Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,196
...malaya anawezaje kuwa mke wajameni?
....hamkomi tu hadi mnakuta wake zenu "vitandani" na marafiki zenu?na mnajua wazi mliwakuta wapi...!
Wee wako umemkuta bikra? Kama siyo bikra unajuaje kama alikuwa hajiuzi? Unajua definition ya kujiuza ni pana sana, na karibu sehemu kubwa ya wanawake tunaooa hivi sasa walishalala na wanaume zaidi ya kumi kabla ya kuolewa, sasa sijui huyu utamtofautisha na yule aliyeamua kujiuza rasmi.
Kumbukeni pia wapo wanaojiuza kwa shiniikizo, wapo wanaojiuza kwa kuwa maisha ni magumu na wanatafuta namna ya kupata chochote kwa ajili ya kutunza familia zao, kwa mfano namfahamu dada mmoja kutoka makete, ambaye hakuwa na baba wala mama, na aliachiwa wadogo zake wapatao watut akiwa darasa la sita tu. Hakuwa na namna ya kuwalea wadogo zake, ikamlazimu aingie kwenye kujiuza ili apate ada za wadogo zake na chakula nyumbani. Thank God hivi ninavyoongea mmoja wa mdogo wake amemaliza university (DUCE), and thank God yule dada sasa amepata mme wa maana na wanasaidiana kusomesha wadogo waliobaki ambao wengi wapo secondary.
Tuwe makini tunapotoa hukumu dhidi ya hawa watu. hakuna mwanamke mwenye akili timamu na mwenye staha anayefurahishwa na shughuli ya kujiuza. Ulizia kila mmoja utatambua ana sababu inayomfanya afanye hivyo. Vinginevyo awe ni mvuta bangi ambaye hana hata fikra juu ya maisha yake ya baadaye. Ninachokiona hapa mwanamke yeyote anafaa kuwa mke as far as ametubu na kukubali hilo jukumu la kuwa mke. Maana tukitaka kujua alikuwa anafanya nini kabla ya wewe kumpata basi unaweza kujikuta hata uliyenaye sasa alishafanya biashara ya kujiuza. maana baada ya bikra kutoka, hakuna tena ushahidi wa alishafanya ngono mara ngapi na katika mazingira yapi.