Je Mrithi wa Regia ilikuwa lazima atoke kasikazini??

Natumaini baada ya maelezo ya wachangiaji mbalimbali ktk uzi huu, wale wakosoaji waliokuwa wamekomaa kuilaumu Chadema bila kufanya utafiti hiyo nafasi inajazwa vipi, watarudi hapa, kuonyesha ukomavu wao wakiri hawakujua utaratibu unaotumika na waombe msamaha...!
Watu tu hamsomi thread na posts za wenzenu. Hili suala Dr Slaa alilitolea ufafanuzi jana.
 
CHADEMA wanaangalia zaidi QUALITY AND NOT QUANTITY. Tulishasema hatumchagui mtu kwa kabila lake wala dini yake na hata anatokea kanda gani. hizo hazina nafasi katika dunia ya werevu. ni mawazo yetu ndo yanauona huo ukaratu but kwangu binafsi naunga mkono ubora wa mtu na si atoka wapi.

Nasuala la kuwahisha kumteua mrithi hata kabla ya maombolezo kuisha unasema je?
 
Amlete wife wake ateuliwe kuwa mpiga kampeni wa Mwigulu Nchemba kuwania kiti kilichowachwa wazi na marehemu Jeremia Sumari.
 
Is an option lakini kama ni hivyo kwani kuna uharaka gani??kwakuwa sheria sawa na za mbunge wa kuchaguliwa!!mbona wakuchaguliwa inachukua hata miezi??sasa kwa mbunge wa viti maalumu wiki??hapana hata ndugu wamarehemu tukienda kwenye arobaini watatunyoshea vidole!!kwa hili sitaacha kusema!
Sheria ni sheria haina option labda ikatungwe upya, ulitaka CDM waanze kampeni ya miezi miwili kutafuta mbunge wa viti maalum? CDM walipeleka majina toka mwaka jana hawakujua Regia atakufa ili anayefuata atoke Karatu, hata hivyo aliyekuwa anafuata alikuwa anatoka Mara akahamia NCCR so what is the problem au sheria inakuwa option linapotokea suala la Chadema?
 
WIKI moja tangu kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Regia Mtema kilipotokea, mchakato wa kumtafuta mrithi wa nafasi yake umeanza.

Regia alifariki dunia Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari katika eneo la Ruvu mkoani Pwani na kuzikwa Jumatano wiki hii nyumbani kwao Ifakara, mkoani Morogoro.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zinasema tayari maofisa husika ndani ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wameanza kushughulikia suala hilo la kuziba nafasi ya mbunge huyo kijana ambaye pia alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Mallaba alisema jana kwamba ofisi yake itatumia orodha ya majina yaliyopendekezwa na Chadema mwishoni mwa mwaka juzi.

“Nadhani tunayo orodha ya mapendekezo ya Chadema, basi kwa jinsi taratibu zilivyo, tutarejea katika orodha hiyo na pale tulipopitisha msitari ndipo tutakapoanzia, lakini lazima huyo anayefuata katika orodha awe na sifa za kuwa mbunge,” alisema Mallaba kupitia simu yake ya kiganjani.

Hata hivyo, Mallaba alisema hivi sasa ni mapema mno kufahamu ni lini uteuzi huo utafanyika na kwamba taratibu za ndani zikikamilika, mamlaka husika zitaarifiwa ili umma pia uweze kufahamu.

Awali, Mallaba alikataa kuonana na waandishi wa habari na mmoja wa maofisa wa Tume hiyo alisema: “Amesema majina yametoka hukohuko Chadema ndipo yakaja huku kwa hiyo kama mnayahitaji mnapaswa kwenda katika ofisi za Chadema ili muweze kupata majina hayo.”

Dk Slaa, Zitto wanena
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa alisema chama chake hakifahamu atakayechukua nafasi hiyo na kwamba hiyo inatokana na ukweli kwamba jukumu hilo liko mikononi mwa NEC.

“Majina ya wagombea wa viti maalumu yapo NEC na wao ndiyo wanaoangalia kuchagua nani anayefuata katika orodha iliyopo Tume, kwa utaratibu, mgombea anayefuata ndiye atakayechukua nafasi hiyo,” alisema Dk Slaa.

Alisema Chadema kilipeleka NEC orodha ya majina 28 ya wabunge wa viti maalumu, Desemba 30, 2010 na kati ya hayo majina 25 tayari wameshachaguliwa ni jukumu la NEC kuangalia jina gani linalofuata kwenye orodha hiyo iliyopo.

Alisema kati ya hayo majina matatu yaliyobaki yeyote atakuwa na uwezo wa kuchukua nafasi hiyo kulingana na vigezo vya NEC na kulingana na utaratibu na Katiba ya Chadema.

“Sina mamlaka ya kujua nani anayefuata na ofisini kwangu hata majina sina majina yapo NEC mimi nawategemea wao waniletee jina kwa mujibu wa taratibu zao nitaliangalia kama muhusika bado ni mwanachama hai nitawajibu na nitawarudishia na ndiyo watalitangaza kwa wananchi,” alisema Dk Slaa.

Alisema kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi, jina watakalopewa kama muhusika atakuwa amefukuzwa katika chama, basi jina litakalofuata baada ya huyo mwanachama ndilo litakaloandikwa na kufanyiwa kazi.

Alisema si rahisi kwa NEC kumtangaza mrithi wa nafasi hiyo bila kuwasiliana kwanza na chama na kuthibitisha kuwa bado ana sifa za kushika nafasi hiyo.

Alisema NEC inajua wazi kuwa haiwezi kumtangaza mtu moja kwa moja pasipo baraka za chama kwa sababu siku hizi kumekuwa na wimbi la migogoro ndani ya vyama vya siasa nchini na wengine kujivua uanachama au kufukuzwa.

Wakati Dk Slaa akisema jukumu hilo ni la NEC, Naibu Katibu wake, Zitto Kabwe alitaja jina la mmoja wa madiwani wa viti maalumu wa chama hicho kuwa ndiye anayefuata katika orodha iliyopelekwa NEC.

Akizungumza jana, Zito alisema kwa mujibu wa orodha yao ya viti maalumu anayefuata baada ya wabunge walioteuliwa mwaka juzi ni diwani huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa.

“Kwa mujibu wa orodha tuliyonayo ya wabunge wa viti maalumu anayefuata baada ya Regia ni diwani kutoka (anataja wilaya na jina lake), ndiye atakayechukua nafasi ya kiti hicho kilichoachwa na marehemu,” alisema Zitto.
 
CHADEMA wanaangalia zaidi QUALITY AND NOT QUANTITY. Tulishasema hatumchagui mtu kwa kabila lake wala dini yake na hata anatokea kanda gani. hizo hazina nafasi katika dunia ya werevu. ni mawazo yetu ndo yanauona huo ukaratu but kwangu binafsi naunga mkono ubora wa mtu na si atoka wapi.

Acha dharau wewe, unataka kusema mikoa mingine hakuna hiyo QUALITY mnayoitaka? Yaani karne hii ya ishirini na moja mnatupakia kwenye gari la ukabila harafu mnataka mpewe nchi kwa kura????? Hii itakuwa ngumu kwenu bana!
 
Ni kweli NEC ndiyo wenye kuteua jina kutokana na ile orodha, na hapa hakuna jinsi ya kubadilisha kama Kakakiiza anavyotaka. kwa upande mwingine CDM watakuwa angalau wamepata somo hapa, safari nyingine hawatateua au kutayarisha orodha kwa kutumia vimemo. nimeshasema sana humu, wengi wa wabunge wa viti maalumu CDM walipatikana kwa vimemo.
 
Mbona unaweka mawazo ya mtoto hapa,panua wigo ktk kufikiri,kwa hiyo watu wa kaskazini wakoje?Mbona ww ni wa kusini na unakwenda kaskazini?Kiongozi ni kiongozi ndugu,atoke magharibi,mashariki au kusini apewaye thamana atutumikie,Endelea na tabia hii ya ubaguzi utafikia kwenye dini,rangi,kabila,jamii fulani,kijiji,tarafa,kata,wilaya,jimbo,mkoa,ukanda fulani,hata vyako utavibagua,kaoge,ule na ukalaleee mtoto mzuri.Acha ubaguzi eeeeeeh mtoto mzuri.
 
Pumba express, watu wauwane kwa lipi? mbona south Africa hakuna uchaguzi wa wabunge na kinachoangaliwa ni idadi ya kura zilizopatikana kwenye uchaguzi wa Rais then chama ndio kinateuwa wabunge wake kinachowataka.
Hiivi watu wenye mtazamo mdogo kama wewe ndio mnataka mje kutuongoza nchi hii?

Labda nimsaidie Ben kujibu. Alichokuwa anataka kusema Ben ni kwamba watu waliokosa kuteuliwa kwenye Orodha ya Viti Maalum inayopelekwa NEC watakuwa wanaombea wenzao waliopata nafasi wafe ili wao wapate nafasi ya kuteuliwa. Si ile dhana ya kwamba watashika Mapanga na Visu wawaue wenzao wa viti maalum waliopo Bungeni.

 
Pumba express, watu wauwane kwa lipi? mbona south Africa hakuna uchaguzi wa wabunge na kinachoangaliwa ni idadi ya kura zilizopatikana kwenye uchaguzi wa Rais then chama ndio kinateuwa wabunge wake kinachowataka.
Hiivi watu wenye mtazamo mdogo kama wewe ndio mnataka mje kutuongoza nchi hii?

Typical reflection of a good fraction of Intellectual dwarfs.....What happened to freedom of expression. It is this attitude of wanting to hear what suits us that breeds sycophants and makes our leaders lie to us.

 
Typical reflection of a good fraction of Intellectual dwarfs.....What happened to freedom of expression. It is this attitude of wanting to hear what suits us that breeds sycophants and makes our leaders lie to us.

Mkuu Ben unakosea unachotakiwa ni kuitetea hoja yako ya watu kuuana kugombea viti maalum na si kumlaumu anayekupinga, kama ni freedom of expression nafikiri iko pande zote.
 
Siyo ulichosikia, huo ndio utaratibu ulivyo na haujaanza leo, kumbuka hata Geturde Lwakatare aliingia bungeni baada yakifo cha Salome Mbatia, na yeye katika ile orodha jina lake ndio lilikuwa linafuatia.
Kumbe huyu Kakakiiza ni sehemu ya vilaza hapa JF? mbona hakuwahi kuhoji kwa nini mkoa wa Morogoro uwe na wabunge wa viti maalum wawili Regia Mtema na Suzan Kiwanga wakati mkoa wa Lindi hauna hata mbunge mmoja wa viti maalum!!?? huku ni kufikiri kwa kutumia kijambio.

haaaah haaah mkuu kweli kabisa kuna watu ni machizi. Jamaa ameleta majungu tu wakati taratibu zinajulikana.
 
Kuna watu ni wakabila sana humu na mleta mada ni mmojawapo. Licha ya kwamba kuna kanuni zilizotumika kumpata mbunge wa kumrithi Regia zilizopo kikatiba, hata hivyo kuna ubaya gani iwapo mbunge mwenye uwezo na mjumbe hai anayejitoa kwa chama amepatikana kaskazini? Kupeana peana kijinga kijinga eti chama kinataka kijijenge Pemba au Lindi au Mtwara hata kama zile sehemu hakuna wajumbe hai wa Chadema hakuna nafasi katika chama makini. Hizo ni sera za CCM za kupeana vyeo kihuni.

Siasa za kuwabeba makundi fulani fulani ya watu bila kuangalia mapenzi yao na uwezo wao wa kukitumikia chama haziwezi kujenga chama husika, zinaendekeza uvivu, zinaendekeza uswahili na hazileti ufanisi. Chadema imekuwa imara leo kwa sera yao ile ile: Wenye uwezo na mapenzi kwa chama ndio watakao jenga chama na taifa kwa ujumla.
 
Dr. Slaa anatoka Karatu, nyie watu wa Mtwara, Ruvuma, Pemba CDM haiwahusu nendeni CUF na CCM

CDM ni chama cha kitaifa acha uzandiki, cha msingi hapo ni kuangalia kama taratibu za chama zimefuatwa na si vinginevyo
 
Ni kweli NEC ndiyo wenye kuteua jina kutokana na ile orodha, na hapa hakuna jinsi ya kubadilisha kama Kakakiiza anavyotaka. kwa upande mwingine CDM watakuwa angalau wamepata somo hapa, safari nyingine hawatateua au kutayarisha orodha kwa kutumia vimemo. nimeshasema sana humu, wengi wa wabunge wa viti maalumu CDM walipatikana kwa vimemo.

muasisi wa vimemo hapa tz ni ccm tangu ilipomteau jk 2005 kila kitu ni vimemo na ushoga(urafiki) serikali ya vimemo ndugu
 
Jamani humu ndani, I mean JF huwa naamini kuwa watu wengi ni waelewa au ni wasomi au hata ni wadadisi wa mambo kidogo. Lakini kuna wakati nashindwa kuamini na hata kuwaelewa baadhi yetu humu lengo na nia la baadhi ya posts ni kitu gani. Hili swala la mbunge wa viti maalumu chama chochote cha siasa kikisha wakilisha orodha ya majina ya watu (hapa niseme wanawake) wanao-qualify kwa vigezo vya chama husika kuwa au kuteuliwa na tume kuwa wabunge wa viti maalumu chama husika hakina tena influence yoyote juu ya jambo hilo bali ni tume ya uchaguzi ndo hutoa orodha ya wabunge wateule kulingana na mgao kwa vyama husika. Ikitokea mbunge wa vitu maalum (hasa wa kundi hilo la wanawake) amefariki tume hutangaza jina la mtu aliyekuwa anafutia katika orodha hiyo bila kujali mtu huyo ametokea upande gani wa nchi. Hii ilishatokea hivi karibuni kwa Salome Mbatia alipofariki kwa ajali ya gari, mtua aliyekuwa anafutia katika orodha ya CCM iliyopelekwa NEC alikuwa ni Getrude Lwakatare (Mchungaji kiongozi, Dr.). Tume wanaangalia aliyefuatia kwenye orodha, na sio vinginevyo, labda anayefuata awe amepoteza sifa kama kufariki, kufukuzwa uanachama au kukoma kuwa mwanachama wa chama husika, n.k. Kwa hiyo chama kama CDM kwa sasa hakina influence yoyote katika jambo hilo. Kama na mimi sijui utaratibu nielimishwe kwa upole na upendo wa kindugu manake JF ndo lengo lake.

Nawasilisha.


Upo sahihi,na umefafanua vizuri! Tatizo,wapo watu ambao hawajui,(sina uhakika kama wanajua kuwa hawajui),lakini hawataki kujua!
Orodha ipo NEC siku nyingi,hata ikipatikana nafasi nyingine,mteule anaefuata anajijua! Orodha hiyo,itatumika mpaka Bunge hili,limalize muda wake!
 
Is an option lakini kama ni hivyo kwani kuna uharaka gani??kwakuwa sheria sawa na za mbunge wa kuchaguliwa!!mbona wakuchaguliwa inachukua hata miezi??sasa kwa mbunge wa viti maalumu wiki??hapana hata ndugu wamarehemu tukienda kwenye arobaini watatunyoshea vidole!!kwa hili sitaacha kusema!



Kakakiiza,
I understand your concern. Lakini napenda tu kukujulisha kuwa swala la kuchagua mrithi wa cdm lipo ndani ya tume. Chadema hawahusiki kwa lolote. Majina yalipelekwa siku nyingi na miongoni mwake ndio tume itamchagua mmoja wao.. Cdm watatakiwa tu kuthibitisha kama bado ni mwanachama wao. Kwahiyo swala ka haraka na kuharakisha ni kwa nec na si cdm.

Kuhusu anapotoka huyo mrithi kwangu mimi sio jamao la msingi. Lamsingi ni kutetea maslahi ya watz wote na kukijenga chama. Awe mzalendo wa kweli na awe tayari kujitoa na kujitolea. Haijalishi ametoka wapi.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom