Je, Ni kweli magereza ya Tanzania yamefikia hali hii?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,805
71,232
Katika page ya East African Radio Facebook wametaarifu kuwa wafungwa 31 wamegoma kula kwa siku kadhaa wakipinga kulazwa chumba kimoja idadi kubwa sana ya watu katika gereza la Maweni huko Tanga. Wametoa na picha ya mlindikano huo vyumbani.

Tungependa tujue jee ni kweli nchi yetu imefikia mahali magereza yetu yanaweza kulaza watu kwa namna hii kweli? Maana pamoja na wao kuwa wafungwa bado ni binadamu, pia bado nchi yetu na hasa jeshi la polisi tunashutumiwa kwa kuwa na kesi nyingi sana ambazo watu wanafungwa kwa kubambikwa, kukosa msaada wa kisheria na kushindwa kutoa hongo.

Katika jumuia ya watu waliostarabika inawezekana kweli kuruhusu hali kama hii ikatokea na hakuna hatua madhubuti za kukabiliana nayo huku tunasema tunataka kupambana na udhalimu?

Picha yenyewe ya wafungwa/mahabusu iliyowekwa na East afrika Radio ni hii hapa;
ImageUploadedByJamiiForums1453040833.890889.jpg

Mambo kama haya si yapo huko Burundi,DRC nk sasa hata kwetu pia?
 
Yap iv ndo wanavyolala jela,,mi nilikaa keko almost 2weeks ,,kwa issue ya traffic kesi,,,sero Namba NNE,bwaro la kariakoo,,,,kipindi km hiki cha joto ni balaa kabisa usiombe,,,jela hakufai kulala SAA kumi jioni ,,na kuhamka kumi na mbili asubuhi kwa kengere,,,,NILICHOPENDA KULE ASUBUI UJI WA DONA WA UKWELI,,,MCHANA DONA na maragwe,,nilirudi kifriji chote kimeisha,,,,,,ila kiukweli serikali wangefanya utaratibu wakupanua magereza,nahisi yatakuwa yamezidiwa na watu mno,,,,
 
Ulidanya kosa gani mkuu...mlishindwa kumalizana kwenye tukio?
 
Hapo haina haja ya kulala, hivi utakuwa umelala au unawaza?? Ati kijambio nyuma teh hapo ni kuangaliana mwanzo mwisho.
 
Ulidanya kosa gani mkuu...mlishindwa kumalizana kwenye tukio?

Ktk eneo la tukio jamaa tulipishana kiswahili,,nikampasua usoni,,,,siunajua mwingine ukimgonga kwa gafla,,akishuka kwenye gari anapanic na moja kwa moja anashuka ili akamchomoe ktk steering aliemsababishia accident,, sasa akujua km nami nipo fit kimtindo na gym boy kitambo ,,,
 
pole mkuu...ila nimecheka sana
 
Kuna kesi nyngine haziihitaji hata mtu kufungwa jela, waanzishe mpangilio wa kifungo cha nje kwa kesi za kipuuzi. Kesi kama za wizi wa simu, kuku, kutuchukuwa mke au mume wa mtu hazihitaji kifungo cha ndani.

Tanzania ni nchi ya ajabu sana sijui kama mahakimu watanzania kama wana akili kisawasawa
 
Katika page ya East African Radio Facebook wametaarifu kuwa wafungwa 31 wamegoma kula kwa siku kadhaa wakipinga kulazwa chumba kimoja idadi kubwa sana ya watu katika gereza la Maweni huko Tanga. Wametoa na picha ya mlindikano huo vyumbani.
Tungependa tujue jee ni kweli nchi yetu imefikia mahali magereza yetu yanaweza kulaza watu kwa namna hii kweli? Maana pamoja na wao kuwa wafungwa bado ni binadamu, pia bado nchi yetu na hasa jeshi la polisi tunashutumiwa kwa kuwa na kesi nyingi sana ambazo watu wanafungwa kwa kubambikwa, kukosa msaada wa kisheria na kushindwa kutoa hongo.
Katika jumuia ya watu waliostarabika inawezekana kweli kuruhusu hali kama hii ikatokea na hakuna hatua madhubuti za kukabiliana nayo huku tunasema tunataka kupambana na udhalimu? Picha yenyewe ya wafungwa/mahabusu iliyowekwa na East afrika Radio ni hii hapa;
View attachment 317458
Mambo kama haya si yapo huko Burundi,DRC nk sasa hata kwetu pia?
Kwa hali kama kweli ni Tanzania basi napata picha ni kwa jinsi gani mambo ya mapenzi ya jinsia moja yanashamili sana magerezani,
 
Kuna kesi nyngine haziihitaji hata mtu kufungwa jela, waanzishe mpangilio wa kifungo cha nje kwa kesi za kipuuzi. Kesi kama za wizi wa simu, kuku, kutuchukuwa mke au mume wa mtu hazihitaji kifungo cha ndani.

Tanzania ni nchi ya ajabu sana sijui kama mahakimu watanzania kama wana akili kisawasawa
Jomba cc mahakimu tunfuatisha sharia.....acha kutuita Haruna akili
 
Yap iv ndo wanavyolala jela,,mi nilikaa keko almost 2weeks ,,kwa issue ya traffic kesi,,,sero Namba NNE,bwaro la kariakoo,,,,kipindi km hiki cha joto ni balaa kabisa usiombe,,,jela hakufai kulala SAA kumi jioni ,,na kuhamka kumi na mbili asubuhi kwa kengere,,,,NILICHOPENDA KULE ASUBUI UJI WA DONA WA UKWELI,,,MCHANA DONA na maragwe,,nilirudi kifriji chote kimeisha,,,,,,ila kiukweli serikali wangefanya utaratibu wakupanua magereza,nahisi yatakuwa yamezidiwa na watu mno,,,,

Hukupaswa kukaa ndani uliisababishia serikali hasara msosi, ulilipa faini?
 
Hyu Kitwanga anakimbizana na boda boda anaacha kuangalia mambo ya msingi kuna haja yakuteua wendawazimu kuwa mawaziri
 
Mkubwa hiyo picha sio tz bhana, hao wawili walio karibu tungeona ndui zao.
Ni picha waliyoitumia kwenye habari yao ya gereza la Maweni Tanga.
Hata hivyo kama sio lakini kama watu wamagoma kula it means hali ni mbaya sana. Jee serikali yetu inajitihada za kuboresha magereza yetu?
Imagine MTU unapelekwa huko kwa kubambikiwa kosa ambalo hujafanya,jee ukitoka huko utakuwa raia mwema kama ulivyokuwa awali au utakuwa mtu wa visasi?
 
Dah kunawatu wanateseka dunian yani bora ufe tu hamna haja ya kuishi. Umaskin ni kitu kibaya sana.
 
Na hayo ya kukata tamaa ndiyo yanasababisha watu kufikia hata kujifunga mabomu mkuu, ogopa mtu anayeona hana cha kupoteza
 
Ktk eneo la tukio jamaa tulipishana kiswahili,,nikampasua usoni,,,,siunajua mwingine ukimgonga kwa gafla,,akishuka kwenye gari anapanic na moja kwa moja anashuka ili akamchomoe ktk steering aliemsababishia accident,, sasa akujua km nami nipo fit kimtindo na gym boy kitambo ,,,
Duh, Pole. Hasira hasara. Sasa umejifunza chochote kwa tukio lako la kupigana?
 
Back
Top Bottom