuhusu siasa na maendeleo kuchagulia watu uongozi makini wa nchi?

Demokrasia ya wengi wape hata kama ni kundi la wajinga na wapumbavu limeamua ina afya kwa taifa au upuuzi ?

Kwa kutumia mtazamo wa kidunia sio kitaifa pekee.
Si sahihi kuruhusu wajinga kuchagua kiongozi ila changamoto ni vigezo na nani wa kuamua yupi ni mjinga na yupi ana akili.
 
Bahati mbaya Mungu hakunyimi vyote. Wajinga wamenyimwa akili, ila wamejaliwa ujasiri. Na ndiyo maana hawa watu huwa wanajiamini sana.

Wakati watu wenye akili/werevu wakiamua kukaa pembeni na kujitenga dhidi ya mambo kama hayo ya kupiga kura, kushiriki kwenye siasa, nk! Hao wajinga utawakuta mstari wa mbele!!

Ujasiri without vision ni empty, ni kama power bila control. Una ujasiri yes but huo ujasiri unakusuma sehem sahihi au ujasiri kwenye ujinga?
 
Hii mada ni muhimu sana.

Kama ambavyo si wote wanaingia bungeni, hivyohivyo inabidi iwe SI WOTE wanaochagua viongozi.

Hiyo kazi inabidi tuidelegate kwa watu wachache sana waaminifu, wenye hekima, wenye maadili mazuri, Watusaidie kupata viongozi. Nje ya hapo mambo ya uchaguzi ni ushabiki kama ulivyo ushabiki mwingine kama vile mpira.
 
Ipi ni njia bora ya kupata waliobora ?

Je, ni kuruhusu wajinga wengi wasiojua chochote kuhusu masuala ya siasa na maendeleo kuchagua viongozi?

Au watu wachache/ kijikundi kidogo kijuacho kuhusu siasa na maendeleo kuchagulia watu uongozi makini wa nchi?

Demokrasia ya wengi wape hata kama ni kundi la wajinga na wapumbavu limeamua ina afya kwa taifa au upuuzi ?

Kwa kutumia mtazamo wa kidunia sio kitaifa pekee.
Nadhani nzuri iwe management by objectives..... yaani majukumu yaainishwe then viongozi (bila kujali chama) waombe nafasi ya urais then kamati ya bunge ifanye consensus (sio kupiga kura) na kumchagua mmoja kuwa Rais/executive prime minister wa nchi.

NB: Najua tyranny of numbers bungeni itaharibu mchakato but at least watakua na uwezo wa kumng'oa akizingua maana sheria zitakua wazi nini kifanyike asipofikia malengo.

So KPI ndio inakua measured na CAG against kila bajeti ya mwaka, ukifeli unaondoka. Ingekua hivyo tungepunguza wagombea na wangekua serious kidogo ila hii style ya miaka 5 alafu unapigiwa kura na wajinga wasiojua hata ilani imeahidi nini hatuwezi toboa.
 
Tatizo ni kwamba bungeni kwenyewe kuna vilaza wengi tu, sio jambo rahisi sana.
 
Hii mada ni muhimu sana.

Kama ambavyo si wote wanaingia bungeni, hivyohivyo inabidi iwe SI WOTE wanaochagua viongozi.

Hiyo kazi inabidi tuidelegate kwa watu wachache sana waaminifu, wenye hekima, wenye maadili mazuri, Watusaidie kupata viongozi. Nje ya hapo mambo ta uchaguzi ni ushabiki kama ulivyo ushabiki mwingine jama vile mpira.
Tume ya Warioba ilikuwa hivyo lakini jambo lake halikufika popote, liliishia njiani na kuvurugika kabisa.
 
Bila shaka unaongea kuhusu wapiga kura. Basi hilo wazo lako ni dhana potofu sana (fallacy).

Kwanza ni kina nani hao nchini wenye mamlaka ya kujua na kuamua wananchi wepi wenye akili na wepi ni wajinga wasiruhusiwe kushiriki kuchagua viongozi?

Vigezo vya kuamua wajinga na wenye akili vinaainishwaje na ni kina nani nchini wenye ujuzi usiohojika wa kuweka vigezo hivyo?

Tukijibu hayo maswali kwa utimilifu bila shaka tutajua uwezekano wa kuwa na “kikundi cha weledi wachache” kuchagua viongozi badala ya “wajinga wengi” kuhusishwa.

Aidha, tujifunze kwenye historia ya Ugiriki na Marekani (USA) jinsi walivyosumbuka kupata mfumo wa utawala sahihi kuwakilisha maslahi ya wananchi wote. Vile vile tupitie harakati za kina Lenin walioamini katika wachache wenye “mwanga” (the vanguard) kuongoza maslahi ya wengi.

Ndivyo itikadi kuu za demokrasia na ukomunisti zilivyozaliwa.

Pendekezo la “wenye akili wachache” kuchagua viongozi linawezekana tu kwenye mfumo wa kikomunisti wa chama kimoja cha siasa, in fact chama dola kinachohodhi mamlaka ya kuongoza nchi.

Haiwezekani, kwenye mfumo wa demokrasia ya vyama vingi kuwa na “vanguard party”. Labda kinafiki.
 
Sio sahihi,ndo maana kuna nchi zilibadilisha utaratibu wa uchaguzi kutoka kwenye wengi wape hadi kwenye kiwango fulani cha asilimia.
 
Back
Top Bottom