Je! Ni halali polisi kuwanyima panyaroad dhamana na kukataza wazazi kuwaona?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,903
nimesikia hiyo habari asubuhi hii. je ni halali hayo? naona kuna watu wanataka kucompansate incompetence yao kwa njia za kionezi. dhamana si haki! mtuhumiwa kutembelewa na ndugu si haki? nasikia wengine hata miaka 18 hawajafika. wanasheria imekaaje hii ishu?
 
hii ndio tz bana, waliopiga pesa za epa, richmond, iptl escrow, tanesco wanapeta mpaka leo, tizama nchi miundo mbinu ndio sifuri kabisa, ndege inayowakilisha taifa hatuna, halafu panya road wanafungwa waliochota pesa ya nchi mpaka nchi inatetereka wanapeta tu, hii nchi mkwere kaiharibu haribu yote, miaka 10 sijaona lolote, halafu anawachekea tu mie nina wasiwasi huyu mkwere yumo tu
 
Mwizi Wa Kuku Nyundo Mbili Jela.Escrow Wanajiuzulu Hela Waharudishi Na Wala Hawana Kesi Ya Kujibu.Ishakuwa Kama Mchezo Wanaiba Then Wanajiuzulu.Tanzania The Beautiful Country Wonder Shall Never End!
 
nimesikia hiyo habari asubuhi hii. je ni halali hayo? naona kuna watu wanataka kucompansate incompetence yao kwa njia za kionezi. dhamana si haki! mtuhumiwa kutembelewa na ndugu si haki? nasikia wengine hata miaka 18 hawajafika. wanasheria imekaaje hii ishu?

Ndio DPP anaweza kutoa hati ya kuzuia dhamana kwa mkosaji yeyote, hiyo ni kwa mujibu wa sheria ya muenendo wa makosa ya jinai.
 
hapo hakuna haki na utaratibu wanaoutumia ni mbovu. kama taarifa ya habari juzi ilivyoonyesha. kuna baadhi ambao hawahusiki, ni jambo lisiloingia akilini kuwa umekamata watu 500 ndani ya siku mbili kwa kesi moja. kwani baada ya wale wawili kukamatwa naimani wengine wameshaondoka dar. nashangaa kova kuwatuhumi hata wasiohusika. kuna uonevu mkubwa kwa ajili ya sifa za kijinga
 
je wakili anaweza kuchallenge uamuzi wa DPP?.na vipi kukatalia wazazi kuwaona?
 
hapo hakuna haki na utaratibu wanaoutumia ni mbovu. kama taarifa ya habari juzi ilivyoonyesha. kuna baadhi ambao hawahusiki, ni jambo lisiloingia akilini kuwa umekamata watu 500 ndani ya siku mbili kwa kesi moja. kwani baada ya wale wawili kukamatwa naimani wengine wameshaondoka dar. nashangaa kova kuwatuhumi hata wasiohusika. kuna uonevu mkubwa kwa ajili ya sifa za kijinga
atafanya mambo kwa jazba na kuvunja sheria maana reputation yake ipo under test. mi nawashauri wazazi hasa wenye watoto under 18 waende kuhakikisha haki za wanao zinapatikana. wakatafute msaada kwa watu wa haki za binadamu.
 
Unaongea hivi kwa sababu hujakutana nao!! Ungesikiliza kipindi cha uchunguzi kamili mwaka jana juu ya hao watoto ungebadili msimamo. Kulikuwa na watu waliokuwa wanawajua hao watoto "maana ni watoto wetu wa mtaani na tunawajua, ila tulijuwa hawatatudhuru maana wanatujua" Ndiyo yalikuwa maneo yao. Lakini picha iligeuka pale watoto hao walipowadhuru. Hao watoto ni hatari. Ila panya road ni "symptom of the problem itself". Panya road imezalishwa na mfumo wa serikali uliopo usio wapa fursa watoto na vijana kuendelea katika nchi yao. Wale watoto wa mtaani wanaoomba kuosha vioo vya magari badala ya kuwa shule au nyumbani kwa wazazi wao wakipata malezi stahiki, vijana wanaokaa vijiweni badala ya kujishughulisha na shughuli mbadala ya kiuchumi ndiyo imezaa panya road. Frustration zao za maisha ndizo zimepelekea wao kujichukulia maamuzi mabovu. Serikali yetu ingekuwa na mipango mizuri ya kulea vijana hawa yote haya yasingekuwepo. Mbona huko nyuma makundi haya hayakuwepo? Kuwakamata bila kuwa na utaratibu wa kumaliza tatizo hili la ajira kwa vijana na shule kwa watoto wote plus kuhakikisha wanapata malezi stahiki panya road haitaisha. Serikali lazima ifanya zaidi kuliko kuishia kukamata tu. Ila wakifanya uhalifu lazima wakamatwe, na sheria ichukue mkondo wake. Hao wazazi kama ni kweli wanakatazwa kuwaona ina maana wapo, nashauri wachukuliwe hatua kwa kushindwa kuwapa watoto malezi stahiki. Malezi mazuri ni haki ya kila mtoto.
nimesikia hiyo habari asubuhi hii. je ni halali hayo? naona kuna watu wanataka kucompansate incompetence yao kwa njia za kionezi. dhamana si haki! mtuhumiwa kutembelewa na ndugu si haki? nasikia wengine hata miaka 18 hawajafika. wanasheria imekaaje hii ishu?
 
Hao wazazi walikuwa wapi hadi mitoto midogo inakuwa miuaji? Walishawashindwa watoto wao.
ukienda hivyo utakuta wakulaumiwa ni serikali. kwa mantiki hiyo serikali haitakiwi kuwakamata kwa sababu haijakuza uchumi ili kutengeneza ajira na kusababisha vijana kuwa panyaroad.
 
Unaongea hivi kwa sababu hujakutana nao!! Ungesikiliza kipindi cha uchunguzi kamili mwaka jana juu ya hao watoto ungebadili msimamo. Kulikuwa na watu waliokuwa wanawajua hao watoto "maana ni watoto wetu wa mtaani na tunawajua, ila tulijuwa hawatatudhuru maana wanatujua" Ndiyo yalikuwa maneo yao. Lakini picha iligeuka pale watoto hao walipowadhuru. Hao watoto ni hatari. Ila panya road ni "symptom of the problem itself". Panya road imezalishwa na mfumo wa serikali uliopo usio wapa fursa watoto na vijana kuendelea katika nchi yao. Wale watoto wa mtaani wanaoomba kuosha vioo vya magari badala ya kuwa shule au nyumbani kwa wazazi wao wakipata malezi stahiki, vijana wanaokaa vijiweni badala ya kujishughulisha na shughuli mbadala ya kiuchumi ndiyo imezaa panya road. Frustration zao za maisha ndizo zimepelekea wao kujichukulia maamuzi mabovu. Serikali yetu ingekuwa na mipango mizuri ya kulea vijana hawa yote haya yasingekuwepo. Mbona huko nyuma makundi haya hayakuwepo? Kuwakamata bila kuwa na utaratibu wa kumaliza tatizo hili la ajira kwa vijana na shule kwa watoto wote plus kuhakikisha wanapata malezi stahiki panya road haitaisha. Serikali lazima ifanya zaidi kuliko kuishia kukamata tu. Ila wakifanya uhalifu lazima wakamatwe, na sheria ichukue mkondo wake. Hao wazazi kama ni kweli wanakatazwa kuwaona ina maana wapo, nashauri wachukuliwe hatua kwa kushindwa kuwapa watoto malezi stahiki. Malezi mazuri ni haki ya kila mtoto.
sijakataa kukamatwa ila sioni kama ni sawa kuwanyima haki ya dhamana na kutembelewa. unakumbuka ditopile mzuzuri aliua na dhamana alipat!?. wazazi sioni kosa lao na wana haki ya kuona watoto wao. kuhusu seerikali umeongea point nzuri.
 
Asee,hivi kweli mkuu wa JF unatetea mhalifu?Yaani hao watoto hata shetani hataki kuwaona sembuse sisi?Wakae "geto" tu.
 
Je kukamata na kuwaweka ndani ndo suluhu?Je kuna miundo mbinu ipi iko in place kudhibiti panya road na pia kuna mazingira gani ya kudhibiti vichocheo vya uhalifu.

Nadhani tungeanza na Esrow the tupambane na madawa ya kulevya hapo tutakuwa tunaelekea kujenga taifa lisilo na panya road
 
Ni kweli mengi yamesemwa lakini sikubaliani na maamuzi haya. Mi nadhani hawa watoto bado ni watuhumiwa tu hivyo hawasitahili kunyimwa dhamana na kutoonana na ndugu zao. Wakati mwingine viongozi wetu hufikia uamuzi wa pupa ili waonekane ni watendaji wazuri. Hii siyo mara ya kwanza kwa kundi hili kutishia amani ya Dar es Salaam, kwa nini hakukuwa na hatua endelevu za kukomesha kikundi hiki mpaka kusubiri kilete madhara?
 
Polis ukiwauliza hawakosagi sababu za kujitetea kwa hili la kuwanyima dhamana, watasema ukiwaachia mapema utahalibu utaratibu wa upelelezi. Nadhan wakimaliza kamata kamata, wataweka swala la dhaman kuwa wazi.
 
hakuna cha haki za kisheria wala nini PANYA ROAD NI WAKUANGAMIZA KABISA/kuwatetea hawa ni zaidi ya ushenzi heri hata wezi wa ESCROW au MAJAMBAZI kuliko hawa wauni wanaokatakata watu ovyo kwa mashoka,mapanga,viwembe bila kujali watoto wazee vilema ni zaidi ya washenzi, WAPOTEZWE KABISA!/tukumbuke hao wana miaka 15~30 baada ya miaka mitano tutarajie majambazi kamili, hatari na makatili kupindukia 500
 
Back
Top Bottom