Je Mrithi wa Regia ilikuwa lazima atoke kasikazini??

Siyo ulichosikia, huo ndio utaratibu ulivyo na haujaanza leo, kumbuka hata Geturde Lwakatare aliingia bungeni baada yakifo cha Salome Mbatia, na yeye katika ile orodha jina lake ndio lilikuwa linafuatia.
Kumbe huyu Kakakiiza ni sehemu ya vilaza hapa JF? mbona hakuwahi kuhoji kwa nini mkoa wa Morogoro uwe na wabunge wa viti maalum wawili Regia Mtema na Suzan Kiwanga wakati mkoa wa Lindi hauna hata mbunge mmoja wa viti maalum!!?? huku ni kufikiri kwa kutumia kijambio.

asante mkuu, na asante wakuu wengine wote kwa kuwanyoosha hawa vilaza.
Akili wanazifungia kwenye makabati ya nguo nyumbani kwao, halafu wanakuja kusumbua watu hapa.
 
muache kulalamika, jitokezeni na mjiunge na chama hicho kwa wingi ili nafasi zenu ziwe kubwa kama hao wa Kaskazini
 
by Ibange
[h=2]
icon1.png
Tamaa Mbaya, Bi Leticia Mosore Akosa Ubunge[/h]
Katika maisha ya kisiasa hata maisha ya kawaida unapaswa kuwa na subiri. Bi Leticia Mosore ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bawacha ndie aliyeshika nafasi ya 26 na ndie alistahili kuchukua nafasi ya Regia. Kwa tamaa zake alienda NCCR kutafuta ubunge na huko hakupata, sasa analia na kusaga meno. Kwa wale wanaotaka kuwagombanisha chadema kuhusu viti maalum hawatendi haki, maana kulikuwa na utaratibu na hasa wao waliwachukua wale waliogombea na kukipigania chama maana viti maalum vinatokana na idadi ya kura za wagombea ubunge wa chama. Je, ni wanawake wangapi wa Mbeya kwa mfano walijitokeza wakanyimwa au kubaguliwa?

Nashauri uchaguzi ujao tutafute njia muafaka zaidi ili kuondoa malalamiko​

Ni kweli NEC ndiyo wenye kuteua jina kutokana na ile orodha, na hapa hakuna jinsi ya kubadilisha kama Kakakiiza anavyotaka. kwa upande mwingine CDM watakuwa angalau wamepata somo hapa, safari nyingine hawatateua au kutayarisha orodha kwa kutumia vimemo. nimeshasema sana humu, wengi wa wabunge wa viti maalumu CDM walipatikana kwa vimemo.

mkuu, hata wewe? Regia alichaguliwa kwa kimemo kipi? Au huyu ambaye atateuliwa na NEC angekuwa yule mama wa mkoa wa Mara, ambaye baada ya NEC kupiga panga kwenye 25, akaamua kuhamia NCCR mageuzi, mngesema nini?
 
muache kulalamika, jitokezeni na mjiunge na chama hicho kwa wingi ili nafasi zenu ziwe kubwa kama hao wa Kaskazini

wanataka 'wapewe' wamezoea kupewa tu....hawataki kujiunga na chama na kupambana na kuonyesha uwezo.
 
Taratibu zote zipo za kumpata viti maalum ndani ya Chadema na zimetangazwa vizuri,kipi hujaelewa au umetumwa kuja kuchonganisha.
 
Kwani Mh. Regia alikua anatokea Kaskazini? There inafter uliwahi kupitia katiba ya CHADEMA ya namna wabunge wake wa viti maalum wanapatikana? Hivi unajua NEC ina majukumu gani katika kucertify wabunge wa viti maalum wa vyama vya siasa!
 
Nimesikia mrithi wa Hayati Regia amepatikana kutoka Karatu! Je ilikuwa lazima wapitie kwenye kumbukumbu za chaguzi zilizopita?? Kwa nini hawakufanya uchaguzi mwingine ili kuleta uhalisia wa usawa kwenye chama na kuondoa dhana kuwa ni chama cha kanda ya Kaskazini??

Na ninafikiri ilikuwa vyema wangeenda Zanzibar,Mtwara,Songea,nafikiri wangepata watu wakuwakilisha viti maalumu na kuziba nafasi iliyoachwa na Regia! Hapakuwepo na uharaka kiasi hiki!

Kwani hata wiki haijaisha tangu marehemu azikwe mimi hapo nimeona kwajicho latatu nimeona kulikuwepo na upungufu!! Kwani Jambo hili limepelekwa haraka sana!
Walioanza mchakato ni tume ya uchaguzi NEC sio CHADEMA. Utaratibu ni kuwa kujaza nafasi ya mbunge wa viti maalum hufanywa na NEC kwa kuangalia aliyekuwa anafuata katika list iliyotumwa na chadema. Chadema ilipeleka majina 28 kama sikosei, yakachukuliwa wa kwanza mpaka wa 25 sasa NEC watachukua aliyekuwa wa 26 kujaza nafasi lakini kabla hawajatangaza watawataarifu chadema ili wathibitishe kama mtu huyo bado ni mwanachama. kama atakuwa sio mwanachama kwa sasa basi atachukuliwa aliyekuwa wa 27. NEC ndio wana haraka maana sio chadema walioomba mchakato wa kujaza nafasi uanze. Kuhusu dhana ya kaskazini, hilo ni propaganda ya ccm ambayo inawashika wale wenye upeo finyu. maana ktk model ya kitila mkumbo hakuna mahali waliposema mbunge wa chadema lazima awe mtu wa kaskazini. Kama watu wa kaskazini wanatimiza vigezo sioni tatizo. CCM inayofanya kazi ya kubalance uwakilishi kwa maeneo ndio inaingiza bungeni watu wajinga watu hata baadhi hawajui hata kusoma na kuandika, ccm ndiko unakoweza kupata wabunge wanajiita Prof. maji marefu na Jah people. Nadhani mnaona michango ya chadema bungeni, hiyo inatokana na vigezo vinavyotumiwa na chadema. Angalieni jinsi Regia mtema alivyokuwa akifanya kazi lakini bila shaka kama ingekuwa ccm Regia angewekwa pembeni na Leticia masore angepewa ubunge kwasababu tu ya kuwa m/kiti wa Bawacha. Na kwa cv zao huwezi kulinganisha utendaji wa Leticia na Regia, Regia was excellent. na hata wangemchukua leticia bado watu wangesema ni wa kaskazini.
 
Mchakato kutafuta mrithi wa Regia Mtema waanza
Saturday, 21 January 2012 09:22

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Regia Mtema
Aziza Masoud na Ellen Manyangu
WIKI moja tangu kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Regia Mtema kilipotokea, mchakato wa kumtafuta mrithi wa nafasi yake umeanza.

Regia alifariki dunia Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari katika eneo la Ruvu mkoani Pwani na kuzikwa Jumatano wiki hii nyumbani kwao Ifakara, mkoani Morogoro.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zinasema tayari maofisa husika ndani ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wameanza kushughulikia suala hilo la kuziba nafasi ya mbunge huyo kijana ambaye pia alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Mallaba alisema jana kwamba ofisi yake itatumia orodha ya majina yaliyopendekezwa na Chadema mwishoni mwa mwaka juzi.

“Nadhani tunayo orodha ya mapendekezo ya Chadema, basi kwa jinsi taratibu zilivyo, tutarejea katika orodha hiyo na pale tulipopitisha msitari ndipo tutakapoanzia, lakini lazima huyo anayefuata katika orodha awe na sifa za kuwa mbunge,” alisema Mallaba kupitia simu yake ya kiganjani.

Hata hivyo, Mallaba alisema hivi sasa ni mapema mno kufahamu ni lini uteuzi huo utafanyika na kwamba taratibu za ndani zikikamilika, mamlaka husika zitaarifiwa ili umma pia uweze kufahamu.

Awali, Mallaba alikataa kuonana na waandishi wa habari na mmoja wa maofisa wa Tume hiyo alisema: “Amesema majina yametoka hukohuko Chadema ndipo yakaja huku kwa hiyo kama mnayahitaji mnapaswa kwenda katika ofisi za Chadema ili muweze kupata majina hayo.”

Dk Slaa, Zitto wanena
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa alisema chama chake hakifahamu atakayechukua nafasi hiyo na kwamba hiyo inatokana na ukweli kwamba jukumu hilo liko mikononi mwa NEC.

“Majina ya wagombea wa viti maalumu yapo NEC na wao ndiyo wanaoangalia kuchagua nani anayefuata katika orodha iliyopo Tume, kwa utaratibu, mgombea anayefuata ndiye atakayechukua nafasi hiyo,” alisema Dk Slaa.

Alisema Chadema kilipeleka NEC orodha ya majina 28 ya wabunge wa viti maalumu, Desemba 30, 2010 na kati ya hayo majina 25 tayari wameshachaguliwa ni jukumu la NEC kuangalia jina gani linalofuata kwenye orodha hiyo iliyopo.

Alisema kati ya hayo majina matatu yaliyobaki yeyote atakuwa na uwezo wa kuchukua nafasi hiyo kulingana na vigezo vya NEC na kulingana na utaratibu na Katiba ya Chadema.

“Sina mamlaka ya kujua nani anayefuata na ofisini kwangu hata majina sina majina yapo NEC mimi nawategemea wao waniletee jina kwa mujibu wa taratibu zao nitaliangalia kama muhusika bado ni mwanachama hai nitawajibu na nitawarudishia na ndiyo watalitangaza kwa wananchi,” alisema Dk Slaa.

Alisema kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi, jina watakalopewa kama muhusika atakuwa amefukuzwa katika chama, basi jina litakalofuata baada ya huyo mwanachama ndilo litakaloandikwa na kufanyiwa kazi.

Alisema si rahisi kwa NEC kumtangaza mrithi wa nafasi hiyo bila kuwasiliana kwanza na chama na kuthibitisha kuwa bado ana sifa za kushika nafasi hiyo.

Alisema NEC inajua wazi kuwa haiwezi kumtangaza mtu moja kwa moja pasipo baraka za chama kwa sababu siku hizi kumekuwa na wimbi la migogoro ndani ya vyama vya siasa nchini na wengine kujivua uanachama au kufukuzwa.

Wakati Dk Slaa akisema jukumu hilo ni la NEC, Naibu Katibu wake, Zitto Kabwe alitaja jina la mmoja wa madiwani wa viti maalumu wa chama hicho kuwa ndiye anayefuata katika orodha iliyopelekwa NEC.

Akizungumza jana, Zito alisema kwa mujibu wa orodha yao ya viti maalumu anayefuata baada ya wabunge walioteuliwa mwaka juzi ni diwani huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa.

“Kwa mujibu wa orodha tuliyonayo ya wabunge wa viti maalumu anayefuata baada ya Regia ni diwani kutoka (anataja wilaya na jina lake), ndiye atakayechukua nafasi ya kiti hicho kilichoachwa na marehemu,” alisema Zitto.
Nimesikia mrithi wa Hayati Regia amepatikana kutoka Karatu! Je ilikuwa lazima wapitie kwenye kumbukumbu za chaguzi zilizopita?? Kwa nini hawakufanya uchaguzi mwingine ili kuleta uhalisia wa usawa kwenye chama na kuondoa dhana kuwa ni chama cha kanda ya Kaskazini??

Na ninafikiri ilikuwa vyema wangeenda Zanzibar,Mtwara,Songea,nafikiri wangepata watu wakuwakilisha viti maalumu na kuziba nafasi iliyoachwa na Regia! Hapakuwepo na uharaka kiasi hiki!

Kwani hata wiki haijaisha tangu marehemu azikwe mimi hapo nimeona kwajicho latatu nimeona kulikuwepo na upungufu!! Kwani Jambo hili limepelekwa haraka sana!
 
Muelewe ubunge chadema hautolewi kama mandazi tu mtu licha ya kuwa mwanamke aonyeshe uwezo basi hatuchague watu kwenda kuuza sura bungeni na kupiga mabenchi kama wabunge wa ccm wa vitimaalum.
 
Nimesikia mrithi wa Hayati Regia amepatikana kutoka Karatu! Je ilikuwa lazima wapitie kwenye kumbukumbu za chaguzi zilizopita?? Kwa nini hawakufanya uchaguzi mwingine ili kuleta uhalisia wa usawa kwenye chama na kuondoa dhana kuwa ni chama cha kanda ya Kaskazini??

Na ninafikiri ilikuwa vyema wangeenda Zanzibar,Mtwara,Songea,nafikiri wangepata watu wakuwakilisha viti maalumu na kuziba nafasi iliyoachwa na Regia! Hapakuwepo na uharaka kiasi hiki!

Kwani hata wiki haijaisha tangu marehemu azikwe mimi hapo nimeona kwajicho latatu nimeona kulikuwepo na upungufu!! Kwani Jambo hili limepelekwa haraka sana!

Sikutukani lakini ninataka ujifunze!! After a life is lost, the remaining should continue with theirs!! Ability to move and move on fast, is an important attribute of leadership. Kama utaratibu ni "anayefuata kwenye orodha", iwe ni leo au siku arobani baadae bado atakuwa ni yule yule. Taratib (rules and regulations) hazivunjwi na hisia (emotions)!! Mambo mengine yataachwa kwa familia ya Marehemu Regia, wengine tuendelee kutimiza wajibu wetu.
 
CHADEMA wanaangalia zaidi QUALITY AND NOT QUANTITY. Tulishasema hatumchagui mtu kwa kabila lake wala dini yake na hata anatokea kanda gani. hizo hazina nafasi katika dunia ya werevu. ni mawazo yetu ndo yanauona huo ukaratu but kwangu binafsi naunga mkono ubora wa mtu na si atoka wapi.
na mtu bora anaye faa CHADEMA NI MCHAGA TU
 
Nimesikia mrithi wa Hayati Regia amepatikana kutoka Karatu! Je ilikuwa lazima wapitie kwenye kumbukumbu za chaguzi zilizopita?? Kwa nini hawakufanya uchaguzi mwingine ili kuleta uhalisia wa usawa kwenye chama na kuondoa dhana kuwa ni chama cha kanda ya Kaskazini??

Na ninafikiri ilikuwa vyema wangeenda Zanzibar,Mtwara,Songea,nafikiri wangepata watu wakuwakilisha viti maalumu na kuziba nafasi iliyoachwa na Regia! Hapakuwepo na uharaka kiasi hiki!

Kwani hata wiki haijaisha tangu marehemu azikwe mimi hapo nimeona kwajicho latatu nimeona kulikuwepo na upungufu!! Kwani Jambo hili limepelekwa haraka sana!

Acheni kuangalia mtu ametoka wapi bali angalia uwezo wake.Kwani Kaskazini sio Tanzania?Halafu next time kabla hujakurupuka na ajenda ya "ukaskazini ndani ya Chadema" ni vema ukajipa tuisheni kidogo kuhusu mfumo wa upatikanaji wa wabunge wa viti maalum.

Mbona hiyo CCM iliyo na viongozi kutoka kila kona ya nchi (well,at least that seems to be what you want to hear) imetawaliwa na ufisadi kupita maelezo?Kipi bora,kiongozi atoke Zanzibar,Mtwara,Songea (as you suggested) kisha awe fisadi au atoke Kaskazini lakini autumikie umma kwa uadilifu?

Halafu mnapoleta upuuzi huu wa u-Kaskazini hamtaki kabisa kutupa mifano hai ya namna gani u-Kaskazini huo umeaithiri Chadema na Tanzania kwa ujumla.Lema,kwa mfano, anatoka Kaskazini,je ukaskazini wake umeathiri vipi medani ya ungozi ndani ya Chadema au Taifa kwa ujumla?

Kwa makusudi kabisa ni watu haohao wanaopigia ukelele juu ya u-Kaskazini wanaojaribu pia kuhoji teuzi kwa kuangalia dini ya mteuliwa.
 
Ni kweli tunaipenda chadema na tunadhan atakua mkombozi wa nchi hii lakini kama chama kinakosea lazima tuseme, sidhan kama lilikua ni jambo la busara kumteua mrithi wa mbunge aliyekua morogoro na mwingine wa mkoa mwingine tena sikufurahishwa zaidi nilipojua mrithi anatoka karatu! hii inaweza jenga picha kua chadema kinapendelea watu wa maeneno fulani, kwa mfano karatu wana mbunge wa kuchaguliwa nadhan mke wa slaa pia ni wa viti maalum sasa kulikua na haja gani ya kuongeza mwingine, nilidhan morogoro walitakiwa wapewe hiyo nafasi direct! uongozi wa chadema kwa hili mmekosea lazima mkubali hamtaeleweka mbele ya jamii inayowa support! na hatusupport chama kama wenzetu wa ccm hata chama kikisoea basi wao wanatetea tu na ndio walipotufikisha hapa!

chadema imeshajijenga north, kwa nini nafasi kama hizi wasitoe maeneo ambayo hawajajiimarisha kama uko coastal, tanga, lindi, mtwara nk ili iwe chachu ya kujenga chama maeneo hayo ktk jitihada ya kufanikisha ultimate plan ya kuchukua nchi, ila kwa mwendo huu sidhan!
 
Kaka kama hujui utaratibu kaa kimya, unaelezwa ficha upambavu wako lakini uoneshe uhodari wako. Uteuzi wa wabunge wa viti maalum haufanywi na vyama bali tume ya uchaguzi kufuatia mlolongo/orodha ya majina waliyopewa awali na vyama husika.
 
Yale majina yapo NEC ya uchaguzi tangu 2010. After Regia, jina lililofuata ni la Pareso.
CDM hawajamteua Pareso, ila tume. Na CDM hawakujua Rejia angekufa kisha arithiwe na Pareso.
Ushauri wako ni null&void!
 
bona kama huelewi kama iktokea akifa mwingine tayari mrithi anajulikana ila hatuombei iwe hivyo.
 
Nadhani hujafuatilia vizuri process ya kupata wabunge wa viti maalum CHADEMA. Tofauti na vyama vingine vya siasa (ccm included), CHADEMA waliandaa formula ya kupata wabunge wa viti maalum na baadhi ya vigezo vilivyotumika ni elimu, muda wa uanachama etc etc. Potential candidates wote walipitishwa kwenye hilo chekeche na kuwa ranked. Na orodha nzima ilipelekwa kwenye tume ya uchaguzi (NEC) tangu 2010.

Kinachofanyika ni kwa NEC kutoa jina kwa kufuata hiyo orodha. Kwa maana hiyo basi. Marehemu Regia Mtema ni wazi alikuwa ranked juu zaidi ya huyu mrithi wake ndio alipata nafasi hapo awali. Na inapotekea kuwa kuna nafasi iko wazi NEC wanaangalia jina linafuata kwenye orodha.

Nadhani utakuwa umeelewa.

NB: CCM wangetumia mfumo kama huo wangeondoa matatizo mengi sana ya rushwa na malumbano yasiyo na tija. Na nina hakika wangepata wabunge bora kuliko ilivyo sasa ambavyo wamejikuta wana wavaa vipini badala ya 'legislatures' wenye uwezo wa kuchambua miswada.
 
Pengine alitaka wife wake akwae hiyo nafasi. Tumekushtukia.
 
Back
Top Bottom