Je ni haki serikali kuwafanyia watoto hawa hivi?

Dopas

JF-Expert Member
Aug 14, 2010
1,151
392
Wana JF,

Nadhani hili wanalofanyiwa watoto hao sio haki. Kwanza hawapati elimu katika hali hii. Nadhani wana haki ya kuishitaki serikali kwa hili...hata baada ya miaka 50.
Ona tu mwenyewe hapa.
View attachment mbarali.docx
 
Inabidi hii picha ipelekwe kwy vyombo vya habari ili jamii ione jinsi serekali ya ccm inavyo watendea raia wao, akuna aki ata kidogo wakati serekali inataka kuwalipa dowans mabilioni wakati watoto wa wapigakura wanateseka. hii ndiyo maisha bora kwa kila mtanzania?
 
Inauma sana sasa hawa viongozi wanafanya ziara za kazi gani hizo pesa si wangetumia kubolesha huduma za kijamii
 
Wanafunzi wa madarasa tofauti watumia chumba kimoja Mbalali.

Friday, March 4, 2011
Na Joachim Nyambo,Mbarali
.
WANAFUNZI katika shule ya msingi Magwalisi wilayani hapa wanalazimika
kutumia chumba kimoja kwa madarasa mawili na kwa wakati mmoja kufuatia
uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa unaoikabili shule hiyo,huku walimu
wane akiwemo mwalimu mkuu wakilazimika kuishi nyumba moja yenye vyumba
vine.

Kwa uapnde wa wanafunzi madarasani kinachofanyika ni wanafunzi wa
darasa moja kuangalia upande mmoja na wa darasa linguine kuangalia
upande mwingine hivyo kilazimu chumba kimoja cha darasa kuwa na mbao
mbili za kufundishia.

Hali hiyo imebainika baada ya wanahabari walioshiriki ziara ya uongozi
wa chama cha walimu CWT mkoa wa Mbeya iliyofanyika shuleni hapo na
kujionea wanafunzi wa darasa la Nne na la Saba wakiwa kwenye chumba
kimoja na darasa la Pili na la Tatu chumba kingine huku darasa la
kwanza na wale wa darasa la awali (Chekechea) wakilundikana kwenye
chumba kimoja pia.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Jonathan Chengula alisema tangu kufunguliwa
kwa shule hiyo mwaka 2002 shule ina uhaba wa madarasa na wamelazimika
kuendelea kufundisha wanafunzi kwa mtindo huo na kufafanua kuwa
inalazimu mwalimu wa darasa moja kuingia huku wanafunzi wa darasa
linguine wakisubiri ama wakiendelea kufanya kazi waliyopewa na mwalimu
wao.

Mwalimu Chengula alisema inapobidi wanafunzi wa darasa moja hukaa
chini ya mti hususani wanaposoma vitabu ili kupisha wanafunzi wa
darasa jingine waendelee kufundishwa na mwalimu wao lengo likiwa ni
kupunguza mgongano wa walimu katika chumba kimoja.

“Hali ni kama mlivyojionea,tunalazimika kupumzisha darasa moja
humohumo ndani wakati lingine likifundishwa na mwalimu na wakati
mwingine mwalimu wa darasa moja anawatoa wanafunzi wake na kukaa chini
ya mti wakimaliza kujisomea vitabu na kupewa zoezi wanarejea darasani
kufanya kazi hiyo” alisema Mwalimu Chengula Na kuongeza
“Ni shida kubwa tunayo,walimu wenyewe sisi wane akiwemo wa kike mmoja
tunaishi kwenye nyumba moja ya vyumba vine,tulichokubaliana na mwalimu
huyo wa kike asilete mgeni wa kiume chumbani kwake wala sisi wa kiume
tusilete wageni wa kike kwenye vyumba vyetu.Tunavumilia kwakuwa
tunaipenda kazi tunaona hakuna wa kuwasaidia wanafunzi hawa”
Hata hivyo mwalimu huyo alisema hali hiyo inatokana na wakazi wa
vitongoji vya Nyaluhanga na Magwalisi kutokuwa na utayari wa kuchangia
ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu wakiamini kutokana
na kuwa wafugaji wakati wowote watahama.


Alitaja changamoto nyingine zinazoikabili shule hiyo yenye jumla ya
wanafunzi 269 kuwa ni upungufu wa madawati 71 kwakuwa yaliyopo hivi
sasa ni 60 wakati mahitaji halisi ni 131 na pia matundu ya vyoo yapo
sita huku mahitaji yakiwa ni matundu kumi na kuutaja upatikanaji wa
maji safi na salama ukiwa ni changamoto nyingine.

Wakizungumzia hali hiyo Mwenyekiti Nelusigwe Kajuni na katibu Kasuku
Bilago wa CWT mkoa wa Mbeya waliiomba serikali kuangalia uwezekano wa
kuwashawishi wakazi wa vitongoji vinavyoizunguka shule hiyo kujitoa
kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za walimu.
Walisema hali iliyopo katika shule hiyo ni changamoto kubwa inayoweza
kuathiri kiwango cha taaluma kwa wanafunzi hivyo kuna haja ya
kuboresha mazingira kwa upande wa walimu pamoja na wanafunzi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali George Kagomba
alipofuatwa ofisini kwake alisema hana nafasi ya kuzungumza na
waandishi wa habari kwakuwa alikuwa akiendesha kikao cha maandalizi
yam bio za mwenge na baadaye kikao cha kamati ya ulinzi na usalama
 
Huo ubunifu wa walimu Mbarali ni wa kusifika. Ama wanapambana haswa na upungufu wa vyumba vya madarasa.
 
Back
Top Bottom