Je mwenge ni stendi ya abiria au soko?

Oct 16, 2012
15
2
Nimekuwa nikifuatilia shughuli zinazoendelea hapa Mwenge stendi ya Daladala cha kushangaza naona hata viongozi wako kimya niliongea na kijana mmoja mfanyabiashara akiwa amebeba meza yake ya biashara kichwani akasema mbona viongozi wa manispaa wanajua maana ukitaka upate sehemu ya kuweka angalau meza yako ya biashara lazima ulipe kiingilio cha TZS 50000 na baada ya hapo kuna ushuru wa Elfu 5000 kila ijumaa ya wiki.

Sasa sijui baadaye stendi hii itafungwa na kugeuzwa kuwa soko maana sioni juhudi zozote za makusudi zikifanywa na serikali. Ina sikitisha sana kuona watu kujiamlia tu sawa biashara ni nzuri lakini basi kuwepo na ustaraabu abiria wanahangaika sana hasa nyakati za jioni huku unatafuta gari na pia uwe makini na vibaka.

Ahsanteni
 
Swali ni Zuri, Ila mwenye Jibu kamili ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni - Rugimbana, Meya wa Kinondoni na Mkurugenzi wake!! - Full siasa!!
 
Both stand na soko! kinondoni hatuna viongozi kuanzia mkuuwa wilaya na mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni!
 
Mchana stendi jioni soko usiku mahakama ya shingo wanatia kabali za kufa mtu mule ndani

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ile sehemu inakeraaaaa, hakuna utaratibu!

Halafu ajabu ni pale manispaa ya kinondoni ilipokuja na wazo la kuhamisha stendi ya Mwenge kwenda Makumbusho ili kupisha wafanyabiashara...
 
Kama nilivyosema kiingilio pale ni TZS 50000 na ushuru wa kila Ijumaa ya wiki TZS 5000 sasa hapa kweli serikali husika watatoa tamko lolote? Jamani hawa viongozi sijui wanatumia nini kufikiri
 
Nilimsikia Mkurugenzi siku moja akiseama, baada ya kutokea mzozo baina ya kigogo mmoja kuweka kontena eneo la wachuuzi, ya kwamba wanajianda kuondoa wafanyabiashara wote eneo hilo. Ila muda si mrefu itakuwa soko kamili na kiwanja cha vibaka......
 
Ni sehemu ya Tanroad, manispaa haiwezi kuweka permanent structures kwa ajili ya stendi sehemu sio ya kwao. Stendi ipo makumbusho.
That place is a road reserve.
Manispaa wanaganga njaa kama hao wafanya-biashara waliopo hapo.
 
Back
Top Bottom