Je, Mgao wa umeme ndio umeisha?

Leo ni takribani siku ya nne sasa umeme haujakatika sasa najiuliza mgao umeisha au kuna jambo jingine.

ndugu mbona hivyo lakini.... we unataka hawa jamaaa wapite humu waone comment yako... watupige penati ya wiki nzima kwa kosa la kutokutoa taarifa za tatizo la kuwa na umeme 24 hrs kwa siku nne bila kukatika, na kushindwa kutoa taarifa kwao...

mambo mengine unakula KOBISI tu hakuna haja ya kusema...
 
Hahaha!! Mkuu umeniacha hoi, dah ngoja nile kobisi basi lol
 
Kwetu pia tunao toka jumamosi... Leo pia tulikuwa twaulizana kulikoni?...
 
watanzani wamefikia kutia huruma mno.....
yaani mambo ya kawaida kama kutokatika kwa umeme ndio yamekuwa sio ya kawaida...
dah.......
 
Kumbe na wewe umegundua hilo eeeh?

Halafu kuna mijitu juzi juzi tu hapa ilikuwa inampigia makofi ya kinafiki Kikwete kwenye ule mkutano wa DICOTA.

Miafrika tunasikitisha.
 
Kumbe na wewe umegundua hilo eeeh?

Halafu kuna mijitu juzi juzi tu hapa ilikuwa inampigia makofi ya kinafikia Kikwete kwenye ule mkutano wa DICOTA.

Miafrika tunasikitisha.
Hahaha!!! NN hiyo ya DICOTA umenikumbusha watanzania jinsi walivyokuwa wanamsifia Kikwete nikasema mhhhh
 
watanzani wamefikia kutia huruma mno.....
yaani mambo ya kawaida kama kutokatika kwa umeme ndio yamekuwa sio ya kawaida...
dah.......
Boss acha tu yaani kuna mambo ambayo yanaonekana kama vile sio haki yenu kuyapata
 
Leo ni takribani siku ya nne sasa umeme haujakatika sasa najiuliza mgao umeisha au kuna jambo jingine.
Haujaisha walikuwa wanataka muendelee kuona sakata la Igunga halafu mlijadili kwa mapana na marefu huku wao wakiendelea kula raha ndio nchi yetu na ccm yake.
 
Duh hatari kubwa tangu Jmosi umeme haujakatika nikajiuliza labda kuna mkubwa kaja Arusha ngoja nikalipie DStv.
 
Hahaha!!! Ngongo banaa kutakuwa kuna kitu eheee si kawaida kabisa mkuu unaenda kulipia DSTV halafu wanaukata
 
Mkuu wangu kabla sijalipia napita TANESCO kuna jamaa zangu pale lazima watanipa nondo za uhakika.

Back
Top Bottom