Je, ni nani asiye na kijicho!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Ukitaka kujua kuwa wewe ni mwenye kijicho dhidi ya mafanikio au jitihada za wenzio, jiulize maswali machache yafuatayo:

Je unaposikia jirani kanunua gari, kajenga nyumba, kafungua biashara kubwa au mwanae kapata nafasi ya kusoma nje ya nchi na mengine mengi kama hayo maadamu yawe mafanikio, unajisikiaje moyoni?

Au jirani yako anapokuomba ushauri wa kuanzisha biashara, kununua shamba, gari au nyumba, unampa ushauri kwa moyo mweupe au unatoa ushauri usiofaa?

Kwa vyovyote vile, majibu ya maswali hayo hapo juu yanatosha kukujulisha iwapo una kijicho dhidi ya mafanikio ya mwenzio au la.

Hebu tusiwe wanafiki, tujifanyie tathmini ili tujijue tuko upande gani……………

Nani athubutu?
 
Nilijua tu kwamba huu uzi wadau wataukwepa maana umegonga ikulu..................
Kumbe wote tulio humu JF tuna KIJICHO eh.......................!
 
Hata ukisoma baadhi ya maoni ya wadau wanapojibu uzi humu JF utajua tu kwamba wana KIJICHO................LOL
 
acha mzee mzima nifunguke...................LOL
Naamini binadamu wote huwa tunapatwa na hisia za wivu sometimes.............................ila sasa kuna wale wenye wivu mkali kiasi kwamba wanaweza kuchukua hatua za kumkwamisha au kumdhuru yule wanaemuonea wivu........................
 
Sina wivu, sielewi even how it feels kumuonea mtu kijicho
Labda nikubali kutamani wakati mwingine na sijui kuyavuta matamanio yangu zaidi ya machoni na inaishia hapo.........
 
lol... Jibu langu huwezi amni... hii tathmin unaweza pata majibu sahihi pale tu kama ni anonymous. sio kwa njia hii...
 
Ukitaka kujua kuwa wewe ni mwenye kijicho dhidi ya mafanikio au jitihada za wenzio, jiulize maswali machache yafuatayo:

Je unaposikia jirani kanunua gari, kajenga nyumba, kafungua biashara kubwa au mwanae kapata nafasi ya kusoma nje ya nchi na mengine mengi kama hayo maadamu yawe mafanikio, unajisikiaje moyoni?

Au jirani yako anapokuomba ushauri wa kuanzisha biashara, kununua shamba, gari au nyumba, unampa ushauri kwa moyo mweupe au unatoa ushauri usiofaa?

Kwa vyovyote vile, majibu ya maswali hayo hapo juu yanatosha kukujulisha iwapo una kijicho dhidi ya mafanikio ya mwenzio au la.

Hebu tusiwe wanafiki, tujifanyie tathmini ili tujijue tuko upande gani……………

Nani athubutu?
Nilijua tu kwamba huu uzi wadau wataukwepa maana umegonga ikulu..................
Kumbe wote tulio humu JF tuna KIJICHO eh.......................!

Mtambuzi, uzi wako siyo watu wanakwepa ila mada uliyoiweka imekuwa na changamoto kwenye kuichangia. Kwa upande wangu mimi suala la kuwa na kijicho au kutokuwa na kijicho inategemea na ukaribu wa huyo mtu ambaye anamuonea kijicho/asiyemuonea kijicho mwenzie.

Kwa mfano si rahisi, mtu akigombana na mwenzake, kwa vyovyote vile, hatapenda kuona mwenzake (huyo mgomvi wake) anafanikiwa kwa yale atakayokuwa anayafanya. Hii ni nature ya binadamu na ndiyo maana kuna msemo unasema adui yako muombee njaa, na huwa hawasemi muombee mafanikio!!!

Lakini ktk hali ya kawaida, huwezi kuwa na kijicho kwa yule mtu ambaye una mahusiano naye mazuri. Kwa mfano rafiki zako, ndugu zako, jamaa zako wa karibu nk nk huwezi kuwaonea kijicho wanapofanikiwa na kama ikitokeo hivyo, basi wewe utakuwa na matatizo au una ile kitu inayoitwa ROHO MBAYA! :confused2:
 
Kwanza tuambie ww upo upande gani.
Mimi sina kijicho na ndio maana hata humu natoa ushauri mwingi tu wa namna ya kujitambua...........
Nikipata muda nitaweka makala kuelezea athari za kijicho hapa hapa JF
 
Sina wivu, sielewi even how it feels kumuonea mtu kijicho
Labda nikubali kutamani wakati mwingine na sijui kuyavuta matamanio yangu zaidi ya machoni na inaishia hapo.........
Heri wewe umekuwa mkweli wengine wenye kijicho nafsi zinawasuta, hawataweza kutia neno humu.............
 
mimi sina kijicho ila nina wivu wa matamanio ya kunisukuma nami niwe kama ama nimzidi fulani.
 
lol... Jibu langu huwezi amni... hii tathmin unaweza pata majibu sahihi pale tu kama ni anonymous. sio kwa njia hii...
Kwani wanaJF wanajuana humu? wote si tunatumia majina na yasiyo yetu.......... sasa hofu ni ya nini? nyie fungukeni tu, wala hakuna atakeyewajua, baadae nitatoa darasa hapa namna ya kuondokana na kijicho..............stay tune
 
Mtambuzi, uzi wako siyo watu wanakwepa ila mada uliyoiweka imekuwa na changamoto kwenye kuichangia. Kwa upande wangu mimi suala la kuwa na kijicho au kutokuwa na kijicho inategemea na ukaribu wa huyo mtu ambaye anamuonea kijicho/asiyemuonea kijicho mwenzie.

Kwa mfano si rahisi, mtu akigombana na mwenzake, kwa vyovyote vile, hatapenda kuona mwenzake (huyo mgomvi wake) anafanikiwa kwa yale atakayokuwa anayafanya. Hii ni nature ya binadamu na ndiyo maana kuna msemo unasema adui yako muombee njaa, na huwa hawasemi muombee mafanikio!!!

Lakini ktk hali ya kawaida, huwezi kuwa na kijicho kwa yule mtu ambaye una mahusiano naye mazuri. Kwa mfano rafiki zako, ndugu zako, jamaa zako wa karibu nk nk huwezi kuwaonea kijicho wanapofanikiwa na kama ikitokeo hivyo, basi wewe utakuwa na matatizo au una ile kitu inayoitwa ROHO MBAYA! :confused2:
Yaani umesema sahihi kabisa..........
Lakini kuna namna nzuri ya kuondokana na hiyo dhana ya "adui yako muombee njaa"
Ninaandaa makala juu namna ya kuondokana na kijicho chenye kisirani............................!
 
Heri wewe umekuwa mkweli wengine wenye kijicho nafsi zinawasuta, hawataweza kutia neno humu.............

Lakini twende mbele turudi nyuma hii staili ya kujizungumzia mwenyewe sio kabisa.........utajisagia vipi? zaidi ya kujifagilia, labda tufanye assessment kwa kila moja wetu hapa kuorodhesha mafanikio halafu tuone tuchangie vipi.......wanafiki watajulikana tu
 
Back
Top Bottom